Mitsubishi outlander, Subaru Forester au Harrier nichukue lipi?

Mitsubishi outlander, Subaru Forester au Harrier nichukue lipi?

Tafuta barabara iliyo bize sana kupita magari, uwe na notebook andika majina ya hayo magari kisha anza kunote idadi kila aina ya gari inayopita kwenye orodha uliyonayo. Jioni rudi nyumbani hesabu gari gani Ina idadi kubwa, kisha chukua hiyo
I don't think this is a good advice
 
Kwenye performance kwa mazingira yetu bado VVTI ni best option.

Bei tofauti kidogo? Hapana, tofauti ni kubwa
Outlander ya 2005 au 2006 Ina range kwenye mil 21 mpaka 23
Harrier ya 2005 au 2006 Ina range kwenye mil 35 mpaka 38
Model za mbele ndio usilinganishe kabisa maana outlander imeachwa mbali kwa bei

Wala si suala la consumer behavior wala pia si suala la wabongo kuzoea Toyota. Ingekuwa hivyo basi Touareg au tiguan ingekua inauzwa bei chini ya suv za toyota. Au Audi Q series zingekua chini ya toyota
Ni kweli kabisa. Outlander Cross SUV inauzwa bei sawa na IST wakati harrier tako la nyani ikiwa pimped unazungumzia 40m+ bei mara mbili ya Outlander
 
Wakuu ninunue gari ipi kati ya hizo budget 34m
Angalia mazingira yako ya maisha yakuongoze, kama location, kama mtu wa safari, rough roads, umri, starehe n.k 1. Kama ni mtu mzima sana na hauna mambo mengi nenda na harrier.
Hii haitakuwa na usumbufu wa mara kwa mara kukulaza porini, kwenda garage, japo wengi wanaiita kubwa jinga nadhani utakuwa umeelewa kwanini imeitwa hivyo.

2. Kama ni mtu wa makamo na hauna mambo mengi pia, unapenda adventure, nenda na outlander.
Uzuri wa hii inakuoffer 4wd ambayo inakuwa na diff lock kukufanya usijutie safari za njia korofi na ukaenjoy pia, nadhani watu wa magari watanielewa kuna muda mtu unaenjoy kunasa kwenye tope na kutumia features zako ili utoke

3. Ikiwa ujana bado unakudai ruka na forester. Hii inakubali chochote utakachopimp, na utazidisha sifa ya kupendwa na wadada kwani wanaifaham sana kuliko outlender, harrier wanajua ni za watu wazima na wazee.

Hivyo chaguo ni lako, mazingira yako ya kuishi yakuongoze.
 
Kluger/Harrier huwezi ku-compare na Outlander interms of perfomance
Mitsubishi reliability yake haiizidi Subaru wala Toyota, tena hapo kwa magari mengi sio hizi aina tatu anazouliza. Ingekuwepo Honda nayo ingeizidi Mitsubishi kwa reliability, au unahisi kwanini hiyo kampuni imepoteza market share duniani.

1. Harrier
2. Subaru
 
Jamaa itakua anaichukulia poa outlander
Mkuu sijui watu wanashida gani, tukubaliane kutokukubaliana kwamba kila mtu anamapenzi yake, watu wanaamini kwamba kuna gari ambazo haziharibiki kirahisi lakini nyingine zinaharibika kilahisi. Bei ya Outlander iko chini si kwa sababu ni mbovu ila uhitaji wake huku kwetu bado uko chini. Wabongo tunanunua magari kwa kuangalia upatikanai wa spea, kunywa mafuta na mafundi ila mimi naamini katika matunzo.

Mimi wakati nanunua Mazda Demio mwaka 2016 (Tsh. 9.5 Mil mpaka kuiweka barabaran)watu walinishangaa, kwamba nimenunua gari ambayo nitapata shida kuiuza, sio maarufu huku bongo, mara gari sio imara, vipuri vya shida. Mimi baada ya kusikia hivyo nikasema gari hii nitaitunza, nilifanya service kwa wakati, matengenezo mengine ya kawaida ya kubailisha vipuli, na kweli mpaka leo hii, gari iko vizuri sana inazidi confotability na apperance magari yetu mengi pendwa ya Toyota ambayo yamenunuliwa baada yangu mimi. Gari ni Matunzo.
Outlander ndio gari ninayotaka sasa hivi, gari zisizopendwa lakini nazitunza vizuri.
 
chukua harier mkuu hii gari utaimudu vizuri ni moja ya gari safi sana fuel economy nzuri kama mapesa yapo kama lugumi chukua outlander vinginevyo itakuwa makumbusho kama gari za nyerere
 
Huu uzi unanichanganya
Nilitaka kuagiza outlander kutokana muonekano wake, idadi ya seat baada ya kusoma uzi huu nimevurugwa
 
Huu uzi unanichanganya
Nilitaka kuagiza outlander kutokana muonekano wake, idadi ya seat baada ya kusoma uzi huu nimevurugwa
Chukua hio outlander...
Hio gari inaizidi perfomance harrier kwenye barabara korofi..

Watanzania ndio zao.. wakikaririshwa gari moja basi ni nchi nzima.. kila kona harrier , kila kona ist..
 

Huyu jamaa yeye ni mfuasi mkubwa wa German cars, hawezi kutumika kama reference ya choices kwenye gari za kijapani. Mimi nina harrier tako la nyani mwaka wa pili huu ninajua faida za hii gari.

NB: kila mtu ana zile gari ambazo hazimfutii machoni kwake na hana sababu zinazomfanya aichukie hio gari, ila anaichukia tu
 
Huyo ni kwa sababu hana hela, alipata ya kununulia ila ya kuhudumia hana au anayo kwa ajili ya gari ndogo. Kifupi huyo ndugu yako aliruka stage.

Ukiweza kuhudumia Harrier(tako la nyani) hushindwi Outlander au Forester. Hizo ni gari za level moja, calibre moja.
Mzee unahudumia gari amekuwa mke?. Naomba ufafanuzi tafadhari.
 
Back
Top Bottom