Miyorgirl: Mwanaume maskini ujue hata akili hana siwezi kuwa naye

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Muigizaji na mwanamitindo nchini, Miyorgirl, amezua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kauli zake tata alizozitoa hivi karibuni wakati wa mahojiano na wanahabari jijini Dar es Salaam, ambapo ameweka wazi vigezo vyake vya mahusiano na msimamo wake wa kutotaka ndoa kabisa.

Akiulizwa na mwandishi wa habari kuhusu aina ya mwanaume ambaye hawezi kabisa kuwa naye kwenye mahusiano ya kimapenzi, Miyorgirl alieleza bila kuficha hisia zake kuwa hawezi kuwa na mwanaume asiye na uwezo wa kifedha.

"Siwezi Kuwa na mwanaume masikini Kwa sababu mwanaume akishakosa pesa ujue hata Akili Hana," alieleza mwanamitindo huyo.

Wakati mwandishi huyo akijaribu kuhoji zaidi kuhusu masuala ya mahari na idadi ya ng'ombe inayoweza kumshawishi kuolewa, Miyorgirl alikataa kwa ukali kujibu suala hilo na kusisitiza kuwa hana mpango wa kuingia kwenye ndoa.

"Sina mpango wa kuolewa, kwenye maisha yangu kitu kinacho itwa kuolewa hakipo, hilo swali ondoa kwenye mahojiano yangu," alisema kwa msisitizo.

Kauli hizo zimeibua maoni mseto kutoka kwa mashabiki na wafuatiliaji wa sekta ya burudani, ambapo wengi wamekosoa mtazamo wake kuhusu wanaume na taasisi ya ndoa, huku wachache wakimtetea kwa kuheshimu msimamo na hisia zake binafsi.
1790318388823.png
 
Ni mwigizaji wa wapi mbona hajulikani au ndio unamtambulisha?
 
View attachment 3677394
Ai🙌🔨
 
Back
Top Bottom