Mitaa yetu mingi haina nafasi za wazi kwaajilli ya kupumzika. Huwa unaenda wapi kupunga upepo?

Mitaa yetu mingi haina nafasi za wazi kwaajilli ya kupumzika. Huwa unaenda wapi kupunga upepo?

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,042
Reaction score
17,320
Nimekaa mitaa mingi maeneo ya kipato cha kati na cha juu hata kufikia kupata kwangu. Changamoto nyingi niliyokumbana nayo ni wakati unatafuta sehemu ukakae peke yako ukatafakari hili na lile. Nyumbani wakati fulani panakuwa na miingiliano mingi ya wife, watoto, jamaa na marafiki au wewe kama baba wakati mwingine unawaachi space wajibinafasi (si unajua dingi akiwepo panakuwa na nidhamu ya woga).

Sasa Bwana nimekuja kuona wengi uishia Bar. Tatizo la Bar lazima uwe na hela ya kukalia siti ya eneo la biashara, hiki ni kipengere wakati mwingine hauko vizuri. Sehemu nyingine ni viwanja vya mipira ambapo hujaa wahuni na teenagers wanaoishi maisha yao panakuwa hapakufai.

Sehemu nyingine zinakuwa mbali na nyumbani ambapo utalazimika kutumia usafiri! Sasa kwa changamoto hii wanajamvi huwa mnafanyaje? Nadhani stress nyingi na maugonvi usababishwa na mtu kukosa mahali pa kupumua! Kwangu anagalau nina "Pub" ambayo sikosi mtu mpya wa kuchill naye kwa kupiga story nikiwa nimeboreka! Wewe huwa unafanyaje?
 
Kama una familia na unapata stress kiasi cha kutaka kuwa mwenyewe basi ujue umeingia choo cha kike.

Hayo mambo waachie mabachela wanaosaka warembo wakuchakata ila kama una familia kaa na watoto wako na mkeo. Wanahitaji uwepo wako zaidi.
 
Umeongea kitu cha maana kabisa.

Mm nimepanga single self. Nawaza hivi nikioa na niko humu. Siku nimegombana na Wife. Tunakaaje, maana haiwezekani mtu kakukera na kila ukigeuka unamuona [emoji16]

Space ni kitu cha muhimu sna kwangu. Nitaoa siku uchumi ukiruhusu kupanga nyumba nzima. Ili tukikosana. Akija chumbani naenda sebuleni, akija sebuleni naenda chumbani nafunga mlango [emoji16]
 
Hii kitu nilikua naongea na mtu Jana, Yani hata mazoezi vitu ambavyo ni vya muhimu serikali ilishashindwa kutenga maeneo, ukitaka kufanya jogging labda ufanyie barabarani bodaboda wakupapue
Kwa mjini. Unakuta watu wamekaa kwenye vile viti vya stand ambapo abiria wanatakiwa kukaa wakiwa wanasubiri usafiri.

Lakini tulitakiwa kua na open space kabisa. Mfano. Iringa katikati pale kuna ka open space, wanaitaje sijui tulikua tunaenda kukaa kipindi tunasoma Advance
 
Kwa maisha ya bongoland maeneo yote wameuziwa na kugawana wenyewe huko (wakubwa)

Kwa maisha haya ya sasa ukitaka open space, pigana vyovyote vile per day upate 1000/- lako kisha nenda bar nunua maji uletewe na glass endelea kuangalia uumbaji na nyimbo kupitia tv ya bar.
 
Kama una familia na unapata stress kiasi cha kutaka kuwa mwenyewe basi ujue umeingia choo cha kike.

Hayo mambo waachie mabachela wanaosaka warembo wakuchakata ila kama una familia kaa na watoto wako na mkeo. Wanahitaji uwepo wako zaidi.
Siyo kweli kwamba familia ni mbaya. Ni nature kwamba ukikaa na mkeo nyumbani muda mrefu lazima mgombane.

Mwanaume unatakiwa utoke ili mkeo akumiss.

Unatakiwa utoke ili mkeo akumiss na awe na mashamsham ya kukuona.

Ukikaa sana home anahisi huwezi kupata mwingine na hivyo anakuwa na mood swings za aina aina fulani.

Hannah
 
Kama una familia na unapata stress kiasi cha kutaka kuwa mwenyewe basi ujue umeingia choo cha kike.

Hayo mambo waachie mabachela wanaosaka warembo wakuchakata ila kama una familia kaa na watoto wako na mkeo. Wanahitaji uwepo wako zaidi.
Wee jamaa unaonekana bado kijana! Ukikua utanielewa
 
Hii kitu nilikua naongea na mtu Jana, Yani hata mazoezi vitu ambavyo ni vya muhimu serikali ilishashindwa kutenga maeneo, ukitaka kufanya jogging labda ufanyie barabarani bodaboda wakupapue
Sasa wewe umenisoma! Open space za public ni muhimu kuwepo mitaani kwetu! Ulaya zipo! Atakama ni mbali lakini usafiri ni rafiki kufika
 
Miji karibu yote yaTanzania ni slums, haijapangwa na hata kama imepangwa maofisa wa CCM wanakula rushwa wanagawana maeneo bila kufuata utaratibu, ukisafiri na ndege usiku ukaangalia chini Dar ni kama pori tuu lenye taa halina mpangilio wowote
 
Umeongea kitu cha maana kabisa.

Mm nimepanga single self. Nawaza hivi nikioa na niko humu. Siku nimegombana na Wife. Tunakaaje, maana haiwezekani mtu kakukera na kila ukigeuka unamuona...
Space yakupumua na kutafsakuri ni muhimu! Wengi tunaendaga bar
 
Watu tunajitahidi tupate muda tutulie na familia wewe unaikimbia
Jitafakaroli sana na ubadirikae
Furahia nao sasa hivi wakati Upo na AFYA NGUVU na Uwezo wa kutafuta pesa lakini kubwa zaidi wakati Upo na uhai
Kuna moment katika maisha haziwezi kurudi tena
Jitahidi sana kufurahia MAISHA na watoto wako pamoja
Vile utakavyokuwa nao ndivyo nawe baadae watakuwa na wewe

Mkuu YOU ONLY LIVE TWICE so ENJOY EVERY MOMENT YOU HAVE waache watoto wafurahi na wewe wakati upo hai na afya
Kama unajisikia kutoka na kupumzika toka na familia
 
Kwa mjini. Unakuta watu wamekaa kwenye vile viti vya stand ambapo abiria wanatakiwa kukaa wakiwa wanasubiri usafiri.

Lakini tulitakiwa kua na open space kabisa. Mfano. Iringa katikati pale kuna ka open space, wanaitaje sijui tulikua tunaenda kukaa kipindi tunasoma Advance
Ndio iringa kuna uwazi wa Manispaa! Hila sasa hivi mafisadi walishajenga biashara kitambo!
 
Kwa maisha ya bongoland maeneo yote wameuziwa na kugawana wenyewe huko (wakubwa)

Kwa maisha haya ya sasa ukitaka open space, pigana vyovyote vile per day upate 1000/- lako kisha nenda bar nunua maji uletewe na glass endelea kuangalia uumbaji na nyimbo kupitia tv ya bar.
😂😂😂😂! Wewe unaelewa! Sehemu pekee ya kimbilio ni bar!
 
Back
Top Bottom