Gari nzuri zisizoongelewa sana na wabongo
Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana, ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa watanzania.
Gari hizi zinavitu vingi sana ambapo gari nyingine kama Toyota huwezi pata hasa ukilinganisha bei yake.
Mitsubishi outlander 2006 - 2015
1.Ni gari inakuja na charging system ya laptop, yaani unaweza kuchomeka switch sockate na ukaweka charger yako vizuri... Kwa kifupi
Gari hili linabadili umeme wa dc kwenda ac.
Kwa watu wanaopenda kutumia laptop wakiwa safari hii gari unaweza kutumia laptop toka Dar mpaka Mwanza, bila kuizima unafanya kazi tu au unaangalia series.
2.Gari hii inakuja na kifridge kidogo kuweka vivywaji uwapo safarini.
3.Gari hii ina option ya 4WD
4.Gari hii inakuambia muda wa kupumzika ukichoka safarini.
5. Gari hii inakuja na mziki mziti yaani subwoofer isiyojaza buti.
6.Gari inakuja na seat 7.
7.Gari hii ina option ya manual na automatic.
8. GARI hii ina gear 6, inaifanya itumie mafuta kidogo.
Hii gari bei yake ipo chini ya kina harrier, kulger na Vanguard. Kitu ambacho hivi vitu vyote vingekuwa kwenye hizo gari bei zake zisinge shikika.