Uchaguzi 2020 Mitandao ya kijamii Tanzania yawa restricted. YouTube, WhatsApp, Twitter, JamiiForums na Telegram zimeguswa - Oktoba 27, 2020

Uchaguzi 2020 Mitandao ya kijamii Tanzania yawa restricted. YouTube, WhatsApp, Twitter, JamiiForums na Telegram zimeguswa - Oktoba 27, 2020

Naona connectivity ya Whatsapp kupitia voda imegoma kabisa mida hii. Hii ni baada ya Twitter nayo kuzimwa usiku wa kuamkia leo. Hili ni jambo geni halijawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Kwanini serikali na vyombo husika vitumie nguvu kubwa namna hii kuminyq uhuru wa mawasiliano Ya Wananchi wakati imebakia masaa machache kabla yq uchaguzi mkuu?
 
Najaribu kuingia YouTube lakini inagoma, kama nusu saa iliyopita nilikuwa naipata.

Kuna yeyote anapata tatizo kama langu?

Natumia mtandao wa Tigo
Iko wazi, sisi tunaipata. Au umeishiwa bundle/salio.
 
Najiuliza sipati jibu.

Ni jambo jipya ambalo halijapata kuwepo nchini tangu mitandao hii ianze.

Ndivyo tunavyotakiwa kulinda amani yetu, umoja wetu na Taifa letu?

Hofu yetu kubwa ni nini hasa juu ya mitandao hii?
 
Mimi pia sipati youtube na whatsapp kwa njia za kawaida mpaka nimefanya nnayojua mwenyewe. Wafunge yote hata simu pia wazifunge.ila JF tu watuachie kipindi hiki muhimu.
 
Back
Top Bottom