Mitambo ya IPTL imeibiwa na jengo kubaki Gofu. Iliwekwa rehani na Herbinder Seth

Uache kiherehere wakati huna ujualo, rudi shule ukajifunze kuandika kwa ufasaha, sasa hivi elimu ni bure.
Wewe si ushajitotelea kunifundisha,alafu mbona umepanic sana na ishu ya IPTL au wewe ndo ulikuwaga nyumba ndogo ya Ruge tuliyekuwa tunasikia ulipewa tenda ya kupeleka pale vitambaa vya kufutia mitambo vumbi ukawa unalipwa 100mln kwa mwezi?
 
Nilishuhudia gari la mwisho lililobeba chuma chakavu kutoka IPTL likikamatwa pale Skansika usiku wa Jumapili 05/03 2023, ambapo watu 3 waliokuwa kwenye gari na Polisi waliokuwa wakilinda Mitambo walikamatwa na Kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa Maelekezo ya Muliro. Gari lenye mzigo lipo Kituo cha Polisi, Kawe Dar es Salaam.

Tarehe 17 Jun 2021, Herbinder Seth aliachiwa huru baada ya kuweka rehani mitambo hiyo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuachia huru kwa masharti Mmiliki wa Kampuni ya Kufua umeme (IPTL), Herbinder Seth, huku pia akitakiwa kulipa fidia ya sh. bilioni 26.9 kwa serikali. Hatua hiyo ilikuja baada ya Seth kuingia makubaliano na DPP ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili kwa njia muafaka.

Aidha Seth alikubali kuweka rehani hati ya kiwanda cha kufua umeme cha IPTL chenye namba 45566 kiwanja namba 292/2 kilichopo Kunduchi Salasala kama dhamana iwapo atashindwa kulipa fedha hizo. Hata hivyo, mshtakiwa Seth alilipa kiasi cha sh. Milioni 200 na kiasi kilichobakia alitatakiwa kukilipa ndanj ya miezi kumi na mbili kuanzia Juni 16, 2021.

July 2017, Independent Power Tanzania Limited (IPTL) maombi yake ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme yalikwama kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu., huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

Hali hiyo ilijitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Afrika Power (PAP), Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kuisababishia hasara Serikali.

Ilikuwa inadaiwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

Leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, 2017 baada ya kufanya kazi kwa miaka 23.

Kampuni hiyo ua IPTL iliingia chini tangu mwaka 1994 na kila mwezi ilikuwa ikilipwa TSh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo,

Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa Tanesco.

Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.

Wengine ni Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Jaji Frederick Werema aliyejiuzulu nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Eliachim Maswi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alisimamishwa kazi pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco waliotakiwa kuwajibishwa, kukaa pembeni baada ya muda wa bodi yao kwisha na ikaundwa nyingine.

Naye Spika wa Bunge wakati huo, Anne Makinda alitangaza kuwa wazi nafasi za wenyeviti wa kamati za Bunge ambao ni William Ngeleja, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Andrew Chenge aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Victor Mwambalaswa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

Azimio jingine lililotaka Harbinder Singh Seth ambaye ni Mwenyekiti wa PAP kufikishwa mahakamani, lilitekelezwa yeye na mwenzake James Rugemalira wa VIP Engineering, walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka 12 yakiwamo ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha.

Baadhi ya maazimio ambayo yalikuwa hayajafanyiwa kazi ni lile la pili lilolotaka Serikali iangalie uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

====
UPDATES;
=====

Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar e Salaam, Muliro Jumanne amesema “Tumezipata hizo taarifa na tunazichunguza, katika uchunguzi kuna watu wanahojiwa.”

Aione Magufuli popote alipo mbinguni kwenye file
 
Wewe si ushajitotelea kunifundisha,alafu mbona umepanic sana na ishu ya IPTL au wewe ndo ulikuwaga nyumba ndogo ya Ruge tuliyekuwa tunasikia ulipewa tenda ya kupeleka pale vitambaa vya kufutia mitambo vumbi ukawa unalipwa 100mln kwa mwezi?

Jitahidi unapoandika uweke koma, nukta nk, maana sentensi zako zinageuka kuwa ndefu sana, jambo hili halikubaliki kiuandishi. Huu ni udhibitisho kuwa una upeo mdogo.
 
Nukta unayo wewe nipe niwe naweka.
 
Hii habari inahitaji mambo mawili ,Kwanza serikali ikanishe au ithibitishe

Pili ikithibitisha iseme wezi waliwezaje kufanikisha hii Nia mbovu na vifaa aliuziwa Nani wakati mwenye KAZI navifaa vya umeme ni TANESCO pekee?
Mama yupo busy huku kilimanjaro na sikukuu ya mwanawake
 
Miaka 6 Ikulu mbona alishindwa kuitaifisha iwe ya umma, tukaishia kufanganywa kwamba anainyoosha nchi, kukimbizana na CDM mabarabarani wakati mitambo inaondoka.
Angeitaifisha bilashaka leo hii ungecoment vinginevyo
 
Ipptl ni scraps tu. Mtambo wala haukua kitu ila kitu cha kuliibia taifa mabilioni. Hapo nadhani hakuna cha maana la msingi wezi wasije dhubutu kudai kitu. Maana wahuni waliopo sasa serikalini wanaweza kula njama kina seth na rugemalila wafungue madai kulisumbua tena taifa.
Ndo nachoona mimi hawajamaa watakuja kudai mitambo yao
 
MIMI NI MKAZI WA TEGETA HILO JAMBO NI KWELI LINAFANYIKA. WANAIBA VYUMA NA MALI TOFAUTI ZA KIWANDA. TUNASHUHUDIA PKPK NA MAGARI ZIKITOKA NA VYUMA IPTL.
 
Kumkumbuka kwa maovu aliyofanya dhidi ya Watanzania. Kuwaua, kuwabanbikia kesi, kusema uwongo na kuiba fedha na kuziweka China. Kuiba uchaguzi ili awe Rais wa maisha na kutuachia bunge la hovyo
Na mimba aliyokuachia pia itakumbukwa
 
We hacha tu yaani kampuni inalipwa biln 5+kwa mwezi kama bonus bado hapo hawajauza umeme?
Kwa miaka 23 ni Sawa na 5*12*23 billions= 1380 or Trillions 1.38, halafu tunaenda kuomba mkopo WA madawati, like seriously 😳
 
Nilishuhudia gari la mwisho lililobeba chuma chakavu kutoka IPTL likikamatwa pale Skansika usiku wa Jumapili 05/03 2023, ambapo watu 3 waliokuwa kwenye gari na Polisi waliokuwa wakilinda Mitambo walikamatwa na Kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa Maelekezo ya Muliro. Gari lenye mzigo lipo Kituo cha Polisi, Kawe Dar es Salaam.

Tarehe 17 Jun 2021, Herbinder Seth aliachiwa huru baada ya kuweka rehani mitambo hiyo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuachia huru kwa masharti Mmiliki wa Kampuni ya Kufua umeme (IPTL), Herbinder Seth, huku pia akitakiwa kulipa fidia ya sh. bilioni 26.9 kwa serikali. Hatua hiyo ilikuja baada ya Seth kuingia makubaliano na DPP ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili kwa njia muafaka.

Aidha Seth alikubali kuweka rehani hati ya kiwanda cha kufua umeme cha IPTL chenye namba 45566 kiwanja namba 292/2 kilichopo Kunduchi Salasala kama dhamana iwapo atashindwa kulipa fedha hizo. Hata hivyo, mshtakiwa Seth alilipa kiasi cha sh. Milioni 200 na kiasi kilichobakia alitatakiwa kukilipa ndanj ya miezi kumi na mbili kuanzia Juni 16, 2021.

July 2017, Independent Power Tanzania Limited (IPTL) maombi yake ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme yalikwama kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu., huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

Hali hiyo ilijitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Afrika Power (PAP), Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kuisababishia hasara Serikali.

Ilikuwa inadaiwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

Leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, 2017 baada ya kufanya kazi kwa miaka 23.

Kampuni hiyo ua IPTL iliingia chini tangu mwaka 1994 na kila mwezi ilikuwa ikilipwa TSh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo,

Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa Tanesco.

Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.

Wengine ni Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Jaji Frederick Werema aliyejiuzulu nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Eliachim Maswi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alisimamishwa kazi pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco waliotakiwa kuwajibishwa, kukaa pembeni baada ya muda wa bodi yao kwisha na ikaundwa nyingine.

Naye Spika wa Bunge wakati huo, Anne Makinda alitangaza kuwa wazi nafasi za wenyeviti wa kamati za Bunge ambao ni William Ngeleja, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Andrew Chenge aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Victor Mwambalaswa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

Azimio jingine lililotaka Harbinder Singh Seth ambaye ni Mwenyekiti wa PAP kufikishwa mahakamani, lilitekelezwa yeye na mwenzake James Rugemalira wa VIP Engineering, walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka 12 yakiwamo ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha.

Baadhi ya maazimio ambayo yalikuwa hayajafanyiwa kazi ni lile la pili lilolotaka Serikali iangalie uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

====
UPDATES;
=====

Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar e Salaam, Muliro Jumanne amesema “Tumezipata hizo taarifa na tunazichunguza, katika uchunguzi kuna watu wanahojiwa.”

Ukiisoma hii habari nchi hii ina kitendawili kimoja hakijateguliwa.

Kuna hii orodha ya watu was watu kwa mujibu wa imani zao za asili.
Kwa maana si watu wabaya, si magaidi. Wanatabia nzuri sana.

Orodha ni mrefu

Harbinder Singh Sethi
James Rugemalira
Sospeter Muhongo
Anna Tibaijuka
Frederick Werema
Eliachim Maswi
William Ngeleja
Andrew Chenge

Halafu kuna watu hatari sana kwa nchi.
Ni watu hatari kuliko majambazi. Ni magaidi. Hawa wanastahili kufundishwa adabu. Wanastahili kukaa jela miaka hata 10. Hata wakofa huko ni halali yao. Wakiumwa hawastahili kutibiwa labda walipie kama wanavyolipia watu wema

Sijui nataka kuzungumza nini lkn ngoja niishie hapa.
 
Back
Top Bottom