Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,828
- 3,579
Hii kauli nimeisikia jana akilalama mama mmoja katika mazungumzo na wenzie kibarazani. Anadai ametunza mtoto peke yake kwa mahangaiko makubwa, kamsomesha kwa tabu kwa pesa za kuokoteza kwenye vigenge, upatu na misaada ya kaka zake. Lakini ameshangaa sana mtoto alipomaliza chuo na kuanza kupata kipato.
Mtoto ameanza kuzunguka huku na huko akiulizia ukoo wake! Huyo mama anadai amemfuma kijana akiwa anaongea na mtu wa ukoo wa babake ambaye huyo mama anamweleza kama kisirani kabisa hataki asogeze pua karibu na mwanae. Anadai amemtishia mtoto wake kuwa akiendelea kutafuta hicho anachodai ni ukoo wake, eti atamlaani!
Nauliza akina mama, hii ni sahihi? Kwanini hutaki mtoto ajue ukoo wake? Kila binadamu ana haki ya kuijua asili yake, hata kama humpendi huyo babake.
Kama unamchukia kiasi hicho huyo baba mtoto na ukoo wake wote, kwanini ulimpa? Si ungemnyima tu kuepusha shari? Mtoto hajahusika na kosa lako/lenu/la babake, kwanini unamnyima haki? Huoni kuwa huo ni unyanyapaa mtoto ajisikie kama mtu aliyeokotwa tu?