Uchaguzi 2020 Mitandao ya kijamii Tanzania yawa restricted. YouTube, WhatsApp, Twitter, JamiiForums na Telegram zimeguswa - Oktoba 27, 2020

Uchaguzi 2020 Mitandao ya kijamii Tanzania yawa restricted. YouTube, WhatsApp, Twitter, JamiiForums na Telegram zimeguswa - Oktoba 27, 2020

Kuna muda nilishangaa mdomo wangu unatoa matusi bila kutarajia. Nimepanga kukutana na hubby sehemu, nimefika hiyo sehemu simu hazitoki. Na yeye ananitafuta sipatikani. Bahati nzuri alikua anazunguka zunguka akaniona.

Yan huu upuuzi wa kuzimiana mitandao ni wa kishamba sana. 2020 tunazimiana mitandao kweli watu wengine biashara zinategemea mitandao watakula mawe. Jiwe et al. ni wehu sana
 
Kama tumejenga uchumi, kama tunapendwa, kama tumenunua ndege, kama tumejenga barabara na madaraja, kama tunatoa elimu bure, kama tumekomesha mafisadi, kama tumeaji, kama tumejenga fly over, kama tume...kama tume... kama tume.....wasi wasi wa nini mpaka mitandao izuiliwe kufanya kazi..?[emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapuuzi fulani tu..
Hawajui tu hasara wanayotupa!!

Alaf kila siku wanadai mitandaoni hamna wapiga kura, Sasa hofu yao ni nini?
Pia naamini nyumbani kwako/kwenu, mkiwa na marafiki zako, ndugu zako, jamaa zako, na kazini kwako kuna utaratibu wa kutoa mawazo na lugha ya kutumia.

Tunapoelekea siku ya kesho uchaguzi ni muhimu kudhibiti walio na tabia ya kuandika ya hovyo, uzushi, nk.

Kwa kuwa hujui kama hujui thamani ya amani, nakusamehe kwa hilo.
 
Back
Top Bottom