Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Katika kipindi hichi cha mwezi wa sita hadi mwishoni mwa mwaka tumeshuhudia kabisa idadi ya watalii ilivo kubwa na inazidi ikiongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda katika miji hii miwili ya kitalii.
Ni aibu kwa mji wa kitalii kama Arusha na Moshi kuwa na aina ya masoko na vituo vya mabasi makubwa ya kwenda mikoani kama vilivyopo.
Masoko pamoja na vituo vya Mabasi makubwa ni vile vile vya tangu tupate uhuru, hamna ujenzi wowote uliofanyika kuendana na Ongezeka la idadi ya watu pamoja na ukuaji wa miji na teknolojia.
Rushwa na siasa imekuwa ikitawala haswa katika miji hii kuhusiana na wapi pajengwe kituo cha mabasi makubwa,swala hilo ndio haswa limekuwa likichelewesha ujenzi wa miundombinu muhimu ya masoko ya kisasa pamoja na stand ya mabasi makubwa ya mikoani.
Kukosekana au kucheleweshwa kwa ujenzi wa miundombinu muhimu kama hiyo inasababisha pia ucheleweshaji kwenye uwekezaji katika mambo mbalimbali ikiwemo viwanda, Sekta za utalii nk.
Ni wakati sasa wa viongozi wa miji hii miwili mikubwa kuweka siasa pembeni na kufanya uboreshaji wa miundombinu