MissTz 2010: Mrembo kakosa umiss kwa kujibu vibaya

Watu walifanya makosa sana kumzomea binti.......

Aisifiaye Mvua jamani. Inawezekana binti alishapelekeshwa ALL NIGHT LONG.

Kutoka siku hiyo akajua Mkwere ni Mchapa fiMbo......ahhaaa samahani mchapa kazi safi sana.

Sasa mlitaka amsifie Slaa? Hata Mzee Kenyantta alijisifu "Wanaosema mie Mzee, muulizeni Mama Ngina".

du hii kali tunaomba clip jamani tuijadili kama ile ya kifaduro........

as of binti kuwa ameshakanyagwa that may be true...lakini kama mtu kusimama juani tu anaanguka..basi tumuombee Mungu yasijemtokea ya Sani Abacha.najuwa ikitokea wata cover up....mnajuwa pia inawezekana ikawa PR move...maana nijuavyo haya maswali huwa wanapewa kabla....sasa inawezekana walidhani angejibu angepigiwa makofi...na wangekuwa tayari wamepata boost...but that is message sent ...maana watu waliokuwa wakiangalia ni wengi sana......
 
Wadau kwa walifuatilia Miss TZ; kakosa UMISS dada niliyemuona kustahili ila katika jibu lake kaweka jina la JK na kumsifia; hivyo ukumbi badala ya kumshangilia ukamzomea? Mliokuwepo hapo ebu tujuzeni

nenda kwenye ile idara ya uchaguzi tayari watu wameshaanza kutupa mawe...bila soo...huyu binyi atapoozwa na JK kwa kuzomewa kwa ajili yake.....atapewa "haki yake""......na angeshinda watu wangerusha viti....

tukisema kina lundenga wamekosa Moral authority ya kuandaa haya mashindano muelewe ...kazi yake kuwauza mabinti za watu kwa hawa wanaowasifia na ma PDG......ndio maana kila mwaka wanavuna aibu.....nadhani watu kama Maria Sarungi na Mustapha Hassanali..,khadika mwanamboka..,Idarious na wengine waki team up wanaweza kuandaa mashindano yenye heshima ....naona kama mashindano anayoandaaga Maria hayajawahi kukumbwa na kashfa.....
hiyo sababu kuwa eti kina lundenga wana haki ya kutumia jina MIss tanzania ni crap....kwani Tanzania ni yetu wote......waondoke na LINO AGENCY yao ..kampuni ya kuuza mabinti kwa wakubwa!!!...wewe jiulize kampuni ina event moja kwa mwaka inajiendeshaje...kama si danguro hilo...???
 
Kwa kweli jana nilifurahi sana pale ukumbini, kwani yule binti hakuelewa upepo ulivyo alijiaribia sana kwani watu walimzomea kwa dakika nzima na hawakunyamaza hadi swali jingine lilipoulizwa, msg sent to Revolutionary Party.
 
nenda kwenye ile idara ya uchaguzi tayari watu wameshaanza kutupa mawe...bila soo...huyu binyi atapoozwa na JK kwa kuzomewa kwa ajili yake.....atapewa "haki yake""......na angeshinda watu wangerusha viti....

tukisema kina lundenga wamekosa Moral authority ya kuandaa haya mashindano muelewe ...kazi yake kuwauza mabinti za watu kwa hawa wanaowasifia na ma PDG......ndio maana kila mwaka wanavuna aibu.....nadhani watu kama Maria Sarungi na Mustapha Hassanali..,khadika mwanamboka..,Idarious na wengine waki team up wanaweza kuandaa mashindano yenye heshima ....naona kama mashindano anayoandaaga Maria hayajawahi kukumbwa na kashfa.....
hiyo sababu kuwa eti kina lundenga wana haki ya kutumia jina MIss tanzania ni crap....kwani Tanzania ni yetu wote......waondoke na LINO AGENCY yao ..kampuni ya kuuza mabinti kwa wakubwa!!!...wewe jiulize kampuni ina event moja kwa mwaka inajiendeshaje...kama si danguro hilo...???
i couldnt agree with you more.... Hashim hata ile caliber tu hana, let alone morals nk.sijui dini yake inamruhusu?

natafuta website ya miss tanzania jamani ipo?
 
Jamani mi nilikuwepo kilichowaudhi wengi ni kuchanganya siasa na burudani iliyotupeleka pale hata angemtaja Slaa angezomewa,watu tunaenda kwenye kumbi za starehe kupumzisha akili baada ya uchaguzi kutawala TV,redio,magazeti,mabango etc.

Uporoto ni mpotoshaji mkubwa, wote tulikuwepo na tuliona kilichotokea! Sisiem wataendelea kujiimanisha lakini ukweli utabakia. "Watz wameichoka ccm, wamemchoka Kikwete. Swali lenyewe lilikuwa la kisiasa na watu hawakuzomea wakati akiulizwa. Walimsikiliza kwa makini na sifa alizokuwa akizitaja ni kama alikuwa akimsema Dk Slaa maana alisema anataka Kiongozi makini, Kiongozi mchapakazi na jasiri, anamtaka kiongozi mzalendo anayependa nchi yake, wakati huo watu kimyaa wakimsikiliza. Akaendelea, " ninamtaka kiongozi atakayetuletea maendeleo kama rais Jakaya Kikwete! hapo watu wakaanza kuzomea na kuonyesha kukerwa na mrembo huyo. hayo yametokea mbele ya Ridhwan mwanaye Kikwete, Rostam Azizi mshirika wake kwenye ufisadi na watu wengine wengi ambao wamekuwa wakimsaidia!!! Looool, CCM inapoteza umaarufu kwa kasi ya ajabu. Hivi star TV hawakukata kweli matangazo kuwa wapenda sanaa ya urembo, wametukana???
Kama hili lilionekana kwenye TV nchi nzima, basi sisiem wameipata aibu ya mwaka
 
jana niliamini, kweli watu hawampendi jk

..na anavyopenda kupendwa...lazima alikuwa anaangalia LIVE maana kabla hajawa rais alikuwa hakosagi kuhudhuria......,nadhani ka presha kalimpanda baada ya tukio la jana......unajuwa they are really miscalculating where to make there PR..Watu wana hasira...yet kila wanapopita ni mabango tu yanaytokana na PAYE zetu...tukiyaona tunazidi kupata hasira..yet watu wanaingia ukumbini kwa kiingilio chao...unawaletea mambo ya kujitangaza ....shwine!!
 
Sisiem imepoteza mvuto kwa watz siyo siri. wale tuliokuwepo mahala pale tuliona jinsi maswahiba wake Kikwete walivo inamisha vichwa vyao baada ya ile zomea. Mrembo yule hakusoma nyakati, hakujua kuwa sisiem haikubaliki tena. Alifikiri kwa kumtaja Kikwete atapata maksi za bwelele kumbe watz hawataki tena. Tukio Lile ulikuwa ni ujumbe tosha kwa wanaoshabikia chama cha mafisadi
 
Hilo swali lilikuwa planned makusudi na UWT kupitia kwa Ludenga kumkampenia JK bila kujua kuwa walikuwa wanafanya kosa limewarudi wao.
 
nilishuhudia mdau. Dada yule kazomewa mpaka karibu aanguke. Hapo ndo utajua watz wamemchoka jk
 
Uporoto ni mpotoshaji mkubwa, wote tulikuwepo na tuliona kilichotokea! Sisiem wataendelea kujiimanisha lakini ukweli utabakia. "Watz wameichoka ccm, wamemchoka Kikwete. Swali lenyewe lilikuwa la kisiasa na watu hawakuzomea wakati akiulizwa. Walimsikiliza kwa makini na sifa alizokuwa akizitaja ni kama alikuwa akimsema Dk Slaa maana alisema anataka Kiongozi makini, Kiongozi mchapakazi na jasiri, anamtaka kiongozi mzalendo anayependa nchi yake, wakati huo watu kimyaa wakimsikiliza. Akaendelea, " ninamtaka kiongozi atakayetuletea maendeleo kama rais Jakaya Kikwete! hapo watu wakaanza kuzomea na kuonyesha kukerwa na mrembo huyo. hayo yametokea mbele ya Ridhwan mwanaye Kikwete, Rostam Azizi mshirika wake kwenye ufisadi na watu wengine wengi ambao wamekuwa wakimsaidia!!! Looool, CCM inapoteza umaarufu kwa kasi ya ajabu. Hivi star TV hawakukata kweli matangazo kuwa wapenda sanaa ya urembo, wametukana???
Kama hili lilionekana kwenye TV nchi nzima, basi sisiem wameipata aibu ya mwaka

habari ndiyo hiyo miye naamini kuwa waliohudhuria hayo mashindano ya mamiss jana idadi kubwa si maamuma ni watu na akili zao kamili,
wanajua nini kimewapeleka pale, kwa mwenye akili na kukili kuwa kweli jambo lile limeonesha kuwa wengi wa watz wameichoka ccm na mgombea wake hawawezi kutetea kule kuzomea eti walizomea siasa kwenye burudani, huo ni mtazamo na utetezi mfu
 
Hilo swali lilikuwa planned makusudi na UWT kupitia kwa Ludenga kumkampenia JK bila kujua kuwa walikuwa wanafanya kosa limewarudi wao.
heheeeeee eeee heeeeee!!! mimi huku mwenzenu ahahhaaaaaaaa ccm ziiiiii, kweli hiyo ni nzuri riziii wanii si atakuwa alikimbia? ama hakwepo
 
akose vipi wakati ..voda ni mdhamini na wao ni share holders??? na bado tutawakimbiza mwaka huu ......mafidadi wanafiki ...lazima tuwapekeke KISUTU...watueleze wamewezaje kujenga ndani ya miaka mitano ...nyumba za kifahari mikocheni,masaki,bagamoyo,na kijiji cha majumba cha MSOGA....

pia watueleze yale magorofa wanayojengewa na subash kule hindu mandal area na maeneo mengine..pesa zimetoka wapi........au kama ni malipo ya kuitoa mchuchuma bure ....na buzwagi pia tuambiwe.......nachukia sana watu wanaojifanya wanapinga ufisadi mchana wakati usiku wanakula nao......
 
heheeeeee eeee heeeeee!!! mimi huku mwenzenu ahahhaaaaaaaa ccm ziiiiii, kweli hiyo ni nzuri riziii wanii si atakuwa alikimbia? ama hakwepo
Wote walikuwepo hata Rostam alikuwepo! ilikuwa ni aibu kubwa. Siku tatu kabla ya jana Ridhwan na kikundi cha vijana wa ccm wanaojitangaza kumuunga mkono rais kikwete kilitembelea kambi ya warembo kwenda kuuza sura zao na ujinga wa CCm. wako warembo walio wachora na kuwaona kama wakware tu. nafikiri lile swali lilitungwa na Ridhwan na kundi lake wakidhani lingemjenga Kikwete. Hawakujua kuwa watz hawadanganyiki tena.
 
dah! hiyo imetulia sana, tatizo huyo rizii wanii hasomi alama za nyakati kutokana na kuwa na upeo mdogo wa kupembua mambo,
amelivaa aibu la mwaka sasa, nadhani akimsimuli babaye basi ni dhahili kaanguka huko aliko
 
Baada ya kuzomewa yule mrembo nilitegemea matangazo yangekatishwa ghafla lakini bahati nzuri yalikuwa yanarushwa na StarTv na sio TBC1.
 
Wamemuonea binti wa watu bure, watu inabidi tujifunze kuweka ushabiki na unazi wetu in check. Tusipeleke hisia zetu za siasa katika kila kitu ni lazima tuheshimu uhuru na maoni ya watu hata kama tunapingana nayo maana huu ndio ukomavu hasa wa mwanadamu.
 
Lile swali lilikuwa unfair na halikustahili kuwepo kwenye orodha ya maswali.Mabinti wale huenda hata hawazijui vizuri siasa za upinzani na hivyo ilikuwa rahisi sana kwa binti kujikuta akiingia kwenye mtego wa kumshabikia "rais wake aliyeko madarakani".
Binti alianza vizuri sana kwa kueleza vigezo vyake yeye vya kiongozi atakaemfaa na atakayempa kura zake. Baada ya kuelezea vema tena kwa ufasaha na kuona anashangaliwa akawa carried away na kuongezea kuwa huyo ni...........JK..... hapo ndipo alipokumbana na ghadhabu za wananchi wenye mtizamo tofauti.... ZOMEAAA kwenda mbele.Kweli ilisikitisha,lakini kosa ni la waandaaji kwani hata kama ndio msimamo wa binti... haukupaswa kujulikana bayana kwenye ile hadhira yenye watu wenye itikadi mchanganyiko.
 
Tusipeleke shutuma kwa watu wengine, waliozomea si waandaaji bali ni wahudhuriaji wa mashindano wa yale na ni hao ndio waliomfanyia makosa binti wa watu kwa kushindwa kuheshimu huru wake wa maoni. Kama ingekuwa tunazomeana kila wakati mtu anaposema jambo tusiloafikiana nalo basi huku mitaani kungekuwa hakuishiki maana ingekuwa ni makelele tu.

Swali lile lilikuwa very balanced na hata dhamira yake ya kupima uwezo wa warembo wetu katika ufahamu wao wa maswala nyeti yanayoigusa jamii kwa sasa.

Heshima ni kitu muhimu sana katika maisha ya wanadamu na ni bure pia.
 
Back
Top Bottom