Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015

Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015

MJADALA KUHUSU ZANZIBAR NA HATMA YA UCHAGUZI

`TUSIWE TAIFA LA KUONGOZWA KWA UONGO-HUMPHREY POLE POLE`

TUNAHIBIRI TUSIYOYATENDA. NI NJAA AU DINARI


Sehemu ya I

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/968731-mjadala-kuhusu-uchaguzi-wa-zanjadala-humphrey-polepole-na-ismail-jussa.html

Tunaendelea na tathmini ya uchaguzi tukidonoa donoa kilakona

Video inayoonekana hapo juu ni ya mada moto, kwa hisani yaaliyeiletea jamvini

Ni majadiliano kati ya Mh Jusa na Humphrey Polepolekada wa CCM na mwanachama mwenzetu hapa jimvini

Tuseme suala la ZNZ lipo kisheria ingawa ni la kisiasa.

Siasa inaingiliana na sheria ingawa siasa si sheria na walasheria si siasa.

Watunzi wa sheria ni wanasheria, wanaozichambua sheria kwamtazamo wa jamii ni wanasiasa (Bunge) kuziwezesha kuwa sheria zikitumiwana wanasheria

Ni makosa kudhani kila jambo ni siasa.

Tuanze mjadala kwa kuwakumbusha mabandiko ya mwanzotumeelezea mchakato wa uchaguzi., kuanzia tangazo linapotoka hadi kutangazwakwa mshindi

Hoja hizi amezitumia Humphrey na tunamshukuru kwa hilo.
Hatahivyo, tofauti na sisi Mwenzetu amaeachavionjo muhimu


Uchaguzi ili uwe nasifa ni lazima uwe wa haki na huru.
Na hiyo haitoshi ni lazima uwe na integratena credibility ili uweze kutoa legitimacy.


Haya HP (Humphrey Polepole) hakuyagusia kwa makusudi kabisahoja zake zilikuwa za kisiasa zaidi ya kiufundi. Zilikuwa zimelenga kutetea tu kwavile utetezi unahitajika.

Hazikuwa hoja za kushawishi mtu aliyekaa chumbani kwake nafikra sahihi

Maoni ya Jusa na Polepole ni yao kwa mitazamo yao. Hayawezikuchukuliwa kama ukweli kamili.
Hata hivyo, maoni hayo yanapaswa yaambatane nautetezi wenye mantiki, mashiko na wa kisomi. `


Kuendelea kupotosha umma ni kuendeleza dhana ile ilealiyowahi kuisema ndugu Polepole kuwa ` `TUSIONGOZWE KWA UONGO NA KUWA TAIFA LAWAONGO``

Kwa kauli hii ya HP tunapswa kuungana naye, kinyume chake tutakuwa `taifa la waongo`

Tunapaswa tuweke uongo pembeni ili kulinusuru taifa. Hapaduru hatuna utamaduni wa kumjadili mtu bali hoja

Ndivyo tutakvyojadilihoja za HP. Tukiacha uongo utamalakitutaendeleza utamaduni wa kulea viongozi waongo wakihubiri tusiseme uongo, hukuwakikaa mbele ya TV kuhusbiri uongo.


Humphrey Pole pole na hoja zake



Inaendelea sehemu ya II na III
 


Sehemu ya II

HUMPHREYPOLE POLE NA HOJA ZAKE

1) Mwenyekitiwa ZEC
HP amesema,``mwenyekiti wa ZEC akiwa kama alama `symbol` ya tume alikuwa na haki ya kutumiabusara zake kufuta uchaguzi``

Alipoulizwani kifungu gani cha sheria za uchaguzi ZNZ au katiba kinachompa, HPhana jibu.

Kwa manenomengine hakuna kifungu bali ni fikra zake tu zinazomtuma kuaminihivyo

2) Katibaya ZNZ na sheria haziwezi kumaliza mgogoro uliopo
Hapa alimaanisha kuwa tatizo lilopo haikuongelewa katika sheria au katibana kwamba busara zitumike.
HP anasahau nchi haiongozwi kwa busara, balibusara zinazosimama katika sheria

Hakuna kipengele kinachosema, yapo mambo ya kitaifa yanayotaliwa kwakut busar
Katiba na sheria za uchaguzi wa ZNZ za mwaka 2015 ndizo zilitumika katikauchaguzi wa 2010.

CUF walikuwa na malalamiko, haikutumika busara kuwasikiliza.
Leo busara inaanzaje ikiwa hatukuwahi kuwa na utatuzi wa matatizo kwabusara

Huu ni upotoshaji kwasababu sheria zipo na zinajieleza.
Msimamizi wa kituo au wa jimbo ndio ZEC .

Hakuna malalamiko ya wasimamizi, busara zipi zitumike ikiwa hakunamlalamikaj

3) Tume ya uchaguzi imejibomoa

HP anasema mgogoro wa tume kama ulivyoelezwa na mwenyekiti umeondoauhalali wa tume . Akasema tena walipaswa kushtakiwa kwa kukiuka dhamanachini ya kiapo

Hapa HP hajaeleza nani walipigana. HP hakuonyesha walipopigana hilolimeathiri vipi upigaji wa kura au kura za vituoni.

Lakini pia HP hasemi kuwatume yenye muundo huo huo anaolalamikia ndio iliyosimamia uchaguzi wa 2010.

Wapi anaweza kusema haina uhalali kwasababu ina wajumbe wa vyama

Ni chama gani kati ya CCM na CUF kilichowahi kulalamika kuhusu tume

Naje matatizo ya tume yanamalizwa kwa busara za mtu mmoja alyemwita `symbol`bilamashauriano na taasisi nyingine

HP alipoulizwa kwanini mwenyekiti wa ZEC hakuwasiliana na wa NEC kamakatiba inavyosema, hakuwa na jibu.

Hapa inaonyesha alichosema si uhalisia washeria bali ushawishi wake binafsi anaotaka umma uuone kama uhalisia.

HP anaishikwa uongo aliowahi kuukataza na kuukemea

4) CCM walalamika na tume yagawanyika

HP anasema CCM ilikuwa na malalamiko na kwavile tume ilikuwaimegawanyika, hakukuwepo na muafaka

HP hajaeleza malalamiko ya CCM yameanza lini na yalihusu nini.

Tarehekabla ya 27 CCM taifa walisema uchaguzi uliendelea vizuri.

Mawakala waohawakuawahi kutoa malalamiko na wala hakuna kituo au jimbo liloahirishauchaguzi.

Haya malalamiko ya tarehe 27 ndiyo HP anataka umma uelewe yaikuwepokuanzia mwanzo. Kama kulikuwa na malalamiko , iweje matokeo yalisaniwa na kuwekwa vituonitena na mawala wa CCM wakisain

5) Tume imegwanyika hakuna muafaka

HP anasema tume ilipokea malalamiko ya CCM. Hakueleza ni kwa barua ipi naya lini.

HP amesahau kuwa uchaguzi umefutwa na Jecha kwasababu ZEC ilionaukiukwaji mkubwa wa uchaguzi.

Hapa malalamikaji si CCM bali ZEC. Na moja yamalalamiko ni ongezeko la watu kwenye vituo vya kupigia kura

Hakuna wakala aliyefikisha malalamiko ya tarehe 25 au 26, haya ya CCM HPkayatoa wapi na lini

6. Anashauri Rais aite kikao kuwe na mjadiliano

Wakati wa uchaguzi CCM ilikuwa na mgombea kama ilivyokuwa CUF.

Leo HPanashauri mgombea wa CCM aitishe kikao kutafuta muafaka kwa kofia ya Urais.Hapa HP anategemea mtu ajihukumu mbele ya mahakama.

Huku ni kusema na kuishikwa uongo

7) Maalim Sefi katangaza matokeo na kuharibu mambo

Hp anasema haikuwa sahihi kwa maalimu kutangaza ushindi. Alipoulizwa tumeilishatangaza kupitia vituo na majimbo, HP akasema sheria inakataza.

Sheria ya uchaguzi ZNZ ina sehemu yake kwa kosa hilo.

Je, sheria ilisemahukumu ni kufuta matokeo.

Sheria inasema hukumu ni 5000 au kifungo.
Ni nanialikwenda mhakamani kumshtaki Seif.

Tunajua hilo halikuathiri kura popote palekwani lilitokea baada ya uchaguz

Hata hivyo HP anaishi kwa uongo alioukemea siku nyingi.

January Mkamba waCCM alitoa takwimu za wabunge wa CCM wakiwemo wale ktuoka ZNZ. Mbona NEChaikufuta uchaguzi.

Mbona HP hakukemea hilo katika majadiliano yake.

Nguvu ya maadili ipi inayomruhusu asikemeejambo aliloshiriki kwake bali akemee jambo kwa jirani. Huku ni kuishi kwa uong

Inaendelea…
 
HOJA ZA H.POLE POLE

Sehemu ya III
8) HP anasema hakuna ombwe la uongozi

Kwa mujibu wawanasheria wa ZNZ Bi Fatma Karume , Jusa na Said A, Rais anakoma muda wakemiaka 5 Endapo kuna tatizo lililorodheshwa katika katiba, ataendeleakwa mujibu wa katiba

HP hakuonyesha ni kifungu gani kinachoziba ombwe na aukukanusha vifungu vilivyoordheshwa na wenzake, hivyo hana ground alizoonyeshani kwanini hakuna ombwe

9) HP anahitimisha kwa kusema, busara zitumike uchaguziufanyike

Hapa HP anakubaliana na madai ya mwenyekiti wa ZEC bila kupima ukweli.
Mh Jusa kamweleza kuwa Jecha ameendakuwaomba radhi wenzake. Vipi HP haoni tatizo


Magazeti yametoataarifa (mwananchi) likiwemo, kuwa baada ya Jecha kuondoka chumba cha kuhesabukura, zoezi liliendelea chini ya makamu mwenyekiti.

Makamu aliondolewa na vyombo vya dola kwa nguvu.HP alipaswakulijua hili kama uingiliaji wamchakato
HP hakuliongeleakakomaa na hoja ya Maalim Seif kutangaza matokeo, hoja kama ya January Makamba


Kwa vile ameamua kuishi kwa kile alichosema `taifa la uongo` hatuna budi kumkubushakauli mbiu yake.

10) HP hakuzingatia madhara ya kauli yake kuhusu kurudia uchaguzi.
Maana yake ni pana,itamgusa Rais wa JMT.

Kura za WZNZ zisipohesbaiwa ina maana hawakumchauakiongozi wa JMT.


Hapa tufafanue maana wapotoshaji hawasemi ukweli.

Kunawapiga kura wa ZNZ wa Rais wa ZNZ, wawakilishi naMadiwani.

Kuna wapiga wa WZNZ pamoja nawa bara wanaoishi ZNZ ambao humchagua Rais na wabunge wa ZNZ wanaoingiaBungeni Dodoma


Maana yake ni kuwa kufutwa kwa uchaguzi wa ZNZkutaondoa WZNZ waliopiga kura kumchaguaRais wa JMT. Kura zitakazobaki ni za Wabara wanaoishi ZNZ tu

Hii itasababisha Rais wa JMT awe amechaguliwa naWaanganyika, na imwanzo wa mgogoro wa kikatiba. Kinyume chakeuchaguzi wote itabidi urudiwe Tanzania

Ndiyo maana msemaji wa kampeni wa CCM aliwahi kuelezakusikitishwa na kauli ya mwenyekiti wa ZEC.
Alijua wazi hilo ni tatizo kubwakwa upande wa CCM bara.


HP anaposhauri mambo kama haya, anapaswa aangalie kwa upanawake, si kuzungumza tu kwasababu amepewa muda na TV.

Haya ni mazoea yakujifunza kuishi kwa uongo kama anavyotushauri HP kwa kauli yake mwenyewe,ndiyo tunayoyakemea


11) Mgogoro wa ZNZhauna ufumbuzi kikatiba
Hayo ni maneno kwa mujibu wa HP. Kwamba katiba haikuwahikueleza ikitokea kama ilivyo nini suluhu yake

HP ameshindwa au anapotosha kuhusu katiba ndio maana hakuweza kufanikiwa kuudanganyaumma.

Katiba ni sheria mama au kuu ya nchi. Ndio msingi wa sheria nyinginezitakazotengenezwa na jamii, taasisi, shirika au NGO ambazo lazima ziakisisheria mama katiba


Katiba ya JMT haielezi watu wakitwangana Makonde wahukumiwevipi bwana Polepole.

Katiba imetaja tu utaratibu kuhusu makosa na haki zawatu.
Wizara ziazohusika ndizo zinatungasheria kuanisha aina ya tatizo na suluhu yake.


Ni kwa msingi huo, katiba ya ZNZ imetoa nafasi ya kuundwakwa ZEC. Na ZEC imetengenezewa sheria zake kuhusu uchaguzi. Sheriaza ZEC hazihusu kutwangana Makonde, isipokuwa zinaeleza tatizo hilo kwamuktadha wa uchaguzi.

Kila kitukinatatuliwa kwa sheria za uchaguzi. Hili suala la ZNZ ni la kisheria, nasheria zipo, kinachohitajika ni utekekelezaji tu


HP pamoja na wenzake wa CCM wanataka sheria zao ndizozitumike, kwamba uchaguzoi ufutwe.
Wanapoulizwa ni kwa mujibu gani, akina HPwanasema `kwa mujibu wa busara`


Busara maana yake ni kuongoza au kuongozwa kwa uongo kamaanavyotukumbusha HP

Hitimisho linafuata

























 


HITIMISHO LA BANDIKO

Kwanza, HP ni mwanachama hapa JF. Ana haki za kujakushauri, kukanusha, kukemea , kujadiliana au kukubaliana na hoja zetu bilakikwazo

Pili, HP ana haki ya kutoa maoni yake, ya chama chake aukikundi chochote anachohusiana nacho , haki anayopewa na katiba ya JMT , hakituliyo nayo sisi pia kama wananchi

Hata hivyo kila haki ina mipaka, na kila haki ina wajibu



RAI YETU KWA WATANZANIA WENZETU

Uchaguzi wa 2015 niwa kihistoria ikiwemo kuacha makovu.

Tunaona hali ya kutokuwa na furaha, chuki na kupungua kwamshikamano na uzalendo.

Uchaguzi umepita sote tunapaswa kuwa wadau wa amani nautulivu


Amani na utulivu haviji kama mvua bali ni kwa jitihada zetusote.

Viongozi wengi ``wameishi kwa uongo wakitanguliza matumboyao na si taifa.

Baada ya uchaguzi, vikumbo vimeondoka mitaani sasa nikuwania madaraka.

Kwa mtu aliyewahi kuonja utamu wa madaraka iwe serikali aukwenye tume yoyote inayolipa vizuri, mtu au watu hao watajitoa fahamu hata kamani kwa hasara ya taifa ili kujenga mazingira ya kuteuliwa kwenye bodi za mashirika au Tume

Ili kufanikisha haja zao za madaraka, mtu au watu hao wapotayari kusimama na kutetea chochote wakijua huo ni utetezi wa matumbo yao na sitaifa.

Wapo tayari kuishi kwa uongo, kutetea uongo, kufinyangaukweli ili mradi hata ukuu wa Wilaya wafikiriwe

Tatizo la ZNZ linatugusa kama sehemu ya nchi.
Kuliongeleakatika hoja nyepesi, zisizo na mashiko na zinazoudhi, kutaendelezatatizo kwa nchi kwa ujumla


Tuna wajibu wa kuponya`` vidonda vinavyovuja damu`` kutokanana uchaguzi`.

Tunawajbu wa kuona ZNZ inaendelea kuwa na amani na utulivu

Hilo si jukumu la vyombo vya dola, ni jukumu la kila mmojawetu.

Vyombo vya habari vina mchango mkubwa kwa hili.

Tunajua BAADHI ya wanahabari wetu uwezo wao wa kuhoji , kufafanua hoja ni hafifu nadhalili.


Inaweza kuwa nitatizo la kitaaluma au kiuchumi.

Ni wakati wa kuongeaukweli, kuridhiana ili twende mbele

Wanasheria waonge kwa lugha yao, madaktari , Walimu na engineer, na wanasiasa kwa zao p

Masuala mazito yasifanyiwe dhihaka na waganga njaa nawatafuta umaarufu

Kauli za kupotosha hazilisadii taifa zaidi ya kuamsha hisiana kutonesha makovu yanayopona

Vyombo husika vijitazame kama vimebeba dhamana ya amani nautulivu sawia.

Vyombohusika si vya dola, hata vya binafsi vina wajibu wa kutunza na kusimamia amani

Hutushauri kuminya uhuru wa watu kujieleza bali uhuru uambatane na wajibu na ukweli

Tusihubiri Amani na utulivu kama ngonjera. Sote tujitazame kwa nafasi zetu kama tunalitendea taifahaki.

Na pale tunapoona hapafai, tusimame na kukemea.

Kila chombo kiwajibike, na kisiwe mlango wa watu kutafutaumarufu kwa gharama nzito tunazoweza kuzilipa

Tusemezane

 
Sehemu ya II

HUMPHREYPOLE POLE NA HOJA ZAKE

1) Mwenyekitiwa ZEC
HP amesema,``mwenyekiti wa ZEC akiwa kama alama `symbol` ya tume alikuwa na haki ya kutumiabusara zake kufuta uchaguzi``

Alipoulizwani kifungu gani cha sheria za uchaguzi ZNZ au katiba kinachompa, HPhana jibu.

Kwa manenomengine hakuna kifungu bali ni fikra zake tu zinazomtuma kuaminihivyo
Hapa sitozungumzia uhalali au mantiki ya kufutwa uchaguzi ule bali nataka kuzungumzia uhalali wa kikatiba. Hata hivyo, ikiwa nitalazimika kuelezea mantiki, sichelei kusema kwamba ule ni uamuzi wa hovyo kabisa kupata kutokea katika kipindi cha miaka 50 ya uwezo wa Zanzibar.

Lakini nikirudi kwenye uhalali wa kikatiba, Ibara ya 119 (10) ya katiba ya Zanzibar ya 1984 toleo la 2010 inasema: "Kiwango cha mikutano ya Tume ya Uchaguzi ni Mwenyekiti au Makamo Mwenyekiti na Wajumbe wanne na kila uamuzi wa Tume ni lazima uungwe mkono na Wajumbe walio wengi."

Hapo tunapata picha moja-- kukishakuwa na wajumbe 5 including Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti, ZEC wanaweza kuitisha mkutano na kufanya maamuzi maamuzi provided "wajumbe wengi" wanaunga mkono! Ikiwa kura ya Mwenyekiti inahesabika, basi wajumbe wengi maana yake ni 3+.

Tukirudi upande wa wajumbe; Ibara ya 119 (1) inazungumzia uteuzi wa wajumbe kama ifuatavyo:
119 (1) b. Wajumbe wawili watakaoteuliwa na Rais kufuatana na mapendekezo ya Kiongozi wa shughuli za Serikali kwenye Baraza la Wawakilishi....
c. Wajumbe wawili watakaoteuliwa na Rais kufuatana na mapendekezo ya Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi au iwapo hakuna kiongozi wa upinzani basi kwa kushauriana na vyama vya siasa;
d. Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa Majaji wa Mahakama Kuu;
e. Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Rais kama Rais atakavyoona inafaa.


Hivyo basi, Ibara ya 119 b-d inatupa idadi ya wajumbe 6 wakati wanaotakiwa kufanyika mkutano ni 4 tu! Kifungu kidogo "b" wajumbe wake wamependekezwa na Balozi Seif Idd... kwa maana nyingine ni wafuasi wa CCM. Kifungu "c" wamependekezwa na Maalim Seif, kwahiyo sina shaka ni wafuasi wa CUF!

Hapo tayari kuna wajumbe 4 na linapotokea jambo lenye maslahi kwa CCM/serikali iliyopo, hao wajumbe 2 kutoka b lazima watahudhuria kikao husika na hivyo kuhitaji wajumbe wa ziada 2. Wajumbe kutoka "c" hawawezi kuhudhuria lakini wa kifungu "d" atateuliwa na Rais mwenyewe kutoka miongoni mwa majaji! Huyu lazima tu ataitika kwa mtu aliyempa madaraka ya ujumbe na hivyo hesabu kuwa 2+1! Mjumbe kutoka "e" anateuliwa na Rais mwenyewe "kama anavyoona inafaa!" Labda umwekee kisu shingoni ndipo anaweza kumteua mtu wa aina ya Jussa na sijui mtu atanishawishi vp hadi nikubali kwamba hawezi kuteua mtu mwenye kariba ya Abdallah Bulembo-- hapana, sio Bulembo kv ni mtu wa siasa za majukwaani... lakini kuna wafia CCM wangapi sehemu kama UDSM ambao hatuwafahamu kwamba ni wafia chama? I hope you got what I mean!

It doesn't take a genius to finally see this simple arithmetic finally turns to 2+1+1 = 4 thus complying 119 (10) Kiwango cha mikutano ya Tume ya Uchaguzi ni Mwenyekiti au Makamo Mwenyekiti na Wajumbe wanne na kila uamuzi wa Tume ni lazima uungwe mkono na Wajumbe walio wengi." Which means, wala hawawahitaji wajumbe 2 watakaopendekezwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani as per 119 (1) c!!! Na kama umefuatilia lile sakata, ni wajumbe wawili ndio walijitokeza kusema Mwenyekiti amefanya maamuzi peke yake... bila shaka, wale ni kutoka 119 (1) c!!!

Now, 119 (1) b, d and e wanatimiza column! Hapo Mheshimiwa Jaji (from 119-1-d) akiwa ni mtu wa kuzingatia maadili yake na kutokuwa tayari kukiuka kiapo chake cha kitaaluma; watakachomwambia ni "thanks for attending...!" lakini kura yake wala hawana shida nayo zaidi tu ya kumtaka ahudhurie coz' kila uamuzi wa Tume ni lazima uungwe mkono na Wajumbe walio wengi ambao ni WATATU... 75% excluding mwenyekiti duh! Ama kweli sheria zilitungwa kuhalalisha uovu!!!!

c.c JokaKuu, Pasco, Mzito Kabwela
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3,

Ni kama hoja zako zilitakiwa kujibiwa na Humphrey Polepole lakini ni kama hujam-mention popote kwa namna ya yeye kuweza kupata notification vinginevyo utakuwa hujamtendea haki. Siifahamu ID yake, ngoja nijaribu: Humphrey Polepole
 
Last edited by a moderator:
Ooops! It worked! Wacha nikatafute mkate wangu wa kila siku, nitarejea kwa hayo mengine.
 
HOJA YA SERIKALI 3 INAPATA NGUVU SASA

CCM walipokataa serikali 3 hawakuweza kuona mbali. Hapa duru tumewahi kuhoji sana, hivi ikiwa vyama tofauti vitashinda bara na visiwani nini itakuwa hatma ya taifa?
Hapa kinachonipa hofu si WHAT IF vyama tofauti vitashinda bara na visiwani bali WHAT IF muungano ukivunjika! Uwepo wa vyama tofauti sioni kama ni tatizo provided wote wapo tayari kuulinda muungano... tatizo litakuja pale upande mmoja utakapokosa dhamira ya kuulinda muungano na hivyo kuwa sababu ya kwanza ya kupelekea hofu yangu... WHAT IF muungano ukivunjika!

Lakini kuvunjika kwa muungano hakuhalalishwi na utawala wa vyama viwili tofauti pekee bali hata chama kile kile kikiwa kinatawala Zanzibar na Muungano, bado hakutoi guarantee ya muungano wetu kutovunjika hasa tukizingatia kulikuwa na "miungano" imara kabisa duniani ambayo ilidumu kwa miongo kadhaa tofauti na huu wa kwetu lakini siku ilipofika, muungano ulivunjika! Suala la Scotland kutaka kujitenga from UK limepitiliza level ya kuita ni red flag kwetu bali ni time bomb!

Now, let's assume LEO muungano unavunjika; je CCM watakuwa tayari kuunda serikali ya mpito instantly kwa kuwa tayari Magufuli atakuwa amepoteza uhalali wa kuongoza kv alipigiwa kura bara na visiwani?! Ni kwa muda gani CHADEMA watavumilia kusubiri uchaguzi mwingine kuitishwa na utaitishwa kwa katiba ipi?

God forbid-- hilo likitokea manake hata katiba iliyopo ita-cease kufanya kazi na taasisi pekee inayoweza kuongoza nchi pasipo na katiba ni jeshi pekee huku "wakisubiri" wanasiasa wa-resolve issues zao!
 
Mkuu Nguruvi3,

Ni kama hoja zako zilitakiwa kujibiwa na Humphrey Polepole lakini ni kama hujam-mention popote kwa namna ya yeye kuweza kupata notification vinginevyo utakuwa hujamtendea haki. Siifahamu ID yake, ngoja nijaribu: Humphrey Polepole
Nas nina uhakika ni msomaji mzuri tu maana hoja nyingi 'tunashabihiana kwa maelezo''
Sikumtaja nikijua fika ni mwanachama wa JF na msomaji mzuri hapa duru

Hata hivyo nakushukuru kwa kumualika. Na mwanzoni tumesema anakaribishwa kabisa kutoa maoni, kutufahamisha, kukanusha , kukemea na chochote ilimradi iwe katrika ustaarab na ukweli. 'Tusiobfozwe na uongo kama asemavyo, ingawa ni mhubiri mkubwa wa uongo anaoukemea''

Humphrey Polepole karibu sana
 
Last edited by a moderator:
Nas nina uhakika ni msomaji mzuri tu maana hoja nyingi 'tunashabihiana kwa maelezo''
Sikumtaja nikijua fika ni mwanachama wa JF na msomaji mzuri hapa duru

Hata hivyo nakushukuru kwa kumualika. Na mwanzoni tumesema anakaribishwa kabisa kutoa maoni, kutufahamisha, kukanusha , kukemea na chochote ilimradi iwe katrika ustaarab na ukweli. 'Tusiongozwe na uongo kama asemavyo HP, ingawa ni mhubiri mkubwa wa uongo anaoukemea''

Humphrey Polepole karibu sana
.......
 
Hapa kinachonipa hofu si WHAT IF vyama tofauti vitashinda bara na visiwani bali WHAT IF muungano ukivunjika! Uwepo wa vyama tofauti sioni kama ni tatizo provided wote wapo tayari kuulinda muungano... tatizo litakuja pale upande mmoja utakapokosa dhamira ya kuulinda muungano na hivyo kuwa sababu ya kwanza ya kupelekea hofu yangu... WHAT IF muungano ukivunjika!

Lakini kuvunjika kwa muungano hakuhalalishwi na utawala wa vyama viwili tofauti pekee bali hata chama kile kile kikiwa kinatawala Zanzibar na Muungano, bado hakutoi guarantee ya muungano wetu kutovunjika hasa tukizingatia kulikuwa na "miungano" imara kabisa duniani ambayo ilidumu kwa miongo kadhaa tofauti na huu wa kwetu lakini siku ilipofika, muungano ulivunjika! Suala la Scotland kutaka kujitenga from UK limepitiliza level ya kuita ni red flag kwetu bali ni time bomb!

Now, let's assume LEO muungano unavunjika; je CCM watakuwa tayari kuunda serikali ya mpito instantly kwa kuwa tayari Magufuli atakuwa amepoteza uhalali wa kuongoza kv alipigiwa kura bara na visiwani?! Ni kwa muda gani CHADEMA watavumilia kusubiri uchaguzi mwingine kuitishwa na utaitishwa kwa katiba ipi?

God forbid-- hilo likitokea manake hata katiba iliyopo ita-cease kufanya kazi na taasisi pekee inayoweza kuongoza nchi pasipo na katiba ni jeshi pekee huku "wakisubiri" wanasiasa wa-resolve issues zao!
Mkuu , siku zote tumewaasa CCM kuwa muungano lazima uwe katika hali ya kisheria na maridhiano.

Yaani usimame wenyewe na si kuwa usisimamishwe na kundi la watu.

Haya tunayoyaona yeote tumeyadili sana hapa. Tulisema, hali ya kisiasa inabadilika kutokana na wakati.

Nchi haiongozwi kwa 'Busara' bali sheria na kanuni.
Ndiyo maana tunasikitika sana vijana kama Humphrey wanaposema eti 'busara' zitumike kama mbadala wa sheria.

Miaka 50 bado tunadhani nchi ni dude linaloelea tu na linategemea busara za watu wawili au watatu na si sheria

Kuongoza kwa busara ndiko kulifanya CCM iamini ina nguvu sana za kidola na ujanja ujanja wa kuweka muungano sawa

Dalili za awali zilionekana wakati wa bunge la katiba. Kufeli kwa bunge la katiba chini ya Kikwete ilikuwa kiashirio kizuri kuwa mbele ya safari kuna giza.

Badala ya kurudi kwenye drawing board na kutathmini nini cha kufanya, zilitumika 'busara' za kuazima maruhani kupiga kura, marehemu n.k. Matokeo yake katiba pendekezwa ya CCM ikakwama

CCM wakaamini wataendelea kuishi kwa ujanja ujanja na uongo ambao Humphrey anaukemea ingawa sasa amepiga kona anauhubiri kwa bidii zote tena akisema busara zitumike

Ukitaka kuliona tatizo ni pale HP anapokuja na kauli kuwa katiba ya ZNZ haipo kamili kwasababu haina majibu ya tatizo ingawa katiba hiyo hiyo imetumika na akina HP tena kuandika rasimu.

Hakuona tatizo kwasababu ilikuwa katika favor ya chama chake.
Leo anasema ina mapungufu kwasababu chama chake kimepoteza ushindi

Sasa kuhusu hoja ya Rais wa JMT, hapa CCM hawana namna. Wakisema uchaguzi ufutwe basi na bara utafutwa kwasababu wapiga kura wa ZNZ hawakushiriki kumchagua Rais wa JMT kutokana na kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi

Tena ni mbaya kweli maana kufutwa kwa uchaguzi ni kutangaza kuwa siku ile ilikuwa null and void, hata zile kura kiduchu za Wabara wanaoishi ZNZ hazitakuwa na maana. Magufuli atakuwa ni Rais wa Tanganyika 'by default'

Hoja itakuja, atakuwaje Rais wa Tanganyika kwa kutumia katiba ya JMT?

CCM wakikubali uchaguzi uendelee, maana yake Rais wa ZNZ ambaye ni mjumbe wa baraza la mawaziri la JMT ataingia katika vikao ambavyo basically ni vya CCM wasiotaka mambo yao ya ndani kutoka. Wanakwama!

Kuacha hali ya ZNZ bila suluhu maana yake ZNZ itakuwa haina baraza la wawakilishi

Rais atakuwa anatawala bila mhimili mmoja kinyume na katiba ya ZNZ.

Dhambi ya kukataa maoni ya wananchi inawarudi CCM kwa kasi na hali ya kutatanisha sana

Haya ni matatizo ya kuongoza nchi kwa 'busara'' na ''uongo' kama anavyotukumbusha Humphrey Polepole'
 
NasDaz Hapo bandiko 25 umeelezea mambo mawili.
Kwanza mantiki ya suala la ZNZ na pili, uhalali wa kikatiba

Nichangie tena kidogo

Kimantiki:
Watu waelewe uchaguzi ni takwa la kikatiba iwe ya JMT au ZNZ. Imeanishwa kikatiba na ndivyo ilivyo

Uchaguzi hauwezi kufutwa kwasababu tayari ni takwa la kikatiba.

Ili uchaguzi ufutwe ni lazima kifungu kinachosema ' kutakuwepo na uchaguzi...' katika katiba zetu kifutwe kwanza
Vinginevyo midhali kifungu hicho kipo intact , uchaguzi haufutwi. Kinachofanyika ni Uchaguzi kuahirishwa

Kwa mfano, ikibainika taratibu za uchaguzi zimekiukwa na uchaguzi hauwezi kufanyika siku hiyo kabla ya kupiga kura, uchaguzi unaahirishwa hata kama ni miaka 5, haufutwi kwasababu tayari ni takwa la kikatiba na lazima lifanyike ili katiba iwe hai

Ikitokea asilimia 95 ya maeneo yana matatizo baada ya kupiga kura, uchaguzi haufutwi bali unaahirishwa katika maeneo husika. Ndio mantiki ya neno kuahirishwa na si kufutwa na ndio maana wasimimazi wa vitu na majimbo wamepewa nguvu hiyo.

Sasa kama ZNZ kuna matatizo majimbo kadhaa na imegundulika baada ya kupiga kura, kinachofuata ni kuahirisha uchaguzi wa maeneo hayo husika na si kufuta uchaguzi mzima.

Tukiendeleza dhana inayotawala ya kufuta uchaguzi ambayo kikatiba haionekani, tutaingia katika matatizo makubwa.

Ipo siku mkoa wa Tanga au Mtwara kutakuwa na matatizo, na italazimu uchaguzi mzima ufutwe.
Hili kimantiki halipo, kilichopo ni uchaguzi kuahrishwa maeneo husika

Kisheria
Kama ulivyoonyesha hapo, mwenyekiti alifuta uchaguzi kama yeye. Humphrey Poleppole anasema ni symbo ya tume na hivyo ana uwezo wa kutumia busara zake kufuta uchaguzi. Ukisoma sheria ulizoweka, mwenyekiti hakupewa nguvu hiyo

Ukisoma barua aliyotumia kufuta uchaguzi, hakusema kwa mamlaka ya tume, alisema kwa mamlaka kama mwenyekiti

Hapa ndipo tunamuuliza Humphrey Polepole, kama ametumia neno mamlaka ina maana kuna kifungu cha sheria kinachompa mtu mamalka hayo.
Ni kipi hicho? Humphrey hakukionyesha alichosema ni kuwa mwenyekiti kama symbol ametumia busara

Kama ametumia busara, ilipaswa aandike kuwa 'kwa busara zake' amefuta uchaguzi.
Hata hivyo, tungemuuliza busara zinazotokana na kifungu gani cha sheria?

Kuna kitu kinaitwa 'Prerogative' yaani mamlaka au nguvu maalumu anazopewa kiongozi katika kutekeleza majukumu yake

Kwa mfano, nchi kwenda vitani inahitaji kupata kibali cha Rais kufanya hivyo.
Hata hivyo Rais ana prerogative ya kuamua kupeleka jeshi kabla ya hapo kwa kutumia busara, si mamlaka ya busara

Hii maana yake ni kuwa Rais anapewa nguvu fulani ya kumwezesha kutekeleza majukumu yake. Nguvu hizo zipo kisheria

Anpofanya hivyo anatumia prerogative akiongozwa na busara, si busara zake tu kwakuwa ameamua hivyo kama Humphrey anavyouaminisha ulimwengu

Sasa, swali linakuja, kufuatana na vifungu alivyonukuu NasDaz hapo bandijo 25, ni wapi mwenyekiti wa tume amekaa hata na wajumbe wake 3 tu na kufikia hitimisho la kufuta uchaguzi?

Hapa ieleweke kufuta tu si sahihi, bali usahihi ni kuahirisha. Hata kama uchaguzi mzima wa ZNZ ungekuwa na matatizo na tume kwa ujumla wake wakaamua urudiwe, haiwezi kusemwa umefutwa, bali umeahirishwa kwasababu ni takwa la kikatiba kwamba siku moja lazima ufanyike

Tusemezane
 
Last edited by a moderator:
NasDaz,

..asante kwa mchango wako hapo juu.

..mimi bado naugulia kipigo tulichopata huku Tanganyika.

..kwa kweli siko sawasawa sasa hivi siwezi kuchangia ya Znz.
 
Last edited by a moderator:
NasDaz,

..asante kwa mchango wako hapo juu.

..mimi bado naugulia kipigo tulichopata huku Tanganyika.

..kwa kweli siko sawasawa sasa hivi siwezi kuchangia ya Znz.
Mimi bado nina maswali. Hivi mbunge, diwani wanawezaje kuwa wa upande mmoja, Rais akachaguliwa upande mwingine. Je, Watanzania wanachagua sura au sera

Hivi Jiji linawezaje kuangukia upande mmoja, halafu Urais uka angukia upande wa pili

Kwanini kulikuwa na jitihada za kuzima makundi mengine yaliyokuwa yanakusanya matokeo. Kama kila jambo lilikuwa halali kwanini kificho ficho!

Hali inayoonekana znz inaakisi sana hali iliyokuwepo Bara. Nini kimetokea, sijui

Hata hivyo, wengine tulisema, huwezi kuwa na kesi ya kuliwa mahindi na tumbili, wakati nyani ni hakimu na sokwe ni mwendesha mashtaka, Impossible
 
BUSARA ZA HUMPHREY POLEPOLE

Katika mahojiano na kitu cha Runinga(uzi upo na video zipo) HP anasema suluhu ya matatizo ya ZNZ haipo kisheria na wala haiwezekani kikatiba. Hoja yake kubwa ni kuwa hakuna sheria inayoeleza hali ikiwa hivyo nini kifanyike

Well, sheria zipo za uchaguzi na zinaeleza hali ikitokea abacd nini cha kufanywa.
Hp anashauri busara zitumike kumaliza suala la ZNZ. Hapa akimaanisha katiba na sheria za ZNZ zina mapungufu.

Katiba na sheria hizo zimepitiwa na wataalamu na kupigiwa kura na WZN.
Ni jambo lisilo na busara kwa mtu mmoja kuziona hazikukamilika ili hali zimetumika miaka ya nyuma

Mwenzetu anachosema ni kuwa sheria ziwekwe pembeni busara zitawale

Tumkumbushe kuwa, hakimu anapomhukumu mtu hutoa adhabu kwa majibu wa sheria zilizopo.

Hata hivyo, kwa kuzingatia busara zake, adhabu inaweza kuwa tofauti kidogo.
Mfano, kama kosa ni la kwenda jela miaka 5, hakimu anaweza kumhukumu mtu kifungo cha nje

Pengine mtuhumiwa ana watoto 37 na kati yao 8 ni wagonjwa na wanaohitaji utegemezi wa mshatakiwa.
Hivyo busara za hakimu ndizo zinamwezesha kutoa hukumu ya kiufungo cha nje.

Hata hivyo, hakimu hatumii busara hizo nje ya sheria
Bado mtuhumiwa atakuwa na hatia na atahukumiwa kwa sheria, ingawa busara zimetawala

Maana yake ni kuwa sheria imetawala suala zima na busara ikizingatiwa.

Hakimu hawezi kuweka sheria pembeni kwasababu yeye ni 'symbol' ya mahakama na kusema sasa tutumie busara maana La hasha, sheria kwanza busara zinafuata

Mwenzetu anaposhauri sheria ziwekwe pembeni ili busara iamue mshindi wa uchaguzi, inatutia hofu sana na hoja zake

Tutakuwa tunajenga taifa kwa misingi ya BUSARA badala ya sheria.

Tutakuwa sawa na wanyama mwituni

Asichotuambia mwenzetu ni vifungu vinavotoa haki za busara hizo

Na kwa ushauri wa HP uchaguzi ufutwe na busara zinasema Rais wa JMT atakuwa amechaguliwa kwa busara tu

Kwamba kura za ZNZ zikifutwa, tukae kama taifa tutumie busara kuhalalisha uchaguzi wa upande mmoja, busara zinasema!

Busara za HP zinasema, Rais wa ZNZ yupo hakuna ombwe.

Tukimuuliza kwa mujibu wa kifungu gani, hatuambii, bali tuahitaji kutumia busara. Kwamba, sasa ni taifa la busara , sheria baadaye

Pengine lipo tusiloelewa kutokana na busara za HP. Tafadhali Humphrey Polepole mwenzetu jamvini karibu hapa utusaidie, pengine upo sahihi ni kwavile tu hatutumii busara kukuelewa.

Tumia busara zako kuja kusemezana nasi katika kulijenga taifa
 
images
 
Kifungu cha 41(6 & 7) cha katiba yetu na 42 (1) vinazuia kwa makusudi kabisa ulichokisema cha haki, integrity na credibility ya uchaguzi wa Rais.

Kwa makusudi mazima ya ki-mfumo na utendaji, na madhaifu haya ya kikatiba ambayo yanaondoa kutokea kwa pingamizi lolote, chama kilicho na madaraka au kuwa na mamlaka wakati uchaguzi ukifanyika na hata kuwa na nguvu na mamlaka ya kuunbda tume, kinajitengenezea mazingira ya kujihakikishia ushindi wa Urais bila kupingwa na kuharakishwa si kutangazwa pekee bali hata kuapishwa.

Hivyo kwa upande mmoja, unafuta kwa makusudi kuwasilishwa kwa pingamizi mahakamani.

Lakini kipengele hiki kina utata.

Kina utata kutokana na tafsiri nyingine ya kimahakama ya kusikiliza shauri lolote la mtu Raia na Mkazi wa Jamhuri ambaye ataonelea kuwa haki yake imedhulumiwa au kuonewa.

Sehemu ya tatu ya katiba, Haki na Wajibu Muhimu: Haki ya Usawa, mtiririko mzima unaonyesha wazi ni vipi haki inaweza kupiganiwa na kulindwa kikatiba.

Kipengele 13;(6) (a)
(6) To ensure equality before the law, the state authority shall make procedures which are appropriate or which take into account the following principles, namely (a) when the rights and duties of any person are being determined by the court or any other agency, that person shall be entitled to a fair
hearing and to the right of appeal or other legal remedy against thedecision of the court or of the other agency concerned;

(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatiamisingi kwamba -(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitajikufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombokinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa nahaki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, napia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine yakisheria kutokana na maamuzi ya mahakama auchombo hicho kingenecho kinachohusika


Ikiwa matokeo ya ubunge yakishatangazwa aliyewekewa pingamizi bado anaapishwa mpaka kesi iende mahakamani, kwa nini sheria au kanuni hizo hizo hazitumiki kwa mgombea Urais?

Utata na udhaifu wa katiba an sheria za uchaguzi na hata kutokuwa na uniformity ya kanuni, katiba na sheria za uchaguzi wa Rais na Wabunge , ni kichocheo pekee cha kuhitaji kuandikwa upya kwa uharaka marekebisho ya Katiba, sheria na kanuni za uchaguzi ili kuondoa utata na hisia za upendeleo na uhujumu wa upigaji kura na kuupa uchaguzi mzima integrity na credibility.

Aidha mfumo wa tume, mfumo wa uchaguzi unachangia sana matatizo haya tuliyoyapuuzia 2000, 2005, 2010 na sasa 2015.

Mchakato wa kutafuta wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na urais ungefanyika kwa kipindi cha mwaka mzima ili kuruhusu ushiriki wa kikamilifu wa wananchi na kuwapa nafasi kuwachuja na kuwapima wagombea na hata kura za maoni za ndani ya vyama kufanyika kwa haki na wagombea walioshinda ndani ya mchakato wa ndani ya chama wanapewa nafasi ya kugombea na kuheshimu demokrasia na kauli za wanachama waliowaamini wanachama wao kugombea nafasi hizo siku ay uchaguzi ikifika.

Tuelimishane.
 
Baadhi ya vifungu katiba JMT

66.-(1) Bila yakuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge,yaani (c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutokamiongoni mwa wajumbe wake

79. Baraza la Wawakilishi litaweka utaratibu litakaoufuatakwa ajili ya kufanya uchaguzi wa Wabunge waliotajwa katika ibara 66(1) ( c) yaKatiba hii
74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri yaMuungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:- ??.
(5) Rais aweza tukumwondoa katika madaraka Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwakutekeleza kazi zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au kwasababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe
(11) Katikakutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzihaitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote yaSerikali, au maoni ya chama chochote cha siasa
(12) Hakuna mahakamayoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tumeya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katibahii
(13) Katika utekelezajiwa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri yaMuungano itashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya Tanzania Zanzibar
90.-(1) Baada yaUchaguzi Mkuu Rais ataitisha Mkutano wa Bunge Jipya ufanyike kabla ya kupitasiku saba tangu kutangazwa matokeo ya huo Uchaguzi Mkuu katika majimbo yauchaguzi yote isipokuwa katika majimbo yale ambako uchaguzi umefutwa nakufanywa upya
 
NasDaz Hapo bandiko 25 umeelezea mambo mawili.
Kwanza mantiki ya suala la ZNZ na pili, uhalali wa kikatiba

Nichangie tena kidogo

Kimantiki:
Watu waelewe uchaguzi ni takwa la kikatiba iwe ya JMT au ZNZ. Imeanishwa kikatiba na ndivyo ilivyo

Uchaguzi hauwezi kufutwa kwasababu tayari ni takwa la kikatiba.

Ili uchaguzi ufutwe ni lazima kifungu kinachosema ' kutakuwepo na uchaguzi...' katika katiba zetu kifutwe kwanza
Vinginevyo midhali kifungu hicho kipo intact , uchaguzi haufutwi. Kinachofanyika ni Uchaguzi kuahirishwa

Kwa mfano, ikibainika taratibu za uchaguzi zimekiukwa na uchaguzi hauwezi kufanyika siku hiyo kabla ya kupiga kura, uchaguzi unaahirishwa hata kama ni miaka 5, haufutwi kwasababu tayari ni takwa la kikatiba na lazima lifanyike ili katiba iwe hai

Ikitokea asilimia 95 ya maeneo yana matatizo baada ya kupiga kura, uchaguzi haufutwi bali unaahirishwa katika maeneo husika. Ndio mantiki ya neno kuahirishwa na si kufutwa na ndio maana wasimimazi wa vitu na majimbo wamepewa nguvu hiyo.

Sasa kama ZNZ kuna matatizo majimbo kadhaa na imegundulika baada ya kupiga kura, kinachofuata ni kuahirisha uchaguzi wa maeneo hayo husika na si kufuta uchaguzi mzima.

Tukiendeleza dhana inayotawala ya kufuta uchaguzi ambayo kikatiba haionekani, tutaingia katika matatizo makubwa.

Ipo siku mkoa wa Tanga au Mtwara kutakuwa na matatizo, na italazimu uchaguzi mzima ufutwe.
Hili kimantiki halipo, kilichopo ni uchaguzi kuahrishwa maeneo husika

Kisheria
Kama ulivyoonyesha hapo, mwenyekiti alifuta uchaguzi kama yeye. Humphrey Poleppole anasema ni symbo ya tume na hivyo ana uwezo wa kutumia busara zake kufuta uchaguzi. Ukisoma sheria ulizoweka, mwenyekiti hakupewa nguvu hiyo

Ukisoma barua aliyotumia kufuta uchaguzi, hakusema kwa mamlaka ya tume, alisema kwa mamlaka kama mwenyekiti

Hapa ndipo tunamuuliza Humphrey Polepole, kama ametumia neno mamlaka ina maana kuna kifungu cha sheria kinachompa mtu mamalka hayo.
Ni kipi hicho? Humphrey hakukionyesha alichosema ni kuwa mwenyekiti kama symbol ametumia busara

Kama ametumia busara, ilipaswa aandike kuwa 'kwa busara zake' amefuta uchaguzi.
Hata hivyo, tungemuuliza busara zinazotokana na kifungu gani cha sheria?

Kuna kitu kinaitwa 'Prerogative' yaani mamlaka au nguvu maalumu anazopewa kiongozi katika kutekeleza majukumu yake

Kwa mfano, nchi kwenda vitani inahitaji kupata kibali cha Rais kufanya hivyo.
Hata hivyo Rais ana prerogative ya kuamua kupeleka jeshi kabla ya hapo kwa kutumia busara, si mamlaka ya busara

Hii maana yake ni kuwa Rais anapewa nguvu fulani ya kumwezesha kutekeleza majukumu yake. Nguvu hizo zipo kisheria

Anpofanya hivyo anatumia prerogative akiongozwa na busara, si busara zake tu kwakuwa ameamua hivyo kama Humphrey anavyouaminisha ulimwengu

Sasa, swali linakuja, kufuatana na vifungu alivyonukuu NasDaz hapo bandijo 25, ni wapi mwenyekiti wa tume amekaa hata na wajumbe wake 3 tu na kufikia hitimisho la kufuta uchaguzi?

Hapa ieleweke kufuta tu si sahihi, bali usahihi ni kuahirisha. Hata kama uchaguzi mzima wa ZNZ ungekuwa na matatizo na tume kwa ujumla wake wakaamua urudiwe, haiwezi kusemwa umefutwa, bali umeahirishwa kwasababu ni takwa la kikatiba kwamba siku moja lazima ufanyike

Tusemezane
Nguruvi3,

Ahsante kwa ufafanuzi wako. Kwanza nitangulie kusema jambo moja. Baada ya kuandika post zangu hapo juu, nikaondoka lakini baadae nilipokuja kutulia nikajiuliza... hivi Mwenyekiti wa ZEC alifuata mkondo upi katika kufuta uchaguzi. Baada ya kurejea taarifa mbalimbali, nashawishika kuamini kwamba, kutaja pungufu moja moja kama kigezo cha kukosekana uhalali wa kufuta uchaguzi itakuwa ni kuwapa credit ZEC manake nimeona watu tunajikita sana kwenye "kuharibika" kwa uchaguzi kisiwani Pemba huku wengine/wajumbe wa baraza la wakionesha vyeti vilivyothibitisha ushindi wao. Nasema tukijikita kwenye pungufu moja moja ni kuipa Credit ZEC kwa sababu ni rahisi kwao kusema hawakufuta uchaguzi kwa sababu tu Pemba kulivurugika bali kuvurugika kwa Pemba ni moja tu ya sababu za kufanya hivyo hasa nikizingatia kwamba wametaja sababu kadhaa!!! Likewise, tukijikita kwenye maelezo ya kuharibika kwa uchaguzi Pemba bila kujali kama ni kweli au si kweli; kwa maana nyingine ni kwamba tunatoa uhalali wa ZEC kufuta (au kusimamisha kama unavyosema) uchaguzi wa Pemba na kuitishwa wakati mwingine.

Kwa maoni yangu, ikiwa kafanya maamuzi ya kufuta uchaguzi kwa kuangalia barua yake kwamba "....kwa uwezo nilionao natangaza rasmi kwamba uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa...." basi uamuzi huo moja kwa moja ni batili bila kujali ikiwa ni kweli kulikuwa na hayo mapungu au hayakuwepo! Na si tu maamuzi hayo ni batili katika kufuta bali hata kama ingekuwa ni kuahirisha kufuatia ufafanuzi wako kwamba uchaguzi huwa haufutwi bali, penye matatizo huahirishwa tu kama ambavyo uliahirishwa Dar es salaam 1995.

Na nikitaka kueleza kwa uchache kuhusu suala la matumizi ya busara; ni sheria peke yake ndiyo inaweza kuchukua uamuzi wa hatari namna hiyo; kwa maana, hata kama kisheria angekuwa na nguvu hizo, basi huenda busara ingeshawishi vinginevyo endapo kweli wangetaka kutumia busara. Kwa maana, hata kama sheria ingekuwa inampa nguvu Mwenyekiti kutoa maamuzi, basi kwa kuangalia unyeti wenyewe, panapo matumizi ya busara angeita team mzima ya ZEC na hata kuomba ushauri NEC na endapo ingebidi, angekutanisha hata pande hasimu!

Itoshe tu kusema kwamba, kama kuna nguvu ya kisheria aliyonayo katika hili, sawa lakini kusema busara ilitumika; HELL NO!
 
Last edited by a moderator:
Mimi bado nina maswali. Hivi mbunge, diwani wanawezaje kuwa wa upande mmoja, Rais akachaguliwa upande mwingine. Je, Watanzania wanachagua sura au sera

Hivi Jiji linawezaje kuangukia upande mmoja, halafu Urais uka angukia upande wa pili
Hili la mbunge kuangukia chama kingine na rais chama kingine ni jambo la kawaida kabisa! Binafsi, sikumpigia Lowassa kwa sababu ambazo tayari nilishazieleza hapa jamvini lakini hata hivyo ubunge na udiwani nilipigia upinzani! Kuna bro wangu yeye ni mtu wa kawaida kabisa... I hope unanielewa namaanisha nini! Yeye nilipomuhoji akasema wazi kwamba Urais amempigia Magufuri lakini ubunge na udiwani akampigia mtu wa UKAWA!

Tukirudi kwenye matokeo kwa ujumla hapa tusisahau kwamba CHADEMA walitumia nguvu kubwa sana kujijenga Kanda ya Ziwa na kwa kweli walifanikiwa. Ukichukua mikoa 4 ya kanda ya ziwa; Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga; watu ambao walijiandikisha walikuwa 3.8 million. Huu ni mtaji mkubwa sana kwa chama chochote. Hao watu 3.8 million ni sawa na waliojindikisha Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Manyara ambazo ndio nguzo za CHADEMA. Hata hivyo, Mbeya sio maeneo yote. Kwa bahati mbaya, kura za mikoa (hiyo 4) ambayo ni ngome ya CHADEMA zikawa dissolved na kura za ngome nyingine ya CHADEMA, yaani kutoka Kanda ya Ziwa ambao waliamua kumpigia kura mtu wa kwao! Kwahiyo investment ambayo CHADEMA waliifanya kwa miaka kadhaa ndani ya kanda ya ziwa ikapotea mara moja tu baada ya CCM kumpitisha mtu wa kanda ya ziwa. Kwa tabia za Kiafrika, ni ngumu sana watu waache kumpa kura za urais mtu wa kwao.

Ukiondoa hiyo mikoa 4, CHADEMA wangeweza kufurukuta tu Mara na kidogo Kagera lakini mikoa mingine yote ambayo ilibaki ilikuwa ni ngome ya CCM except for Dar es salaam at least kwa uchaguzi uliopita. Kwa bahati mbaya, kama unavyofahamu watu wa Dar es salaam kwa kujifanya wapo bize, nilipiga hesabu za haraka haraka na kukuta waliojitokeza kupiga kura ni around 55-57%!

Binafsi nilipokuja kuona kumbe Tabora, Tanga, Dodoma na Morogoro kwa ujumla wao wana wapiga kura wengi kuliko Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Mbeya kwa ujumla wake tayari nikaona ugumu walionao UKAWA huku kanda ya ziwa ikiwa inatafuta nani wa kui-dissolve!

Hivyo basi, waliosaliti UKAWA ni watu wa kanda ya ziwa ambao waliamua kumpigia mtu wa kwao na Dar es salaam ambao hawakujitokeza kwa wingi!
 
Back
Top Bottom