Mita mpya za maji ni kama king’amuzi, maji yakiisha inaji-lock

Mita mpya za maji ni kama king’amuzi, maji yakiisha inaji-lock

MR LINKO

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2016
Posts
3,034
Reaction score
3,526
Dn-20-IC-Card-Prepaid-Water-Meter-Smart-Water-Meter96665.jpg

Serikali kupitia Wizara ya Maji kuanzia mwezi Julai inatarajia kuanza kufunga mita za maji za malipo ya kabla[PRE PAID WATER METERS] ambazo zitakuwa na mfumo wa King’amuzi unaweza ukanunua ukiwa sehemu yoyote duniani

Katibu mkuu Wizara ya Maji mhandisi Antony Sanga amesema utofauti wa mita hizo na mita zingine ni kuwa unaweza ukamgawia jirani uniti za maji kama unavyohamisha salio kwenye simu na akaendelea kupata huduma, vilevile kama unahama nyumba uliyokua ukiishi na kuna uniti zako zimebaki kwenye mita unaweza ukahama nazo pia.
 
Hili ndilo litakuwa mwarobaini wa tatizo la kubambikiana Bills! Unatumia maji ya 3000 unapewa bill ya 12000
Litasaidia pia kuepusha visasi. Kuna jamaa wa idara ya maji tulishwahi kuzinguana naye home, atatubandika bill ya laki 6 na maji yakafungwa eti anasema alikuta tumeweka karatasi ndani ya mita, haizunguki.
 
Katibu mkuu Wizara ya Maji mhandisi Antony Sanga amesema utofauti wa mita hizo na mita zingine ni kuwa unaweza ukamgawia jirani uniti za maji kama unavyohamisha salio kwenye simu na akaendelea kupata huduma, vilevile kama unahama nyumba uliyokua ukiishi na kuna uniti zako zimebaki kwenye mita unaweza ukahama nazo pia. KONGOLE SANA
 
Hivi wanavyotoa bill kubwa wakati hawanufaiki na chochote inawasaidia nini?
Wanapewa monthly targets (malengo) hivyo kuyafikia wanalazimisha kwa kubambikia wananchi akara za maji.

Kingine ni roho mbaya na husuda tu.

Pia wanatengeneza mazingira ya rushwa kwamba next time kabla hawajasoma mita uwatafute muongeee nao kabla ili kuona uwezekano wa kui temper.

Ni hila hila tu [emoji57][emoji57]
 
Back
Top Bottom