Mitaa yetu mingi haina nafasi za wazi kwaajilli ya kupumzika. Huwa unaenda wapi kupunga upepo?

Mitaa yetu mingi haina nafasi za wazi kwaajilli ya kupumzika. Huwa unaenda wapi kupunga upepo?

Nakaa karibu na baharini, nikiona hovyo naenda ufukweni... Japo nina muda sasa sijaenda huko.
Ikiwa nyakati za jioni nachukua viatu vyangu naenda uwanjani kucheza mpira.
Huwa naenjoy mnoo kucheza na vijana, nikifika wananipokea kwa shangwe, naburudika, najisikia faraja kubwa mnoo.
 
Hii kitu nilikua naongea na mtu Jana, Yani hata mazoezi vitu ambavyo ni vya muhimu serikali ilishashindwa kutenga maeneo, ukitaka kufanya jogging labda ufanyie barabarani bodaboda wakupapue
Maeneo yapo sema yamevamiwa
Na serikali hiyo watu wa manispaaa wameyauzwa/ama kuwapa watu wafanye shuguli za biashara
Watu na watoto hawana sehemu za kwenda kupumzika ama kucheza
Watoto wanaishia kucheza vichochoroni tu na huko wanaishia kukutana na mambo ya ajabu tu
Serikali zetu ni za ajabu sana

Ova
 
Siyo kweli kwamba familia ni mbaya. Ni nature kwamba ukikaa na mkeo nyumbani muda mrefu lazima mgombane.

Mwanaume unatakiwa utoke ili mkeo akumiss.

Unatakiwa utoke ili mkeo akumiss na awe na mashamsham ya kukuona.

Ukikaa sana home anahisi huwezi kupata mwingine na hivyo anakuwa na mood swings za aina aina fulani.
Asante mkuu kwa kumpa somo kijana! 👍
 
Huwa nikiangalia movie za nje nikiona zile parks naumia sana kuona sisi huku hatuna maeneo kama hayo.

Mtu ukitaka kutuliza akili ni hadi uende beach kule kusikokuwa na watu wengi na isiwe siku za weekend na bado nako ni hatari kuwa peke yako na zaidi ni mbali kutoka katikati ya jiji.

Zamani kidogo Magomeni Mapipa pale kulikuwa na eneo limetengwa maeneo ya Kanisani pale watu walikuwa wanapumzika ila pameshauzwa sasa hivi kuna mabaa kibao.
 
Miji karibu yote yaTanzania ni slums, haijapangwa na hata kama imepangwa maofisa wa CCM wanakula rushwa wanagawana maeneo bila kufuata utaratibu, ukisafiri na ndege usiku ukaangalia chini Dar ni kama pori tuu lenye taa halina mpangilio wowote
Kinondoni na sehemu za mwananyama nyingi zilikuwa na open space ila zote zimevamiwa
Zimechukuliwa na yote hii wahusika ni watu wa serikali ya ccm

Ova
 
Watu tunajitahidi tupate muda tutulie na familia wewe unaikimbia
Jitafakaroli sana na ubadirikae
Furahia nao sasa hivi wakati Upo na AFYA NGUVU na Uwezo wa kutafuta pesa lakini kubwa zaidi wakati Upo na uhai
Kuna moment katika maisha haziwezi kurudi tena
Jitahidi sana kufurahia MAISHA na watoto wako pamoja
Vile utakavyokuwa nao ndivyo nawe baadae watakuwa na wewe

Mkuu YOU ONLY LIVE TWICE so ENJOY EVERY MOMENT YOU HAVE waache watoto wafurahi na wewe wakati upo hai na afya
Kama unajisikia kutoka na kupumzika toka na familia
Hujamuelewa jamaa, hamna asieipenda familia ila pamoja na kua baba wewe pia ni binadamu.
Kuna muda unahitaji kukaa utafakari ya hiyohiyo familia, ufanye mambo yako private.
 
Mkuu park kama central park huwezi kufananisha na back yard yako.
Kwa hiyo kila wakati ukitaka kutafakari utakuwa unaenda central park?

Jitahidi mnunue maeneo makubwa ndani ya backyard unaweza kuplan maeneo kama hayo ya kupumzika na kutafakari (backyard rest area)

Wakati fulani unaweka BBQ grill yako na vinywaji ukawa unafanya tafrija na familia au ndugu, jamaa na marafiki
 
Kwa nini ulinunua kiwanja cha 20×20 mkuu?

Wenye viwanja vikubwa vyenye nafasi ya kutosha hawakosi mahali pa kukaa na kutafakari
Nina eneo kubwa bro! Zaidi 1200sqm na mita 20 kutoka nyumba yangu nina pub! Naongelea kwa waliowengi na changamoto nilizopitia nyuma kulazimika kujijengea kapub ka kukutana na watu!
 
Kwa hiyo kila wakati ukitaka kutafakari utakuwa unaenda central park?

Jitahidi mnunue maeneo makubwa ndani ya backyard unaweza kuplan maeneo kama hayo ya kupumzika na kutafakari (backyard rest area)

Wakati fulani unaweka BBQ grill yako na vinywaji ukawa unafanya tafrija na familia au ndugu, jamaa na marafiki
Kwahio unafikiri wanaoenda park hawana maeneo makubwa? Nyumbani ni nyumbani na public park ni public park. Maeneo mawili tofauti.
 
Na bado ukipata eneo hila kuna watu hawajui msemo wa "mind own business" mtu anakuja hata hajakaribishwa na kuanza maswali ,vistory vya kijinga mpaka unaona home pana nafuu zaidi ya hapo
 
Moja ya matatizo makubwa ambayo tunayo ndani ya nchi yetu ni hili la open space ambalo ni zao la city Planning,sababu tumekosa watu wenye akili mwisho,tumeshindwa hata jambo ndogo kiasi hicho.
 
Kwa mjini. Unakuta watu wamekaa kwenye vile viti vya stand ambapo abiria wanatakiwa kukaa wakiwa wanasubiri usafiri.

Lakini tulitakiwa kua na open space kabisa. Mfano. Iringa katikati pale kuna ka open space, wanaitaje sijui tulikua tunaenda kukaa kipindi tunasoma Advance
Yeah !
Nakumbuka ile bustani ilikuwepo pale Iringa mjini ,sijui kama ipo hadi sasa .
Nakumbuka enzi hizo , siku ya outing tukienda town tunachill pale kwenye bustani .
Baada ya kuzunguka town kufanya shopping na mambo mengine .
Iringa ,moja kati ya miji ya mkoloni wa kijerumani iliyokuwa imepangika vizuri .
Tatizo ni kukosa mwendelezo
 
Kwahio unafikiri wanaoenda park hawana maeneo makubwa? Nyumbani ni nyumbani na public park ni public park. Maeneo mawili tofauti.
Wana maeneo makubwa lakini sio mahali ambapo wanaaenda kila siku.

Nilijfunza vitu nikiwa nje na nikagundua wabongo wengi hatuna indoor na outdoor recreational activities with family members at home

Wenzetu backyard wanazitumia effectively kwa mambo mengi sana ya kupumzika, kutafakari na michezo
 
Back
Top Bottom