MissTz 2010: Mrembo kakosa umiss kwa kujibu vibaya

yule dada ovyo sana kuna namna nyingi za kujibu swali lile tena lilikuwa open

yeye akabwatuka na kutaja jina la mgonjwa wa kifafa
ni dhahiri kuwa haifa
 
when politics rule. nothing can stand before it.
 
Swali lilikuwa AINA ya rais alitakiwa kujibu sifa ambazo Rais huyo awe nazo ili amchague hajaulizwa nani.

Kwani hiyo siyo siasa??? Mbona hawakuzomea??. Mbona unamacho lakini huoni?, Unamasikio lakini Husikii?? Ewe mtanzania ni nani aliyekuroga??
 
Basi hawafai kuipeperusha bendera ya nchi yetu kama hata hawaelewi nini kinaendelea.Na yule binti ni wa chuo kikuu,utasema vipi alionewa kupewa lile swali?
 
Kwani hiyo siyo siasa??? Mbona hawakuzomea??. Mbona unamacho lakini huoni?, Unamasikio lakini Husikii?? Ewe mtanzania ni nani aliyekuroga??

Kwa mtazamano wangu naona lile swali lilikuwa sahihi kabisa kuulizwa pale na kwa vile sasa tuko katika mchakato wa uchaguzi .tatizo aliyejibu IQ yake ilikuwa ndogo sana hakujua atoe jibu gani ndio maana kabakia kubwatuka .Maskini nilijikuta namuhurumia badala ya kumsikitikia.
Alikuwa na haki ya kulijibu kwa umakini kabisa ama kutokulijibu akieleza sababu gani zinazomfanya asijibu.
Ila kwa ujumla Miss Tanzania ya mwaka huu haikuwa na mvuto hata kidogo.
 
tatizo sio kumpigia kampeni jk tatizo ni wakati gani wa kufanya hivyo na kwa kiwango chake cha elimu kweli yule mrembo anatumia kamasi kufikiri.au kaambiwa ukimrusha kidogo tu jk basi unapata ukuu wa wilaye manake jk haeleweki.
 
Umemuelewa lakini uliyem quote?
 
Suala lilikuwa halali, na jibu pia lilikuwa halali (kama tutalitizama kama limeweza kujibu suala lililoulizwa au la).

Tatizo ni kuwa jibu halikuwapendeza wahudhuriaji, sio kuwa jibu lilikuwa na makosa.
 
Kweli kabisa,na binti alikuwa na bahati ya kuulizwa moja kati ya maswali rahisi na zuri mno,na alianza vizuri; tatizo ni kuwa hawa ndo mamiss wa nykati hizi!!!
 

hapo mpendwa hebu tufahamishe IQ ni ndogo kivipi?
 
Nadhani upo sahihi; na hapo ndipo mrembo huyo amemsaidia El Sahaf (makamba) kujiuliza kama ni mtaji au la. Kaisaidia REDET na Synovate pia!
 
Jamani,hebu tufikirie wengi wetu tulipokuwa kidato cha 6 tungekuwa na uwezo wa kujibu maswali yale na confidence kwenye watu wengi namna ile? Tuwe wakweli jamani, chonde chonde,wengine humu mnataka ajibu kama mtu aliyemaliza chuo kikuuu na ma experience kibao. Kwani na nyinyi si mnao dada,watoto wenu etc wenye elimu na umri huo?Waulizeni swali hilo x 2, muone mtakavyoshangaaa. Ameshindwa basi.lakini uwezo wake uliishia pale na wala si wa kumlaumu saaaaana,si ajabu wangeulizwa wote wale tofauti ingekuwa ndogo sana kwenye kujibu swali lile,
 

Aisifaye mvua imemnyea... Na Mzee mkwere si ndio zake? Masikini binti huyo... Angejua...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…