Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Safari ya Zanzibar bado?
Niliona mwaliko hapa jukwaani!
Habari za mchana wapendwa,
Leo nasukumwa kusema haya. Nimekuwa nikiwatazama watu wa jinsia tofauti kwa mtizamo wangu na mwishowe kumuweka huyo mtu kwenye kundi ninaloona anafaa. Hii imenisababishia hadi sasa siko kwenye mahusiano maana nimekuwa nikijiona niko juu ya hao wote ninaokutana nao.
Nomba msinielewe vibaya, si kuwa ninawasengenya au kuwasema watu niliokutana nao maana sitawataja hapa ila ntaongelea jinsi nilivyokuwa nawachukulia.Tangu niko mschana nimekuwa nikipenda niwe na mwanaume ambaye amenizidi kwa asilimia 40 hadi 60 kwenye nyanja zote.
Yani nakuwa nina furaha iwapo nakuwa na mwanaume anizidi kiumri, kimaarifa, kielimu, kiustaarabu, anizidi kimaamuzi, kiuchumi, uwezo wa kutafsiri mambo na hata kimtazamo kwa ujumla.
Mfano, huwa nagundua mwanaume ninayetoka naye nimemzidi kiuchambuzi au kiutambuzi pale ambapo tunakuwa tunaangalia movie ambapo wote mnaangalia hiyo movie halafu unakuta anakuuliza sasa hapo alipofanya hivo ndo anamaanisha nini, to me that's a negative sign to go on with that relationship.
Kama huwa anafanya hivo ili kunogesha tuu maongezi au kuuliza tuu maswali kama maswali ya kimapenzi yaanimie huwa naboreka na huwa sijibu swali.Utakuta imefikia kipindi kwenye hiyo movie wana kiss on the move to make love halafu unakuta jamaa anakuuliza, ndo wanataka kufanyaje hapo mie kimoyomoyo.
Are you blind!? Kwa wana saikolojia huwa wanatumia picha au michoro flani kisha wanakupa uitafsiri ili kujua akili yako inaweza kuona nini na nini na unaweza kuitafsiri hiyo picha beyond au utaishia kutafsiri tukio moja tuu wakati picha inazaidi ya message moja.Sasa utakuta unatoka na mwanaume kwenye maonesho ya painting.
I like painting so huwa naenda sana kwenye maonesho ya picha na vitabu) sasa mnasimama kwenye picha au paint mojawapo halafu unaitizama na kuanza kuidadavua emotionally in my thinking kasha unamuuliza what do you see in this picture anakwambia flowers yaani najikuta nakuwa demoralized kuendelea kuwa nae I just keep myself off that relationship.
Si kuwa nawaona hawana akili ila kutokana na mie kuona kuwa naweza kuchambua vitu zaidi yake naona siwezi kuwa chini yake maana ideas zake ntaziona ziko low na ntaona kama ananirudisha nyuma kila nnachotaka kufanya.Kitu kingine huwa namuona mtu niliyemzidi ideas, thinking ntakuwa kama namburuza na mwisho kuniona mie ni kiburi.
My thinking has made me to date being single and I don't think if I can intermingle. Yes I go out with a man, we talk, we chill, we dance da da da of we go no string attached lools. Hope sijamsema mtu hapa zaidi nimejidadavua mwenyewe.
Am I overconfidence!?
Iftar njema.
Kasie.
Mpaka nimehisi kichwa kinauma maana Kwa hilo hakuna wa kuweza kukubadilisha zaidi ya Allah mlezi wako maana mapenzi na na uelewa wa vitu ni vimepishana sana ila nakushauri jifunze kuangalia anaefiti katika mapenzi yako ukiona anakufurahisha na kukuhandle vyema tulia nae na uwe tayari Kwa lolote juu yake, mengine achana nayo maana huko unakoelekea utakuja kupata maumivu yakukufanya uone dunia ni mbaya sana kuwa makini sana katika mapenzi yanahitaji vitu vidogo sana lakini vingi mno
Am I overconfidence!?
Kasie.
Cc: Mwalimu wako wa kizungu Nyani Ngabu
Not yet, nasubiria mfungo uishe ili nijiachie vizuri haswa kule beach
Kwa lugha nyingine hutaki kuwa Ng'ombe, unataka kuwa mkia, yaani kutingishwa tingishwa tu. Nyie viumbe sijui mtajielewa lini, mkienda shule noma, msipokwenda shule ndiyo noma kabisaa!! Halafu ukimpata anayekuzidi kila kitu utalalamika anakunyanyasa kwa kuwa kakuzidi kila kitu. Badilikeni.
Ngumu sana kupata mtu anaejua kila kitu aisee bila kujali jinsia na hii inategemeana na hobby kwani kila mtu hubase kule kwenye Hobby yake mfano wewe utakuwa vizuri sana kwenye muziki wa R&B sababu ndo music unaoufeel sana so ikipigwa R&B tukiwa pamoja sababu najua we unajua hizo nyimbo si mbaya nikikuuliza hivi wimbo huo kaimba nani....Na mimi nipo fit kwenye hip hop so ikipigwa Dum Dums ya Das EFX naukaona natikisa kichwa na kutiririka mashairi yake sintakuona hujui utakaniuliza eti mchumba huo wimbo kaimba nani vile...Ndo hivyo hakuna anaejua kila kitu kila wakati ndo maana we ni dokta utamhitaji mwanasheria katika kesi zako....
utapitia wengi sana kabla ya kukutana na aliekuzidi 40-60% kwenye nyanja zote!!!! kama mimi hapo kwenye paint tu ungeshanimwaga maanake ningekuwa natazama vitu vingine kabisa probably mchoraji, badala ya paint yenyewe! mambo ya akina Picasso?! bado sana
Mimi naona una akili mbaya sana wewe mwanamke japo naelewa unachomaanisha. Mimi sipendi mwanamke ambaye hawezi hata kurekebisha alarm kwenye simu yake ila sitamkinai kwa sababu hiyo tu..!!