Sawa. Sasa umeweka vema. Mwanzoni nilikuw na mawazo ya majumbani. Miti mizuri kwa hicho unachotaka ni hii hapa chini (fungua link). Kitaalamu huitwa Milicia excelsa. Uitaji majina kwa mimiea ni kizungumkuti, utaona hapo common name wameuita mvule (sina hakika kama ndo mivule hiyo). Ni miti safi mno. Inanyooka na kuwa na mbao ngumu safi sana. Changamoto yake ni kukua taratibu. Mti mwingine ninaona unatumika sana Uchagani ni Grevillea. Cheki link ya pili. Hii haichukui muda kukomaa, nayo ni chanzo kizuri cha mbao laini.
1.https://en.wikipedia.org/wiki/Milicia_excelsa#/media/File:Milicia_roadside_small.jpg
2.https://en.wikipedia.org/wiki/Grevillea_robusta#/media/File:Silveroak.jpg
zingatia
Hali ya hewa ya mahali ulipo ni muhimu sana. Waone wataalamu wa misitu wakupe shule na ushauri.Popote ulipo, tafuta ofisi za wakala wa misitu, huwa wanauza mbegu za miti ya aina nyingi. Ninajua Morogoro,kwa mfano, wapo. Usiende kwa wabongo, akina sisi tunaojiuzia miti chini ya kivuli,nenda ama tafuta mtaalamu.