MissTz 2010: Mrembo kakosa umiss kwa kujibu vibaya

MissTz 2010: Mrembo kakosa umiss kwa kujibu vibaya

swali lingekuwa ataje sifa za Rais anayefaa kuongoza, na majibu yake ingekuwa kutoa sifa tu na si kutaja majina. hii ingekuwa ni katika kuelimisha umma na mwishowe mtu achague amtakaye. nafikiri ilikuwa kosa kutaja Jina

lakini General Knowlege kwa vijana wengi ni tatizo kubwa, tumeona katika mashindano mbalimbali mf. yale ya kushindanisha vijana wa vyuoni nk yanayodhaminiwa na zain kwa nchi za east africa. Jamii haijawa na mwelekeo huo wa kuwafunza vijana
 
Wote walikuwepo hata Rostam alikuwepo! ilikuwa ni aibu kubwa. Siku tatu kabla ya jana Ridhwan na kikundi cha vijana wa ccm wanaojitangaza kumuunga mkono rais kikwete kilitembelea kambi ya warembo kwenda kuuza sura zao na ujinga wa CCm. wako warembo walio wachora na kuwaona kama wakware tu. nafikiri lile swali lilitungwa na Ridhwan na kundi lake wakidhani lingemjenga Kikwete. Hawakujua kuwa watz hawadanganyiki tena.

Huyu dogo sidhani kama akili yake inakua au kudumaa. Nadhani kiwango cha kufikiri kwake kiko chini ya kile cha baba yake.
 
Ila ukweli unaonekana,mkubali mkatae,JK ni mchapazi.
Fainali ni Oktoba,31.

mtiwadawa,
Elewa kuwa kuna totafuti ya kuchapa kazi (usiku kucha) kwa ufanisi na kushindwa kulala kwa matatizo ya ki-afya. JK ni mhathirika wa hili la pili kutokana na athari za kulindika madawa ya kupunguza maumuvu. Hili ndo jawabu la JK kukesha ofisini anapotembelea wizara. Hakuna cha kuchapa wala kupiga kazi. Kazi inapimwa kwa tija na ufanisi wala si porojo, ahadi mpya, takwimu za kupika n.k
 
Nadhani binti amejifunza, na amewasaidia mabinti wa umri na kaliba yake waliojiandikisha kupiga kura kuelewa taifa linataka nini. Naamini wakati wa kupiga kura watakumbuka zomea zomea
 
CCM is a bIG Party, chama cha mapinduzi

Mapinduzi ya kiuchumi

Mapinduzi ya kifkra

Mapinduzi ya Elimu

Mapinduzi ya Kilimo

Mapinduzi ya Afya

Mapinduzi ya kidemokrasia

Mapinduzi ya Utamaduni na Michezo

Mapinduzi ya Viwanda

Mapinduzi ......



na Katu si Chama cha kuwaweka watanzania kwenye DEMA, si chama cha mitego
 
Huyo ni KIJANA! Hana habari na kinachoendelea anaimba wimbo ule ule maarufu wa TOT! Vijana wetu hawana vuguvugu la kimapinduzi wanataka status quo! Ni conservatives! Yaani hata bila ya kusita ungetegemea vijana, na hasa kwa kuona kinachoendelea wangekuwa wanatamani kitu kingine, lakini ppppppppppppppppppppooohh, ila hawa sio wale wanaotembea uchi ufukoni wakiwa na baba zao!?
 
Mimi nadhani alishajibu swali kwamba atamchagua rais mchapakazi. Labda mniambie ni kosa kujibu swali kwa kutoa mfano.
 
CCM is a bIG Party, chama cha mapinduzi

Mapinduzi ya kiuchumi

Mapinduzi ya kifkra

Mapinduzi ya Elimu

Mapinduzi ya Kilimo

Mapinduzi ya Afya

Mapinduzi ya kidemokrasia

Mapinduzi ya Utamaduni na Michezo

Mapinduzi ya Viwanda

Mapinduzi ......



na Katu si Chama cha kuwaweka watanzania kwenye DEMA, si chama cha mitego

Una akili sana mkuu. Hongera sana ...kwa kuchanganya na zako
 
Mhhh haya lakini ujumbe umefika mwenye sikio na asikie:glasses-nerdy:
 
Una akili sana mkuu. Hongera sana ...kwa kuchanganya na zako

Upupu huo. nyinyi mnaendelea kusambaza upupu na kushindwa kujipanga na kujibu hoja. Watu wanakuzomeeni nyinyi mnaona ni ushabiki, wanawaambia mfalme hajavaa nguo, nyinyi mnaona anatukanwa, mna ambiwa watanzania wamebadilika nyinyi mnaimba chama cha mapinduzi na kujipongeza, shauri yenu mtakapo kuta mwana si wenu! Mnaambiwa mwende kwenye midahalo mseme mlichofanya na kile ambacho mnategemea kuwafanyia wananchi nyinyi mnakacha na kusema si lazima, shauri yenu! kwa nini hamtaki kujibu hoja kwa hoja? kwa nini mnakimbilia siasa za maji taka na mipasho tu? yetu macho, 31 octoba si mbali. Jana amezomewa binti yule kwa kusema kikwete ni mchapakazi kwenye ukumbi alimo mwanaye, kesho atazomewa chumbani aliko mkewe. Subiri utaona
 
CCM is a bIG Party, chama cha mapinduzi

Mapinduzi ya kiuchumi

Mapinduzi ya kifkra

Mapinduzi ya Elimu

Mapinduzi ya Kilimo

Mapinduzi ya Afya

Mapinduzi ya kidemokrasia

Mapinduzi ya Utamaduni na Michezo

Mapinduzi ya Viwanda

Mapinduzi ......



na Katu si Chama cha kuwaweka watanzania kwenye DEMA, si chama cha mitego
Na Mapinduzi ya Wizi pia
 
Watu walifanya makosa sana kumzomea binti.......

Aisifiaye Mvua jamani. Inawezekana binti alishapelekeshwa ALL NIGHT LONG.

Kutoka siku hiyo akajua Mkwere ni Mchapa fiMbo......ahhaaa samahani mchapa kazi safi sana.


Sasa mlitaka amsifie Slaa? Hata Mzee Kenyantta alijisifu "Wanaosema mie Mzee, muulizeni Mama Ngina".
Sikonge ilikuwa ni kichekesho sana,ukweli iilibidi tuzomee,bi dada kajitutumua kumnadi mgombea wake,kilichofuata kitabaki ktk kumbukumbu zake!
 
dah! hiyo imetulia sana, tatizo huyo rizii wanii hasomi alama za nyakati kutokana na kuwa na upeo mdogo wa kupembua mambo,
amelivaa aibu la mwaka sasa, nadhani akimsimuli babaye basi ni dhahili kaanguka huko aliko
Hahitaji kusimuliwa,kitu ilikuwa LIVE Star TV,na hawakukata matangazo kama wale TBC!
 
Jamani mi nilikuwepo kilichowaudhi wengi ni kuchanganya siasa na burudani iliyotupeleka pale hata angemtaja Slaa angezomewa,watu tunaenda kwenye kumbi za starehe kupumzisha akili baada ya uchaguzi kutawala TV,redio,magazeti,mabango etc.

mjomba acha kujing'ata. tunawajua CCM hodari wa kugeuza hasi kuwa chanya.

Bashe si raia. Sasa hivi ni raia.
Masha kapita bila kupingwa. Sasa hivi kapata mpinzani.

Watu walizomea baada ya yule binti kuanza kujikomba kwa JK. Yeye mwenyewe anajua watu walizomea.

kwa hiyo wewe hatukuelewi na chai zako.

Kikwete hakubaliki. Kitakacho muokoa mwaka huu ni WIZI WA KURA TU.
 
Na nyie mnaenda kuangalia vichupi vya wasichana, naona mliona wivu wa JK kusifiwa? Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.

Inaelekea wote nyie ni wapenda watoto pamoja na huyo JK wenu.
 
Naombeni niulize. Niliwahi kusikia kwamba yale maswali huwa si mageni, utaratibu ni kwamba warembo huwa wanayapitia maswali na majibu yake, na mrembo ataulizwa maswali kadhaa kutoka katika yale mengi waliyokwishapewa wayapitie (ikiwa pamoja na majibu yake). Kwa hiyo mtihani huwa ni namna ya kukumbuka majibu na kuyaelezea. Sasa swali langu ni hili, je, ina maana alipoulizwa swali hilo, hata jibu lake wakati wa maandalizi aliambiwa aseme atamchagua JK?
 
Ndiba, umenichekesha sana, You've made my day..haahhahaha

Baada ya kuzomewa yule mrembo nilitegemea matangazo yangekatishwa ghafla lakini bahati nzuri yalikuwa yanarushwa na StarTv na sio TBC1.
 
Wamemuonea binti wa watu bure, watu inabidi tujifunze kuweka ushabiki na unazi wetu in check. Tusipeleke hisia zetu za siasa katika kila kitu ni lazima tuheshimu uhuru na maoni ya watu hata kama tunapingana nayo maana huu ndio ukomavu hasa wa mwanadamu.

akina nani? mbona hujawa specific na swali lako, walio mzomea? ama waliompa swali la namna hiyo?

NB: uhuru wa maoni haina maana kukubariana na kila kitu eti kwa sababu ya kuheshimu uhuru huo,
maana mpaka hapo wewe pia hujaheshimu uhuru wa maoni ya kuzomewa kwa bi dada huyo, kipofu wa nyakati
 
Wamemuonea binti wa watu bure, watu inabidi tujifunze kuweka ushabiki na unazi wetu in check. Tusipeleke hisia zetu za siasa katika kila kitu ni lazima tuheshimu uhuru na maoni ya watu hata kama tunapingana nayo maana huu ndio ukomavu hasa wa mwanadamu.

Na wewe unawaonea wazomeaji bure kwani Hata Kuzomea ni maoni ya watu na ni Lazima Kuheshimiwe vile
 
Tusipeleke shutuma kwa watu wengine, waliozomea si waandaaji bali ni wahudhuriaji wa mashindano wa yale na ni hao ndio waliomfanyia makosa binti wa watu kwa kushindwa kuheshimu huru wake wa maoni. Kama ingekuwa tunazomeana kila wakati mtu anaposema jambo tusiloafikiana nalo basi huku mitaani kungekuwa hakuishiki maana ingekuwa ni makelele tu.

Swali lile lilikuwa very balanced na hata dhamira yake ya kupima uwezo wa warembo wetu katika ufahamu wao wa maswala nyeti yanayoigusa jamii kwa sasa.

Heshima ni kitu muhimu sana katika maisha ya wanadamu na ni bure pia.

ULICHOKISEMA hapo kwenye bold ni sahihi kabisa ila kwangu mimi bado nitasimamia maoni yangu kuwa lile swali halikuwa zuri kwa vigezo vyovyote vile kwenye yale mashindano. Binafsi nilisikitika pale walipomzomea binti wa watu...na hata baadhi ya watu walihisi hivyo hivyo. Kile kitendo cha kuzomewa huenda ..nasema huenda kiliathiri hata maoni ya majaji. Mzoemeo ule haukuwa mdogo eti!Utadhanii ukumbi mzima ulizomea.
 
Back
Top Bottom