Ndama Jeuri
JF-Expert Member
- Jul 9, 2015
- 1,520
- 1,504
Hakuna mama mwenye akili timamu ambae atakataa matunzo kutoka kwa mzazi mwenzie Ni wazi baba alikua hawajibiki Kama baba angekua na nia ya kulea mtoto tangu mwanzo mtoto angemjua baba yake na hizo hasira za uyo mama zisingekuwepo kiasi hicho wababa wanasemaga hawalei acha walelewe huko wakikua watanitafuta Sasa hiyo inatia hasira unawajibika kulea halafu unataka kufaidi matunda ya mtoto kkkk
Mimi nilikuwa natoa matunzo since mtoto akiwa tumboni mpaka amezaliwa na ana mwaka mmoja sasa na bima ya afya nimemkatia akiwa na miezi miwili tu,cha ajabu anadai nimemtelekeza mtoto,kwa sababu baada ya kumlipia mahari kwao nikavunja uhusiano baada ya kuona si familia sahihi kuweza kuoa,kuna mambo yaliyotokea baada ya kulipa mahari,so now nimemwambia siwezi kutoa hata mia mpaka aende ustawi au mahakamani ili nitolee matunzo huko na imepita miezi miwili since nisitishe kutoa huduma kwa mtoto,kama unatoa matunzo na anakugeuka,je akifika miaka mitano akageuza kibao kuwa ulikuwa humtunzi mtoto je?Kwa akili ya haraka tu nimegundua huyo mama mwenyewe anashida ndio maana kumekuwa na kukosekana kwa ushirikiano wa kutoka upande wa pili.
Wanawake mjifunze sana binafsi nina mtoto yupo standard two namsomesha shule ya kulipia mwanzoni nilikuwa naletewa report za shule matokeo ya mitihani everything lkn saizi sijamuona mtoto since 28 December 2020 wala test na kila kitu nimelipa mpaka transpo je wapi nimekosea?
Je nikiamua kususa nikae pembeni itakuwaje ?