Mitoto unaihangaikia peke yako ikifika ukubwani inaenda kutafuta ukoo wao...

Mama anatakiwa ampe mtoto nafasi ya kujua hilo pia. Watoto hupenda kujua ukweli wa hayo madai ya mama kuwa baba alikutelekeza, na wengine
Unafikiri Kama babaako alikukataa ukiwa mdogo ukienda kwake umeshakua mkubwa atakuambia nlikukataa? Au nilikwepa majukumu ya kukutunza? Lazima akubadilishie stori ukimpata babaako umeshakua mkubwa sio tegemezi tena lazima utamuona mwema Sana na atakupokea vzuri kweli kweli

Mamaako hawezi kukupeleka kwa babaako upate kuamua mwenyewe Kama Ni mzuri au mbaya kwasababu ya hasira mtu kashakukatalia mtoto na kukwepa majukumu unampeleka mtoto amjue ili iweje shida hujajiweka kwenye nafasi ya huyo mama
 
Kwa hili mtoto ana ombwe moyoni
Hivyo anatafuta majibu

Heri aambiwe Baba yake alifariki..sema nayo atataka kumjua na kuhakiki kaburi!
 
Hiyo ni nature ya akina mama wengi,hata mimi Maza kuna watu huwa anasema hapendi nihusiane nao, Kwa hiyo ni wewe mwenyewe kujiongeza.
 
Shida ya single mama wakiachana na waume zao hua wanataka ugomvi urithishwe hadi kwa watoto na hua wanataka mtoto asimjue baba kabisa, stupid.
Baba anapokataa mimba/mtoto mama atamlazimisha?.
 
Baba mwema gani unakwepa mwanao hadi mtoto akutafute?.

Kuna ile mtu anaachana na mwanamke ila anawajibika kwa mtoto

Hakuna mwanamke atakataa support ya Baba mtoto wake..HAYUPO..

Ila Baba watoto naona ndio wanaongoza kwa kukataa watoto..

Mama ana machungu
Ila ni heri mtoto aambiwe ukweli akikua
Akiwa mdogo mama naona anakwepa kumuonyesha mwanae kuwa amekataliwa..si kitu kizuri hata kiroho..
 
Kwa akili ya haraka tu nimegundua huyo mama mwenyewe anashida ndio maana kumekuwa na kukosekana kwa ushirikiano wa kutoka upande wa pili.

Wanawake mjifunze sana binafsi nina mtoto yupo standard two namsomesha shule ya kulipia mwanzoni nilikuwa naletewa report za shule matokeo ya mitihani everything lkn saizi sijamuona mtoto since 28 December 2020 wala test na kila kitu nimelipa mpaka transpo je wapi nimekosea?

Je nikiamua kususa nikae pembeni itakuwaje ?
 
Tatizo wazazi wa siku hizi wanafikiri kumsomesha mtoto na kumpa mahitaji ya msingi ni hisani,au deni kwamba mtoto akikua lazima alipe fadhila,la hasha,sasa mtoto umemzaa mwenyewe!ulitaka asomeshwe na nani!?
Hilo ni jukumu la mzazi,baada ya kujitegemea mtoto akigoma kutoa msaada kwa wazazi alaumiwe kwa kosa Hilo lakini sio kwa kumsimanga kwamba hana shukrani hataki kulipa walichompa wazazi.
Mimi watoto wangu nawapa huduma Bora sio kama hisani au deni kwmaba nawakopesha,ndio jukumu langu,
Mimacho wapa nataka kiwasaidie wao na uzao wao(ambao ni wangu vile vile),
Ili nitakapo kuwa nimelala milele,najua vitukuu vyangu na kizazi mpaka Cha 4,wataishi vzr
 
Wapo wamama wanaokimbia na watoto kwa kuwa wamekorofishana na baba watoto. Wanadai wanao uwezo wa kutunza watoto peke yao, hakuna sababu ya kuhangaika na "vimeo".
 
Ndio maana nimeshauri wamama wasisubiri hadi mtoto akue aende kwa baba kivyake. Wamwambie tangu mapema kuwa babako ni fulani yuko mahali fulani, akitaka kumwambia sababu ya kutengana ni juu yake, lakini mtoto amjue huyo baba. Uzuri au ubaya wake aujue mapema tu, usisubiri akue. Na huwezi kumzuia kutafuta upande wa pili wa story yako, ni haki yake. Bora ajue mapema, aulize maswali yake yote ajibiwe, apate amani ya nafsi yake.
Kumbuka kadri unavyojitahidi kumnyima mtoto taarifa ndivyo naye anavyozidisha mashaka na kukosa amani.
 
Jinsia zote mbili kuna wema na wabaya.
Wapo wamama viburi. Nina pesa naweza kulea peke yangu. Mama anamuuliza mtoto "unamtafuta baba wa kazi gani, kwani umepungukiwa nini hapa kwangu, mbona una maisha mazuri kuliko hao wenye baba!" Lakini hapo hapo mtoto anamuona mamake anavyojirusha na wanaume wengine, baadae akipata akili anawaza au anagundua kuwa hata hawa wababa ninaowaonaga hapa nyumbani wana familia zao na watoto kama mimi wanaoulizia baba zao! Akipata wasaa wa peke yake anafanya utafiti wake, na akipata majibu ni ya kwake hata kama mama hatayapenda! Hebu jitafakarini wamama.
 
Wanaweza kuwepo ila ni wachache sn

Mwanamke atake kulea mwenyewe?!!asema tu kakataliwa hana option
 
Hawezi kumuonyesha mtoto kwa baba yake kwasababu ya chuki na hasira kulea mtoto peke yako sio kazi rahisi lakini kwa nnavyokuona huwezi kukubali mawazo tofauti umeshaset your mind kwamba huyo mama ndo mbaya baba Ni mzuri na yeye kukaa mbali na mtoto Ni kosa la mama mtoto amtafute tu baba yake hapo huwezi kumzuia Ila I feel so bad kwa huyo mama namuonea huruma Sana maumivu yake nayaelewa
 
Wala sijasema baba ndio mzuri. Kama kweli baba alitelekeza mtoto, hiyo ni mbaya. Lakini pia mama kumnyima mtoto haki ya kumjua baba yake ni mbaya pia. Two wrongs do not make a right.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787] hii nzuri
 
Ukiwalea watoto kwa kuwalisha sumu za kuchukia mmoja w wazazi wao na ukoo ndo umejipalia makaa ya kukimbiwa wakishakua watu wazima
 
Afrika mambo ya kufuatiliana ni yakishamba sana.

Kawaida mtoto akishafikishafika umri wa kujitegemea mzazi unatakiwa kuacha kumshikia mawazo.

Ni jukumu la mzazi kumlea mtoto. Akishakuwa huna mamlaka ya kumshikia mawazo.
 
[emoji38][emoji38]
 
Ukweli huru ni kuwa mtoto ni wa baba siku zote_wapo wamama wengi wenye uwezo wa kipesa na wengine wasio na chochote kile zaidi ya KIBURI na UJINGA ambao walijiaminisha kuwa 'wameweza kulea watoto wao wenyewe' bila ya msaada wowote ule toka kwa wababa husika na mwishowe WATOTO HAO HAO WAKAWAITA MAMA ZAO WACHAWI[emoji41]....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…