DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Juzi nilikuwa Morogoro kwenye Mtaa wa Mganza, Kata ya Mindu, nilikutana na moja ya changamoto ambayo ukweli inawaumiza Wakazi wengi wa hapo.
Nilichokiona ni kuwa Wananchi wengi wa hapo wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya Barabara hali ambayo imesababisha athari kadhaa hasa kwa Wanafunzi kutumbukia kwenye makorongo wakati wa kuvuka.
Jambo lingine ni kuwa kuna usumbufu wa kubeba Wagonjwa na Wajawazito hususani katika kipindi hichi cha mvua.
Baadhi ya Wananchi kadhaa niliozungumza nao wa eneo hilo wamesema licha ya kuwepo kwa changamoto ya Barabara bado wanakabiliwa na changamoto ya nishati ya umeme, huduma hiyo haipo Wanadai wameshafika kwenye mamlaka zinazohusika na umeme mara kadhaa lakini hawajapata msaada.