Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wale jamaa waliokuwa wanapaswa kupita mitaaani kusoma mita manually walikuwa wanapika sana data. Unakuta hwajafika hata eneo la tukio wapo kwa mama ntilie wana jaza jaza tu taarifa za bill za uongo,Hili ndilo litakuwa mwarobaini wa tatizo la kubambikiana Bills! Unatumia maji ya 3000 unapewa bill ya 12000.
Tumezibuni na kutengeneza wenyewe au tumezitoa kwa MABEBERU?
Serikali kupitia Wizara ya Maji kuanzia mwezi Julai inatarajia kuanza kufunga mita za maji za malipo ya kabla[PRE PAID WATER METERS] ambazo zitakuwa na mfumo wa King’amuzi unaweza ukanunua ukiwa sehemu yoyote duniani
Katibu mkuu Wizara ya Maji mhandisi Antony Sanga amesema utofauti wa mita hizo na mita zingine ni kuwa unaweza ukamgawia jirani uniti za maji kama unavyohamisha salio kwenye simu na akaendelea kupata huduma, vilevile kama unahama nyumba uliyokua ukiishi na kuna uniti zako zimebaki kwenye mita unaweza ukahama nazo pia.
Ila Bongo kila neno lazima wafupishe. Mfano Chama Cha... duh haya mavyama yako mengi.Lipa Maji Kadiri Unavyotumia
LIMKU
Wizara ya Maji mnitoe mkianza kutumia hili jina.
LIMAKULipa Maji Kadiri Unavyotumia
LIMKU
Wizara ya Maji mnitoe mkianza kutumia hili jina.
Watapangiwa kazi nyingineKwahy wale wafanyakaz wanazunguka kusoma meters watakosa kazi
Msishangilie sana tatizo litakuja kwenye upatikanaji hizo meter!! Sio mara ya kwanza luku za maji kuletwa ; namkumbuka enzi ya Lowassa akiwa Waziri Mkuu kulikuwa na bwana mmoja akiitwa engineer Kaaya aliyekuwa mkuu wa DAWASCO alizileta hizi meter halafu zikapotea!!! Hopefully, safari hii zitakuwepo za kutosha na hakutakuwa na mizengwe ya milungula!!!Katibu mkuu Wizara ya Maji mhandisi Antony Sanga amesema utofauti wa mita hizo na mita zingine ni kuwa unaweza ukamgawia jirani uniti za maji kama unavyohamisha salio kwenye simu na akaendelea kupata huduma, vilevile kama unahama nyumba uliyokua ukiishi na kuna uniti zako zimebaki kwenye mita unaweza ukahama nazo pia. KONGOLE SANA
Ni bure hakuna ghalama yoyote wejiandae July kutumia mita mpya inaitwa LIMKU yaan lipia maji kadili unavyotumia.Wanafunga bure..!??
Khaa mkuu hata kama exaggeration hii imezidi sasaHii unapanga nyumba iliyo na kina dada, hawavumilii kukosa maji, kuliko wanaume ambao anaweza kutoboa mwezi hana tone la maji ndani.
Kwa nn ianzie mkoani??? Hii ni dharau za wazi wazi kwa wanadaresalama aseeHii system niliikuta Mbeya, Mwanjelwa na Soweto.View attachment 1807838
Uhasi wangu una sababu na ukweli. Maendeleo yana gharama, na siku zote mtumiaji ndio mlipaji. Ujio wa mitaa si wa kufurahia, una gharama. Moja wapo ni watu kukosa maji hapo program inapotibuliwa makusudi ilu programmer apate hela.Mbona uko hasi
Kubambikiwa bill kwenye mita huwa ni jambo la muda. Msoma mita hana uwezo wa kusogeza mita mbele, zinazo ongezwa ni tarakimu, ambao hupingwa kwa physical reading, na ukiwafikisha mahakamani, with proven evidence, una fidia kubwa.Siijui mkuu.ila nadhani itakuwa kubwa sawa na any initial investment kwenye biashara yoyote.ila ninachojua over long run kutakuwa na manufaa zaidi.ukiangalia kwa macho ya karibu unaweza usione manufaa.kulinganisha na usumbufu na kubambikiwa bills ,kama walivyofanya Tanesco,sasa hiv haina kubambikiana mibili ya hovyo
Dar ni mkoani, inategemeana unausemea tokea wapi.Kwa nn ianzie mkoani??? Hii ni dharau za wazi wazi kwa wanadaresalama asee
Lengo lilikua ni kumpatia gawio mwendazake, kama vile ATCL walivyokua wanapata faida nyingi na kuipatia serikali gawio lake.Hivi wanavyotoa bill kubwa wakati hawanufaiki na chochote inawasaidia nini?
Yani wajiandae. Teknolojia huwa inakuja na positive and negative effects. Wajifunze ufundi wa hizo meters ili waendelee kuwa relevant.Kwahy wale wafanyakaz wanazunguka kusoma meters watakosa kazi