Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa Watanzania

Oman Hyundai na KIA zimejazana kama uchafu ila huku Bongo ukiwa nazo unaonekana unatembea na jipu na muda wowote litatumbuka.
 
Kuna vitu vinatuharibu sana bongo na mojawapo ni:
1. Umasikini....tunataka gari za kimasikini za kubana matumizi.
Utasiki achana na suzuki au mitsubish spea zake ni ghali na badala yake nunua noah sr40.

...hebu tuangalie utofauti na ughali wa spea.
Mfano ukinunua shock absorber moja ya mitsubishi ni 180k na inadumu zaidi ya miaka 3, noah shock absorber yake ni 60k lakini haimalizi mwaka mmoja.
Hapa ipi ni ghali?
Tatizo tunafuata mkumbo.

2. Kupokea maneno ya uzushi kutoka tena vijiweni au hata mtu ambaye hajawahi kuendesha gari

3. Mafundi uchwara wanaposhindwa kurekebisha tatizo walisingizia gari
 
Poti agiza kinywaji nakuja kulipa
 
Chief hata ya 2010 ni moto sana
Sawa iko vizuri ila huwezi fananisha na toleo lake la tatu, kwanini nimemwambia achukue io?. Ni kwasababu kasema anataka achukue ya 2012 ambayo ni bora akaongeza pesa kidogo adake chuma kizuri zaidi.

Angekua anataka achukue za 2010 kushuka chini sawa hata nisingemshauri kitu, ila mtu anaechukua Outlander ya 2011 au 2012 bora aachane nazo achukue za kuanzia 2013 sio kwamba zina matatizo hapana ila zina tumia teknolojia iliyoboreshwa zaidi kuliko matoleo ya nyuma huko.

Sent from my CPH1989 using JamiiForums mobile app
 
Ya 2013 nzuri pia japo Sokoni pia bei yake itakua juu zaidi hizo new models
 
Hapo jamaa wamethibitisha kuwa kweli gari ni porsche. 🤣 Yani expensive haswa kuanzia material.

Hizo parts za miguu ukiziyeyusha unapata seti nzima ya masufuria na sinia la kulia pilau.
HahaHa ukiyeyusha vile vispoku vya haria pale juu nina uhakika unapata kakijiko ka kulia cha kula na kasufuria ka kuchemshia chai kikombe kimoja.
 
Hapo jamaa wamethibitisha kuwa kweli gari ni porsche. 🤣 Yani expensive haswa kuanzia material.

Hizo parts za miguu ukiziyeyusha unapata seti nzima ya masufuria na sinia la kulia pilau.
Na vijiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…