Misururu ya magari kwenye misafara ya ziara za viongozi wetu ni ushamba wa kizamani sana!

Kila mtu na urefu wa kamba yake.
 
Msururu wa magari 50 weka mafutaaa..weka PER DM hapo ndo utajua afrika tuna laana hizo gharama za mafuta na per DM zinaweza fika gharama za mradi husikaaa
 
Kuna kiongozi simjui Ila anapitaga yeye tu na dereva wake na Gari ni ndogo Ila vimwakumwaku vya Polisi kuonyesha huyu anaepita ni kiongozi sio hio mi LC300 halafu safi Ila dereva wake ana kazi 2 kumlinda kiongozi na kuendesha Gari maana hakuna ulinzi
 
Na wengine utawaona wamezungukwa na maaskari wakiwa na mabunduki utafikiri nchi ipo vitani! Lakini hayo huwezi kuyaona kwa viongozi wa nchi zilizoendelea kama USA,UK,France au Germany,yote ni kwa sababu ya kujikweza,kupenda utukufu na ulimbukeni tu.
 
Naunga mkono hoja
P
 
Leo kwenye follen barabara ya Bagamoyo niliona gari inapiga king'ora ili ipishwe, nyuma ni "W" , nauliza nae waziri ana king'ora?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…