Azniv Protingas
JF-Expert Member
- Oct 29, 2020
- 352
- 585
Soko la buguruni ni moja ya soko kubwa na maarufu ndani ya jiji la Dar es salaam ambalo linahudumia watu wengi hasa kwa wafanyabiashara wa matunda. Lakini cha kusikitisha miundombinu ya soko hilo ni kero kwa wafanyabiashara na wanunuzi ambao hufika hapo kwa ajili ya ununuzi wa mahitaji yao ya kila siku.
Licha ya kukarabatiwa kwa soko, lakini njia ambayo ndio inatumika kwa ajili ya kushushia bidhaa si rafiki kwa watumiaji hasa kipindi cha mvua. Mamlaka husika sijui ziko wapi kwani kila siku kodi za vizimba zinakusanywa, usafi pamoja na ulinzi lakini kwenye suala la usafi bado si salama kwa wafanyabiashara na wakaazi ambao wanaokaa karibu na soko. Taka zinazotoka kwenye soko zinakaa kwa muda mrefu hadi zinatoa harufu, na zinawekwa kwenye njia ambayo ni kwa ajili ya kupita watu.
Njia inashindwa kupitika hasa baada ya mvua kunyesha hasa kwa kukosa njia za kupitisha maji na barabara mbovu ambazo hutuamisha maji na kusababisha tope kwenye njia.
Naomba taarifa hii iwafikie wahusika ili waweze kulishughulikia suala hili na waweze kulifanyia kazi kwani ni adha kwa wajasiriamali.
Pia soma:KERO - Miundombinu ya soko la Buguruni ni hatari kwa afya ya watumiaji