Miujiza Nepal; Sanamu ya Budha yabaki imesimama imara katikati ya Mafuriko makubwa!

Miujiza Nepal; Sanamu ya Budha yabaki imesimama imara katikati ya Mafuriko makubwa!

Kitu kama sanamu kinachoaminika na watu kinajengwa kwa msingi imara kama mwamba.

Wangejenga kwa foundation ya kawaida ingeshasombwa na maji kitambo sana.
Kwa sababu huamini tu Budha ndio maana unatafuta sababu za kukataa miujiza yake.
 
Ni tukio liliowashangaza wengi duniani Sanamu ya Budha kubaki imesimama imara wima katikati ya Mafuriko View attachment 3659816
ungejiliza kuwa hiyo sanamu imejengwa kwa uimara gani (si unajua ni kitu wanacho kiamini sana)
kuna hata ile gorofa moja imebaki na watu wake wote waliokuwa wanaishi hapo kuokolewa. Lakini utafiti umeonesha nguzo zake zimeenda chini takriban meta tano.
Pamoj na kwamba silihusishi mafuriko na imani nyingine ILA najua kwa miezi kadhaa sasa Nepal wamekuwa na wimbi la kuharibu misikiti na Kitabu kitakatifu...
 
Kama unaamini huu ni muujiza bas unaweza kupigwa kirahisi sana na mafuta ya upako, na kufufua watu waliopangwa
 
Kuna watu duniani kweli wana akili ndogo sana. Unatengeneza cement na udongo unaanza kuabudu. Badala ya kumwabudu muumba.
 
Shetani nae anafanya miujiza!
Yani sikutegemea kabisa jibu kama hili kiukweli na kwa jina la ID yako, daah nimesikitika mno nyie mnaojikuta ndiyo wakristo wasafi pepo ya kwenu mnafanya vitu vya kipumbavu sana kuliko hata Abbot wa monasteri. Ndiyo maana hata katika mafundisho ya Yesu alisema wazi yule anajiona amesimama na aangalie asianguke.
 
Nazungumzia kuumba sio kuunda. Kuumba na kuunda ni vitu viwili tofauti. Mwenye uwezo wa kuumba ni MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi pekee.
Hilo naelewa sanaa tena sanaaaa acha kudharau Imani za wengine wewe naamini hata uhalisia wa biblia huujui naamini 100% ukiona mtu anadharau Imani ya mwingine ujue huyo bado sana kwenye scriptures za kiimani.
Ni hivi sasa “Si lazima uamini kile ambacho mwingine anaamini, lakini unapaswa kuwa na heshima ya kutambua kwamba imani yake ni takatifu kwake. Kumdhihaki mtu kwa sababu ya imani yake hakukufanyi uwe na hekima zaidi; kunaonyesha tu jinsi ulivyo mdogo katika kuheshimu usichokielewa.”
 
Back
Top Bottom