Mita mpya za maji ni kama king’amuzi, maji yakiisha inaji-lock

Litasaidia pia kuepusha visasi. Kuna jamaa wa idara ya maji tulishwahi kuzinguana naye home, atatubandika bill ya laki 6 na maji yakafungwa eti anasema alikuta tumeweka karatasi ndani ya mita, haizunguki.
Usiiombee, huku tanga kuna baadhi tuliwekewa kwa ule usumbufu wake wa kununua token mpaka walikuja kuiondoa
 
sema izi mita ni nzuri yaan unaweza kumuamishia jirani units za maji kama kwake zimeisha kitu ambacho luku za umeme hazina
 
Tumeshaona faida za hizi mita sasa Wizara ianze kazi mara moja ya kuzifunga, kwa kuanzia na mkoa wa DSM ambao ndio unaongoza kwa kuwa na malalamiko ya kubambikiwa Bili.
Hongera sana Mhe. Waziri Awesu kwa ubunifu.

Tukiwa na Mawaziri wa aina ya Aweso hakika kero za wananchi zitabaki kuwa historia.
 
Hawa wasoma mita n wababaishaji sana. Hapa home msoma mita hajaja miez mitatu ilopita. Leo kaja katuambia bili ni 55000 kwa miez yote mitatu. Nimegawanya hyo pesa kwa kila mwez ni kama 18000. Sasa cha ajabu n kwamba hapa home kahamia mama ana watoto watatu mmoja n mdogo wa mgongon. Kila sku huyu mama anafua lakn cha ajabu bill imekuja ile ile sawa na ambapo alikua hajahamia huyu mama. Nmeenda kuangalia kwny mita ya maji nakuta ina ukungu yaan zle namba hazionekan na huwezi kuzisoma lakn jamaa katupa bill.

Nilichojifunza n kwamba hz bill za maji huwa wanakadiria tu hakuna cha kusoma mita wala nn.
 
Je, inawezekana nikaunganishiwa maji kutoka kwa jirani aliewekewa mita ya luku? Lakini kwangu nitumie sub mita ambay itakua inampa ukweli wa kiasi cha maji nilichotumia!!!
 
Tumeshaona faida za hizi mita sasa Wizara ianze kazi mara moja ya kuzifunga, kwa kuanzia na mkoa wa DSM ambao ndio unaongoza kwa kuwa na malalamiko ya kubambikiwa Bili.
Hongera sana Mhe. Waziri Awesu kwa ubunifu.

Tukiwa na Mawaziri wa aina ya Aweso hakika kero za wananchi zitabaki kuwa historia.

Kweli kabisa, huyu ustazi ni mfano wa kuigwa

jumaa Awesome B
 
Litasaidia pia kuepusha visasi. Kuna jamaa wa idara ya maji tulishwahi kuzinguana naye home, atatubandika bill ya laki 6 na maji yakafungwa eti anasema alikuta tumeweka karatasi ndani ya mita, haizunguki.
Ha ha ha mliingia cha kike. Kwahiyo mkalipa?
 
Hivi wanavyotoa bill kubwa wakati hawanufaiki na chochote inawasaidia nini?
Bill kubwa wanatoa kwa sababu maji mengi yanapotea kwa uzembe wao au wa wananchi.pale Moshi, mitaa ya shule ya old Moshi kuna bomba hua limepasuka linamwaga maji hata siku 3 mfululizo,hii ndio sababu serikali inabambika bill za maji ili kufidia hasara
 
Wale jamaa waliokuwa wanapaswa kupita mitaaani kusoma mita manually walikuwa wanapika sana data. Unakuta hwajafika hata eneo la tukio wapo kwa mama ntilie wana jaza jaza tu taarifa za bill za uongo,
Akizunguka nyumba tano akichoka anaenda kwenye ka-glosari anaagiza safari moja anaanza kupika data za mtaa mzima. Kuna nyuma walisafiri miezi kibao ila wakakuta bili inawasubiri.
 
Hawa wasoma mita n wababaishaji sana. Hapa home msoma mita hajaja miez mitatu ilopita. Leo kaja katuambia bili ni 55000 kwa miez yote mitatu. Nimegawanya hyo pesa kwa kila mwez ni kama 18000. Sasa cha ajabu n kwamba hapa home kahamia mama ana watoto watatu mmoja n mdogo wa mgongon. Kila sku huyu mama anafua lakn cha ajabu bill imekuja ile ile sawa na ambapo alikua hajahamia huyu mama. Nmeenda kuangalia kwny mita ya maji nakuta ina ukungu yaan zle namba hazionekan na huwezi kuzisoma lakn jamaa katupa bill.

Nilichojifunza n kwamba hz bill za maji huwa wanakadiria tu hakuna cha kusoma mita wala nn.
Hapo kwenye ukungu ndani ya mita ni tatizo sugu ndugu, huwezi kujisomea units zako unaletewa bills za kupikwa tu
 
Back
Top Bottom