Hii line niliyonayo nimeitumia miaka zaidi ya 10 na sijawahi kulalamikia hilo suala kwasababu halikuwahi kunikuta. Isipokuwa kwa mtandao wa halotel niliwahi kuwaeleza na hawakunikata tena.
Ila sasa hawa vodacom jana wamekata hela yangu na mbaya zaidi maelezo wanayotoa sio sahihi yanakinzana! Mara oh nilikopa, tena wanadai nilijiunga na muito kwa wanipigiao. Wapuuzi sana!
Nahitaji wenye tatizo kama langu tuungane tufungue kesi. Mi niko tayari kutafuta hela ya kugharamia wakili mahiri!