Mitambo ya IPTL imeibiwa na jengo kubaki Gofu. Iliwekwa rehani na Herbinder Seth

Mitambo ya IPTL imeibiwa na jengo kubaki Gofu. Iliwekwa rehani na Herbinder Seth

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Nilishuhudia gari la mwisho lililobeba chuma chakavu kutoka IPTL likikamatwa pale Skansika usiku wa Jumapili 05/03 2023, ambapo watu 3 waliokuwa kwenye gari na Polisi waliokuwa wakilinda Mitambo walikamatwa na Kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa Maelekezo ya Muliro. Gari lenye mzigo lipo Kituo cha Polisi, Kawe Dar es Salaam.

Tarehe 17 Jun 2021, Herbinder Seth aliachiwa huru baada ya kuweka rehani mitambo hiyo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuachia huru kwa masharti Mmiliki wa Kampuni ya Kufua umeme (IPTL), Herbinder Seth, huku pia akitakiwa kulipa fidia ya sh. bilioni 26.9 kwa serikali. Hatua hiyo ilikuja baada ya Seth kuingia makubaliano na DPP ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili kwa njia muafaka.

Aidha Seth alikubali kuweka rehani hati ya kiwanda cha kufua umeme cha IPTL chenye namba 45566 kiwanja namba 292/2 kilichopo Kunduchi Salasala kama dhamana iwapo atashindwa kulipa fedha hizo. Hata hivyo, mshtakiwa Seth alilipa kiasi cha sh. Milioni 200 na kiasi kilichobakia alitatakiwa kukilipa ndanj ya miezi kumi na mbili kuanzia Juni 16, 2021.

July 2017, Independent Power Tanzania Limited (IPTL) maombi yake ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme yalikwama kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu., huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

Hali hiyo ilijitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Afrika Power (PAP), Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kuisababishia hasara Serikali.

Ilikuwa inadaiwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

Leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, 2017 baada ya kufanya kazi kwa miaka 23.

Kampuni hiyo ua IPTL iliingia chini tangu mwaka 1994 na kila mwezi ilikuwa ikilipwa TSh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo,

Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa Tanesco.

Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.

Wengine ni Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Jaji Frederick Werema aliyejiuzulu nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Eliachim Maswi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alisimamishwa kazi pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco waliotakiwa kuwajibishwa, kukaa pembeni baada ya muda wa bodi yao kwisha na ikaundwa nyingine.

Naye Spika wa Bunge wakati huo, Anne Makinda alitangaza kuwa wazi nafasi za wenyeviti wa kamati za Bunge ambao ni William Ngeleja, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Andrew Chenge aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Victor Mwambalaswa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

Azimio jingine lililotaka Harbinder Singh Seth ambaye ni Mwenyekiti wa PAP kufikishwa mahakamani, lilitekelezwa yeye na mwenzake James Rugemalira wa VIP Engineering, walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka 12 yakiwamo ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha.

Baadhi ya maazimio ambayo yalikuwa hayajafanyiwa kazi ni lile la pili lilolotaka Serikali iangalie uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

====
UPDATES;
=====

Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar e Salaam, Muliro Jumanne amesema “Tumezipata hizo taarifa na tunazichunguza, katika uchunguzi kuna watu wanahojiwa.”

IMG-20230309-WA0011(1).jpg


IMG-20230309-WA0007(1).jpg
IMG-20230309-WA0010.jpg
IMG-20230309-WA0008(1).jpg
IMG-20230309-WA0009.jpg
IMG-20230309-WA0006(1).jpg
 
lazima kuna uhuni tu unataka kufanyika hapo, hayo HOF engines kwasasa utamuuzia nani? tena yamekaa miaka kadhaa bila kuunguruma. Hapo wametumwa wahuni wafanye uhuni ili mtu ajipigie mahala, TIME IS THE BEST DOCTOR.
 
Subhanallah...🙆‍♂️
R.i.P John...😪
Na kama hivyo ndivyo basi natamani sikumoja tupate tena Rais kichaa (kama walivyo muita).
By the way, sinto shangaa siku nikija kisikia kwamba Chamwino imeibiwa na wanatafutwa walio iiba "Chamwino" ili wahojiwe...
 
Back
Top Bottom