Mitoto unaihangaikia peke yako ikifika ukubwani inaenda kutafuta ukoo wao...

Mitoto unaihangaikia peke yako ikifika ukubwani inaenda kutafuta ukoo wao...

Ni kweli mama lazima akasirike na mtoto lazima uwe na huruma kwa mama / kwa mlezi wako. Mimi nimelelewa na mama na baba wa kambo ukoo wangu kwa baba nawajua ila sina Shobo nao na wale wachache niliowahi kukaa nao niliwaambia najisikia amani zaidi nikiwa na ndugu wa kwa mama kuliko kwa baba. Japo hawakunielewa / hawanielewi huo ni msimamo wangu. Nalia na aliyelia nami kipindi sijiwezi. Japo siyo kamanina pesa hapana.
Safi [emoji122]
 
Kuna kitu nime jifunza Kwa wa Zanzibar wao ukizaa na mwanamke nje ya ndoa wana Amin mtoto siyo wao ni wa Mwanamke kwaiyo Mwanamke itakubid umtunze mwao tokea mdogo mpaka aweze kujitegemea bila msaada wowote kutoka kwa ndugu wa upande wa mwanaume, kuna rafiki yangu alizaliwa nje ya ndoa sasa kuna siku alienda Kwa Baba yake Baba yake aka mwambia ukiwa una kuja nyumba kuonana na Mimi husiniite Baba niite Mzee Juma, Yan nilishangaa kweli Nika staajabu kwel na nikawaza mbali .
Aisee [emoji848]
 
Mimi nilikuwa natoa matunzo since mtoto akiwa tumboni mpaka amezaliwa na ana mwaka mmoja sasa na bima ya afya nimemkatia akiwa na miezi miwili tu,cha ajabu anadai nimemtelekeza mtoto,kwa sababu baada ya kumlipia mahari kwao nikavunja uhusiano baada ya kuona si familia sahihi kuweza kuoa,kuna mambo yaliyotokea baada ya kulipa mahari,so now nimemwambia siwezi kutoa hata mia mpaka aende ustawi au mahakamani ili nitolee matunzo huko na imepita miezi miwili since nisitishe kutoa huduma kwa mtoto,kama unatoa matunzo na anakugeuka,je akifika miaka mitano akageuza kibao kuwa ulikuwa humtunzi mtoto je?
Duh Kama Ni hivyo pole Sana jaribuni kuweka kikao na watu wazima na yeye mnaweza kupata muafaka namna ya kumtunza mtoto
 
Hii kauli nimeisikia jana akilalama mama mmoja katika mazungumzo na wenzie kibarazani. Anadai ametunza mtoto peke yake kwa mahangaiko makubwa, kamsomesha kwa tabu kwa pesa za kuokoteza kwenye vigenge, upatu na misaada ya kaka zake. Lakini ameshangaa sana mtoto alipomaliza chuo na kuanza kupata kipato.

Ivi wewe Mtoto azaliwe uletewe umkatae alelewe mwaka mmoja mpk 27 bila msaada wowote na pengine upo kwenye nafasi nzur ya kutoa msaada af hutoi...dah af mi ndo Anko ake na uyo Mtoto aisee utaisoma namba
 
Mtoto ameanza kuzunguka huku na huko akiulizia ukoo wake! Huyo mama anadai amemfuma kijana akiwa anaongea na mtu wa ukoo wa babake ambaye huyo mama anamweleza kama kisirani kabisa hataki asogeze pua karibu na mwanae. Anadai amemtishia mtoto wake kuwa akiendelea kutafuta hicho anachodai ni ukoo wake, eti atamlaani!

Nauliza akina mama, hii ni sahihi? Kwanini hutaki mtoto ajue ukoo wake? Kila binadamu ana haki ya kuijua asili yake, hata kama humpendi huyo babake.

Kama unamchukia kiasi hicho huyo baba mtoto na ukoo wake wote, kwanini ulimpa? Si ungemnyima tu kuepusha shari? Mtoto hajahusika na kosa lako/lenu/la babake, kwanini unamnyima haki? Huoni kuwa huo ni unyanyapaa mtoto ajisikie kama mtu aliyeokotwa tu?
Kuna wakati mwingine kina Mama wanakosea wenyewe, wanamficha mtoto ukweli kuhusu baba yake na ukoo wake kisa eti babake alimtelekeza. Zamani wanawake waliweza kutudanganya kuhusu watoto wetu ila siku hizi kuna msema ukweli aitwaye DNA ambaye anapingwa na kila mwanamke. Utakuta mwanamke hata kama kaolewa anajirusha na mtu bila kinga mwisho wa siku akipata ujauzito anatafuta mwanamme aliyetulia atajirahisisha kwake kisha aje kumsakizia mtoto ambaye si wake. Mwanamme mwerevu anaomba matokeo ya DNA, Mama anapinga na kumkataza mwanawe kujihusisha na baba yake na ukoo wake.
 
Hii kauli nimeisikia jana akilalama mama mmoja katika mazungumzo na wenzie kibarazani. Anadai ametunza mtoto peke yake kwa mahangaiko makubwa, kamsomesha kwa tabu kwa pesa za kuokoteza kwenye vigenge, upatu na misaada ya kaka zake. Lakini ameshangaa sana mtoto alipomaliza chuo na kuanza kupata kipato.

Mtoto ameanza kuzunguka huku na huko akiulizia ukoo wake! Huyo mama anadai amemfuma kijana akiwa anaongea na mtu wa ukoo wa babake ambaye huyo mama anamweleza kama kisirani kabisa hataki asogeze pua karibu na mwanae. Anadai amemtishia mtoto wake kuwa akiendelea kutafuta hicho anachodai ni ukoo wake, eti atamlaani!

Nauliza akina mama, hii ni sahihi? Kwanini hutaki mtoto ajue ukoo wake? Kila binadamu ana haki ya kuijua asili yake, hata kama humpendi huyo babake.

Kama unamchukia kiasi hicho huyo baba mtoto na ukoo wake wote, kwanini ulimpa? Si ungemnyima tu kuepusha shari? Mtoto hajahusika na kosa lako/lenu/la babake, kwanini unamnyima haki? Huoni kuwa huo ni unyanyapaa mtoto ajisikie kama mtu aliyeokotwa tu?
Huyo mama anakosea. Hata yy binafsi atakuwa na ukoo wake
 
Ivi wewe Mtoto azaliwe uletewe umkatae alelewe mwaka mmoja mpk 27 bila msaada wowote na pengine upo kwenye nafasi nzur ya kutoa msaada af hutoi...dah af mi ndo Anko ake na uyo Mtoto aisee utaisoma namba
Sema mpwa wako ndiyo ataisoma namba kwa sababu ndiye anayetafuta baba yake. Na usishangae ukajikuta unaisoma namba wakati mtoto anakutana na baba yake na wanaelewana.

Sisi tulilea mtoto wa aina hiyo. Dada yetu alianza kazi akiwa binti mdogo, enzi hizo post yake aliyoanzia iliitwa "afisa ujamaa na ushirika" ndio kwanza alikuwa amemaliza form four akaajiriwa baada ya kozi ya mwaka mmoja. Mwaka wa pili akaja nyumbani na mimba. Akajifungua mtoto wa kike, baba hajulikani, akiulizwa anajibu hovyo. Mtoto alipofikisha miaka miwili, mamake akapata nafasi ya kujiendeleza akaenda kusoma diploma akatuachia mwanae wazazi wetu wakaendelea kulea. Kule alikoenda akapata mchumba, akaolewa akaanza familia na anayo mpaka leo. Huku nyumbani binti akakua na ikafika muda tukapokea barua ya uchumba. Tukiwa tunaandaa sendoff tukashangaa binti anasema amempata baba yake na anataka aje kwenye sendoff. Dada yetu akawa mkali kama mbogo, hataki kumuona huyo "mhuni". Binti akaweka msimamo anataka baba yake awepo. Tulikuja kugundua mambo mawili yaliyotushangaza: kwanza, kumbe binti alimfahamu baba yake kitambo na walikuwa wakiwasiliana. Pili, na hii ilitushangaza zaidi, kumbe huyo baba yake ni mtu ambaye hata sisi tulikuwa tukimfahamu, mtu mzima mwenye mji wake na watoto wakubwa kama huyo dada yetu aliyezaa naye! Katika mazingira hayo wajomba tulipaswa kumlaumu nani, na kwa faida gani?
 
Back
Top Bottom