Mitambo ya IPTL imeibiwa na jengo kubaki Gofu. Iliwekwa rehani na Herbinder Seth

Nilishuhudia gari la mwisho lililobeba chuma chakavu kutoka IPTL likikamatwa pale Skansika usiku wa Jumapili 05/03 2023, ambapo watu 3 waliokuwa kwenye gari na Polisi waliokuwa wakilinda Mitambo walikamatwa na Kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa Maelekezo ya Muliro. Gari lenye mzigo lipo Kituo cha Polisi, Kawe Dar es Salaam.

Tarehe 17 Jun 2021, Herbinder Seth aliachiwa huru baada ya kuweka rehani mitambo hiyo.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuachia huru kwa masharti Mmiliki wa Kampuni ya Kufua umeme (IPTL), Herbinder Seth, huku pia akitakiwa kulipa fidia ya sh. bilioni 26.9 kwa serikali. Hatua hiyo ilikuja baada ya Seth kuingia makubaliano na DPP ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili kwa njia muafaka.

Aidha Seth alikubali kuweka rehani hati ya kiwanda cha kufua umeme cha IPTL chenye namba 45566 kiwanja namba 292/2 kilichopo Kunduchi Salasala kama dhamana iwapo atashindwa kulipa fedha hizo. Hata hivyo, mshtakiwa Seth alilipa kiasi cha sh. Milioni 200 na kiasi kilichobakia alitatakiwa kukilipa ndanj ya miezi kumi na mbili kuanzia Juni 16, 2021.

July 2017, Independent Power Tanzania Limited (IPTL) maombi yake ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme yalikwama kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu., huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

Hali hiyo ilijitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Afrika Power (PAP), Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kuisababishia hasara Serikali.

Ilikuwa inadaiwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

Leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, 2017 baada ya kufanya kazi kwa miaka 23.

Kampuni hiyo ua IPTL iliingia chini tangu mwaka 1994 na kila mwezi ilikuwa ikilipwa TSh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo,

Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa Tanesco.

Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.

Wengine ni Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Jaji Frederick Werema aliyejiuzulu nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Eliachim Maswi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alisimamishwa kazi pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco waliotakiwa kuwajibishwa, kukaa pembeni baada ya muda wa bodi yao kwisha na ikaundwa nyingine.

Naye Spika wa Bunge wakati huo, Anne Makinda alitangaza kuwa wazi nafasi za wenyeviti wa kamati za Bunge ambao ni William Ngeleja, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Andrew Chenge aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Victor Mwambalaswa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

Azimio jingine lililotaka Harbinder Singh Seth ambaye ni Mwenyekiti wa PAP kufikishwa mahakamani, lilitekelezwa yeye na mwenzake James Rugemalira wa VIP Engineering, walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka 12 yakiwamo ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha.

Baadhi ya maazimio ambayo yalikuwa hayajafanyiwa kazi ni lile la pili lilolotaka Serikali iangalie uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

Juni 20, 2017 akiwa ziarani mkoani Pwani, Rais John Magufuli, alisema serikali itaendelea kuchukua hatua dhidi ya watu wanaolihujumu Taifa ikiwamo kujihusisha na vitendo vya wizi na rushwa na haitakatishwa tamaa na watu wanaolalamika na kubeza juhudi hizo.

====
UPDATES;
=====

Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar e Salaam, Muliro Jumanne amesema “Tumezipata hizo taarifa na tunazichunguza, katika uchunguzi kuna watu watahojiwa.”

Yaani mpaka msaramia mwema anagundua haya maana yake ni kwamba dola ya Tanzania inayaacha haya yatokee mbele ya macho yao hadi waambiwe wachukue hatua ndo watu wanahojiwa.

Katiba mpya inapaswa kuwawajibisha viongozi wote wanaoshindwa kulinda maslahi nchi.

Hongera sana figganigga kwa kutujulisha umma haya madudu
 
Ilikuwa inalindwa na nani na ilikuwa chini ya nani? Sheria inasemaje dhamana ikitoweka chini ya aliyekuwa anaishikilia?
Dhamana zote za serikali zinakuwa chini ya Msajili wa Hazina.
Nchi ngumu hii
 
Kwa hiyo kwa tafsiri nyingine nyingine ni kuwa mali za PAP zimeibiwa mikononi mwa Msajili wa Hazina au? Na itakuwaje akidai mali zake?

Atakayelipa siyo msajili wa Hazina bali Kodi yangu na yako...

Nchi hii tumerogwa na hakuna anayesikia makali ya kiwembe
 
Hii nchi haina TISS

Ndo maana kwenye uzi wangu wa Usiri wa TISS niliongelea Usiri wao kwenye ajira haya ndo matokeo
Inasikitisha sana TISS haipo kuisaidia nchi yetu
 
RIP JPM,TAIFA LITAKUKUMBUKA,
Kumkumbuka kwa maovu aliyofanya dhidi ya Watanzania. Kuwaua, kuwabanbikia kesi, kusema uwongo na kuiba fedha na kuziweka China. Kuiba uchaguzi ili awe Rais wa maisha na kutuachia bunge la hovyo
 
Unachekesha kwakweli
 
Hii nchi haina TISS

Ndo maana kwenye uzi wangu wa Usiri wa TISS niliongelea Usiri wao kwenye ajira haya ndo matokeo
TISS kimekuwa ni kitengo cha hovyo tena chenye URASIMU SANA watu waliopo hawajui hata majukumu yako na wengi wao wanajiropekea tu kuwa yye ni TISS ni hovyo kuliko hovyo
 
Nilishuhudia gari la mwisho lililobeba chuma chakavu kutoka IPTL likikamatwa pale Skansika usiku wa Jumapili 05/03 2023, ambapo watu 3 waliokuwa kwenye gari na Polisi waliokuwa wakilinda Mitambo walikamatwa na Kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa Maelekezo ya Muliro. Gari lenye mzigo lipo Kituo cha Polisi, Kawe Dar es Salaam.

Tarehe 17 Jun 2021, Herbinder Seth aliachiwa huru baada ya kuweka rehani mitambo hiyo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuachia huru kwa masharti Mmiliki wa Kampuni ya Kufua umeme (IPTL), Herbinder Seth, huku pia akitakiwa kulipa fidia ya sh. bilioni 26.9 kwa serikali. Hatua hiyo ilikuja baada ya Seth kuingia makubaliano na DPP ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili kwa njia muafaka.

Aidha Seth alikubali kuweka rehani hati ya kiwanda cha kufua umeme cha IPTL chenye namba 45566 kiwanja namba 292/2 kilichopo Kunduchi Salasala kama dhamana iwapo atashindwa kulipa fedha hizo. Hata hivyo, mshtakiwa Seth alilipa kiasi cha sh. Milioni 200 na kiasi kilichobakia alitatakiwa kukilipa ndanj ya miezi kumi na mbili kuanzia Juni 16, 2021.

July 2017, Independent Power Tanzania Limited (IPTL) maombi yake ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme yalikwama kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu., huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

Hali hiyo ilijitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Afrika Power (PAP), Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kuisababishia hasara Serikali.

Ilikuwa inadaiwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

Leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, 2017 baada ya kufanya kazi kwa miaka 23.

Kampuni hiyo ua IPTL iliingia chini tangu mwaka 1994 na kila mwezi ilikuwa ikilipwa TSh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo,

Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa Tanesco.

Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.

Wengine ni Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Jaji Frederick Werema aliyejiuzulu nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Eliachim Maswi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alisimamishwa kazi pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco waliotakiwa kuwajibishwa, kukaa pembeni baada ya muda wa bodi yao kwisha na ikaundwa nyingine.

Naye Spika wa Bunge wakati huo, Anne Makinda alitangaza kuwa wazi nafasi za wenyeviti wa kamati za Bunge ambao ni William Ngeleja, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Andrew Chenge aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Victor Mwambalaswa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

Azimio jingine lililotaka Harbinder Singh Seth ambaye ni Mwenyekiti wa PAP kufikishwa mahakamani, lilitekelezwa yeye na mwenzake James Rugemalira wa VIP Engineering, walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka 12 yakiwamo ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha.

Baadhi ya maazimio ambayo yalikuwa hayajafanyiwa kazi ni lile la pili lilolotaka Serikali iangalie uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

Juni 20, 2017 akiwa ziarani mkoani Pwani, Rais John Magufuli, alisema serikali itaendelea kuchukua hatua dhidi ya watu wanaolihujumu Taifa ikiwamo kujihusisha na vitendo vya wizi na rushwa na haitakatishwa tamaa na watu wanaolalamika na kubeza juhudi hizo.

====
UPDATES;
=====

Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar e Salaam, Muliro Jumanne amesema “Tumezipata hizo taarifa na tunazichunguza, katika uchunguzi kuna watu watahojiwa.”

Ni kiwango (standard), nadra sana ya uwasilishaji wa mada wa aina hii hapa JF siku hizi.
Taarifa iliyojitosheleza kabisa, isiyokuwa na ushabiki wa aina yoyote.

Pongezi sana kwa kazi hii nzuri.
 
Subhanallah...🙆‍♂️
R.i.P John...😪
Na kama hivyo ndivyo basi natamani sikumoja tupate tena Rais kichaa (kama walivyo muita).
By the way, sinto shangaa siku nikija kisikia kwamba Chamwino imeibiwa na wanatafutwa walio iiba "Chamwino" ili wahojiwe...
Nitaungana nawe katika "kushangaa" huko!

Lakini tuseme ukweli, kwa hali inavyokwenda, hilo halitakuwa tukio la kushangaza hata kidogo.
 
Back
Top Bottom