Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ila ukweli unaonekana,mkubali mkatae,JK ni mchapazi.
Fainali ni Oktoba,31.
Swali lilikuwa AINA ya rais alitakiwa kujibu sifa ambazo Rais huyo awe nazo ili amchague hajaulizwa nani.
hakika Tanzania bila ccm inawezekana
Mchapazi ni mtu wa aina gani? Mshirikina?
Huyo dada labda alimaanisha maneno ya Salma kazi ya shuka kwa shuka!
Basi hawafai kuipeperusha bendera ya nchi yetu kama hata hawaelewi nini kinaendelea.Na yule binti ni wa chuo kikuu,utasema vipi alionewa kupewa lile swali?Lile swali lilikuwa unfair na halikustahili kuwepo kwenye orodha ya maswali.Mabinti wale huenda hata hawazijui vizuri siasa za upinzani na hivyo ilikuwa rahisi sana kwa binti kujikuta akiingia kwenye mtego wa kumshabikia "rais wake aliyeko madarakani".
Binti alianza vizuri sana kwa kueleza vigezo vyake yeye vya kiongozi atakaemfaa na atakayempa kura zake. Baada ya kuelezea vema tena kwa ufasaha na kuona anashangaliwa akawa carried away na kuongezea kuwa huyo ni...........JK..... hapo ndipo alipokumbana na ghadhabu za wananchi wenye mtizamo tofauti.... ZOMEAAA kwenda mbele.Kweli ilisikitisha,lakini kosa ni la waandaaji kwani hata kama ndio msimamo wa binti... haukupaswa kujulikana bayana kwenye ile hadhira yenye watu wenye itikadi mchanganyiko.
Kwani hiyo siyo siasa??? Mbona hawakuzomea??. Mbona unamacho lakini huoni?, Unamasikio lakini Husikii?? Ewe mtanzania ni nani aliyekuroga??
Umemuelewa lakini uliyem quote?Upupu huo. nyinyi mnaendelea kusambaza upupu na kushindwa kujipanga na kujibu hoja. Watu wanakuzomeeni nyinyi mnaona ni ushabiki, wanawaambia mfalme hajavaa nguo, nyinyi mnaona anatukanwa, mna ambiwa watanzania wamebadilika nyinyi mnaimba chama cha mapinduzi na kujipongeza, shauri yenu mtakapo kuta mwana si wenu! Mnaambiwa mwende kwenye midahalo mseme mlichofanya na kile ambacho mnategemea kuwafanyia wananchi nyinyi mnakacha na kusema si lazima, shauri yenu! kwa nini hamtaki kujibu hoja kwa hoja? kwa nini mnakimbilia siasa za maji taka na mipasho tu? yetu macho, 31 octoba si mbali. Jana amezomewa binti yule kwa kusema kikwete ni mchapakazi kwenye ukumbi alimo mwanaye, kesho atazomewa chumbani aliko mkewe. Subiri utaona
Kweli kabisa,na binti alikuwa na bahati ya kuulizwa moja kati ya maswali rahisi na zuri mno,na alianza vizuri; tatizo ni kuwa hawa ndo mamiss wa nykati hizi!!!Kwa mtazamano wangu naona lile swali lilikuwa sahihi kabisa kuulizwa pale na kwa vile sasa tuko katika mchakato wa uchaguzi .tatizo aliyejibu IQ yake ilikuwa ndogo sana hakujua atoe jibu gani ndio maana kabakia kubwatuka .Maskini nilijikuta namuhurumia badala ya kumsikitikia.
Alikuwa na haki ya kulijibu kwa umakini kabisa ama kutokulijibu akieleza sababu gani zinazomfanya asijibu.
Ila kwa ujumla Miss Tanzania ya mwaka huu haikuwa na mvuto hata kidogo.
Kwa mtazamano wangu naona lile swali lilikuwa sahihi kabisa kuulizwa pale na kwa vile sasa tuko katika mchakato wa uchaguzi .tatizo aliyejibu IQ yake ilikuwa ndogo sana hakujua atoe jibu gani ndio maana kabakia kubwatuka .Maskini nilijikuta namuhurumia badala ya kumsikitikia.
Alikuwa na haki ya kulijibu kwa umakini kabisa ama kutokulijibu akieleza sababu gani zinazomfanya asijibu.
Ila kwa ujumla Miss Tanzania ya mwaka huu haikuwa na mvuto hata kidogo.
Nadhani upo sahihi; na hapo ndipo mrembo huyo amemsaidia El Sahaf (makamba) kujiuliza kama ni mtaji au la. Kaisaidia REDET na Synovate pia!My Take: Nani kasema kajibu vibaya? Kujibu vizuri au vibaya na kuzomewa ni vitu viwili tofauti. nafikiri tunahitaji tafakari zaidi katika kuchangia. Binafsi sioni ubaya kwa yeye kujimtaja JK (ama hata kama angekuwa mwingine yeyote) kama mchapakazi kwa kadri anavyoona yeye. Tatizo naona watu tumeanza kuhamanika na siasa na kuacha kutafakari
Watu walifanya makosa sana kumzomea binti.......
Aisifiaye Mvua jamani. Inawezekana binti alishapelekeshwa ALL NIGHT LONG.
Kutoka siku hiyo akajua Mkwere ni Mchapa fiMbo......ahhaaa samahani mchapa kazi safi sana.
Sasa mlitaka amsifie Slaa? Hata Mzee Kenyantta alijisifu "Wanaosema mie Mzee, muulizeni Mama Ngina".