Mizengo Pinda declares assets in anti-graft drive

Mizengo Pinda declares assets in anti-graft drive

Sasa kama sheria ipo lakini ni non binding kuna umuhimu gani wa kuwa na hiyo sheria? Ni kama vile mtu aseme kuna sheria ya "usiibe" lakini hainilazimishi kutoiba. Yaani hiyo sheria ilitungwa kufurahisha tu baraza?

- Mkuu Jasusi, hapa tupo pamoja sana ndio maana jana niliuliza hivi nini faida ya PM kutangaza mali zake, wakati kwanza hakuna wa kutuhakikishia with facts kwamba anayosema ni kweli,

- Halafu wengine hawana sababu ya kutangaza hasa wale wote walio chini yake, ndio nikasema kwamba hakukuwa na sababu ya yeye kusema mali zake, kwa sababu haina impact yoyote kwa masilahi ya taifa!

- In the future, Usalama Wa Taifa ndio wapewe jukumu la kutangaza mali za viongozi wetu wakuu wa taifa, otherwise tutaendelea kudanganyana tu kama alivyofanya Pinda!

Respect.


FMEs!
 
Tunamjua Makinda, alichokifanya Ruvuma wakati akiwa mkuu wa mkoa tunakijua sana na hatujakisahau!!
 
zaidi ya kuwa sheria ina mapungufu nk, kuna kitu kingine ambacho kina mapungufu, mfano ntu akijenga nyumba akampa mwanae/bintiye hiyo mali inakuwa kwenye list ya nani. Pinda anaweza kuwa sio fisadi lakini anatakiwa ataje mali za wanao muhusu ambazo zimepatikana kwa mgongo wake.
 
Huo ndio ukweli?

Wewe unaonaje? 70% ...hata pinda anajua hili ndio maana anatudanganya kweupe pee.Pinda ni muongo,tatizo watanzania ni wajinga tena sana. sasa katangaza ndio wenzake wanambeza,ina maana kumbe kutangaza sio lazima. mimi nina uhakika Pinda ni mnafiki ndio maana alijifanya analia .mwanaume halii huyu jamaa style yake ni ya kunawa mikono ma kukaa pembeni. HAFAI KABISA
 
Mimi namwelewa kabisa Makinda.Anasema hata mafisadi kina Mkapa walitangaza mali zao walivyoingia urais lakini hawakutangaza walipotoka, wala hakuna sheria inayowalazimu kutangaza, so what is the point?
 
Baada ya kusoma sheria inayoitwa Public Leadership Code of Ethics Act ya mwaka 1995, nimeona mapungufu kadhaa katika lugha iliyotumiwa kiasi kuwa inaacha mianya mingi sana kwa viongozi kuficha mali zao. Ninadhani kuwa kwa vile wakati sheria hii inatungwa (1995), tayari rushwa ilisishashamiri na kuonekana kama sehemu mojawapo ya fringe benfits za kazi, waandikaji wa sheria ile walitafuta namna ya kuficha mali zipatikanazo kwa njia ya rushwa na hivyo kuifanya sheria yote iwe diluted.

Pamoja na mapungufu ya sheria ile, ninadhani huyu mama Makinda kakosea katika kudai kuwa kutangaza mali ni hiari, sheria ile haisema kuwa ni hiari kwa kiongozi kutaja mali zake bali inasema ni lazima. Inawezekana kama mama makina alikuwa anatumia kinga nyingine ya kikatiba au sherioa nyingine yenye nguvu kuliko hii kulingana na lugha iliyotumika katika kifungu cvha 9(1) cha sheria ile. Kama kweli kuna sheria nyingine inayo-overwrite sheria hii, then hatuna haja ya kuwa na sheria hii ya mwenendo wa viongozi.


(1) Sheria hii ya mwenendo wa viongozi inasema kuwa ni lazima kiongozi ataje mali alizo nazo, haisema kuwa ni hiari kufanya hivyo. Kifungu cha 9(1) cha sheria ile kinamtaka kila kiongozi ataje mali zake, za mme au mkewe na watoto wao wadogo (minors) katika siku 30 tangu kuanza uongozi, kila mwisho wa mwaka, na siku anamaliza madaraka yake. Ingawa kifungu cha 9(2) ni ngao isiyokuwa na manufaa kwa taifa ila kiliwekwa pale kuwalinda viongozi, bado kifungu hicho hakizuii kifungu cha 9(1) kufuatwa kwa vile kinasema kuwa mali ya kiongozi, ya mkewe/mmewe na watoto wao wadogo(minors). Kwa hiyo hata kama mali hiyo siyo mali ya pamoja au haimilikiwi kwa pamoja baina ya kiongozi na partner wake wa ndoa (mkewe au mmewe) ni lazima itajwe kwenye 9(1) kama ni mali ya partner wa ndoa.


PART III
CODE OF ETHICS APPLICABLE To ALL PUBLIC LEADERS
8. The provisions of this Part shall constitute part of the Code public leaders for the provisions of the Constitution, a breach of which results in the Vacation of the office of the public leader concerned.
9.- (l) Every public leader shall, except where the Constitution or any other written law provides otherwise;
(a) within three months after the commencement of this Act, or liabilities
(b) within thirty days after taking office;
(c) at the end of each year, and
(d) at the end of his term of office,
submit to the Commissioner a written declaration, in prescribed form'' of all property or assets owned by, or liabilities owed to', him, his spouse or unmarried minor children, subject to subsection (2).
(2) A public leader shall not be required to declare as his property, and property shall not be deemed to be declarable by a public leader if-
(a) it is not matrimonial property;
(b) it is not jointly owned with the public leader's spouse or spouses;
(c) there is no allegation that a public leader appears to have suddenly and inexplicable come into possession of extraordinary riches in relation to his observable sources of income.
(3) Any property or asset acquired by a public leader after the initial declaration required by paragraph (a) or (b) of subsection (1) and which is not attributable to income, gift, or loan approved in the Code shall be deemed to have been acquired in breach of the Code unless the contrary is proved.
10.- (1) Assets and interests for private use of public leaders and their families, and assets that are not of a commercial character shall not normally be subject to public declaration divestment.
(2) Non-declarable assets referred to in subsection (1) shall include:-
(a) residences, recreational, property and farms used or intended for use by public leaders or their families;
(b) household goods and personal effects;
(c) works of art, antiques and collectibles;
(d) ''motor vehicles and other personal means of transportation for private use; ,
(e) gains or advantage derived through labour on land owned or occupied by a public leader;
(f) registered retirement savings plans that are not self-administered, annuities and life insurance policies;
(g) money saved by a previous employer, client or partnership; and
(h) person loans receivable from the members of the public leader's immediate family and small personal loans receivable from other persons where the public leader has loaned the money receivable.

11.- (1) A public leader shall make it declaration of assets that are not non-declarable assets in order for him to be able to deal with them without giving rise to a conflict of interest.
(2) Declarable assets shall included
(a) cash and deposits in a bank or other financial institution;'';
(b) Treasury Bills and other similar investments in securities of fixed value issued or guaranteed by the Government or agencies of the Government;
(c) interest on money deposited in a bank, building society or other financial institution;
(d) dividends or other profits from stocks or shares held by a public leader in any company or other body corporate,,
(e) interest in business that do not contract with the Government, and do not own or control publicly traded securities, other than incidentally, and whose stocks and shares are not traded publicly:
(f) farms under commercial operation;
(g) real property which is not it non-declarable asset-,
(h) assets that are beneficially owned, which are not non-declarable assets and which are administered at arm s length.
Vile vile Pinda naye kafanya makosa kadhaa katika kutangaza mali zake kulingana na sheria hii ingawa inaweza kuwa inatokana na mapungufu katika lugha iliyotumiwa na sheria hiyo.

(a) Sheria ile inasema kuwa kiongozi hawezi kutangaza nyumba anayotumia kama maskani ya familia yake. Hayo ni mapungufu makubwa katika sheria hiyo kwa vile kiongozi wa nchi anaweza kuwa na nyumba nchi nzima akasema kuwa nyumba hizo huzitumia na familia yake wakati wanapotembelea sehemu hizo za nchi kwa hiyo hana haja ya kuzaitaja. Sheria ingeruhusu nyumba zote zitajwe bila kueleza matumizi yake. Pinda alitaja nyumba zake zote ambapo ni pamoja na nyumba anazosihi wakayi sheria haimhitaji kufanya hivyo.

(2) Sheria ile inasema kuwa kiongozi hahitaji kutaja magari anayotumia na familia yake. Huo pia ni upungufu mkubwa sana katika sheria kwa vile kiongozi anaweza kuwa na magari lukuki akadai kuwa ni kwa amtumiz ya familia wakati siyo kweli. Sheri ingewataka viongozi wataje magari yote hata kama hawatatuambia wanayatumiaje.Pinda kataja kuwa ana gari moja alilopata kwa mkopo wakati sheria haimhitaji kufanya hivyo.
 
Sasa kama sheria ipo lakini ni non binding kuna umuhimu gani wa kuwa na hiyo sheria? Ni kama vile mtu aseme kuna sheria ya "usiibe" lakini hainilazimishi kutoiba. Yaani hiyo sheria ilitungwa kufurahisha tu baraza?

Kama ile sheria yetu ya rushwa......aisee
 
Habari wadau wenzangu……nimekua nikitafakari kwa makini sana mustakabali wa nchi hii, ilipotoka, ilipo na inapoelekea…mchanganyiko na mvurugiko wa mambo ulivyo sasa, bado hatujielewi kabisa..CCM kama chama kimetuangusha kwa kiasi kikubwa sana, however kuna watu ndani ya CCM ambao wanaweza….namuona Prime Minister Pinda kama mtu wa namna hiyo, ingawa kwa kiasi kikubwa anakosa support toka ndani, whether from His Excellency or the Cabinet…..kwa maoni yangu therefore, a man is the right Candidate for CCM in 2015 elections….he is mean, open, simple, humble………….and most important..Nyerererised much enough, both historically and ‘intelligenti-cally’-Tanzania anaijua in and out………he is the right person to save this country…NAWAKILISHA!!

........unataka ufisadi uendelee kulindwa eehh.....au umesahu kauli zake kuhusu skandali za nchi.............
 
tunahitaji kijana ambaye umri wake ni chini ya miaka 45 na zaidi... Mwenye sifa kama za mheshimiwa pinda, anayechanganua maswala kama mheshimiwa zitto, asiyependa rushwa kama mheshimiwa sila, mwenye sera za kidiplomasia kama za mheshimiwa raisi wa jamhuri yetu kikwete, mchapa kazi kama mheshimiwa magufuli, mwenye vision kama ya mwalimu nyerere na charismatic kama raisi obama.

Kazi kweli kweli
wewe na nani (tuna)
 
- Unajua haya matatizo ni makubwa sana tunayoletewa na hii drive by media ya Tanzania, hivi kweli mtumzima na akili timamu unawezaje kukaa chini na Waziri Mkuu, akaongelea mali zake bila ya kumuuliza nia na madhumuni ni nini hasa?

- Pinda ananikumbusha Mwinyi, alipokuwa akibanwa kuhusu uwezo mdogo wa kuongoza siku zote alikua anatishia kujiuzulu, mpaka amemaliza miaka 10, hivi hivi hajajiuzulu wala anything, kumbe ilikuwa ni political style tu ya kumaliza kipindi chake, sasa huyu Pinda naye tunakubali kwamba personally ni mstaarabu na tunakubali kwamba sio mwizi, lakini what is the agenda here? Anataka Ikulu nini?

- Something is not right hapa, Pinda hawezi kuamka na kuanza kusema mali zake bila sababu, something is cooking and what is that? Mama Makinda anahitaji heshima kwa ku-raise the bar kwamba Pinda amesema mali zake so what? Mbona hata kina Sumaye na Mkapa walifanya hivyo na hukukuwa na lolote?

- Hiyo ni challenge nzito sana kwa Pinda, kwamba simama sasa useme sababu ya kutangaza kwako mali, ni aibu kwa Pinda kuanza kubezwa na walio chini yake, ndio maana nilisema what is the good of this Pinda's act? kama wa chini yake hakuwalazimisha kufanya kama yeye?

- I am glad Mama Makinda amerudisha mpira kwake Pinda, sasa ajibu Makinda is just the devil advocate here!



Respect.


FMEs!
 
Wabunge wampinga Pinda

Imeandikwa na Waandishi Wetu;
Tarehe: 16th January 2010


WABUNGE wengi wamepinga mapendekezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kutaka kuwepo ukomo wa ubunge.

Hata hivyo baadhi yao wanaunga mkono pendekezo hilo wakisema litaondoa baadhi yao kuhodhi nafasi kama mali binafsi na wengine wakisema demokrasia iachwe mikononi mwa wananchi.

Wasomi na wanasiasa wengine hususan kutoka vyama vya upinzani wamesema tatizo la kuwepo maneno na kutafutana uchawi wakati wa mchakato wa kuwania ubunge, utatuzi wake si ukomo, bali namna wanavyochaguliwa kutokana na baadhi kutoa rushwa.

Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango -Malecela, amepinga pendekezo la Waziri Mkuu kwamba muda wa kuwa Mbunge usizidi miaka 15.

Mbunge huyo amesema, wabunge wasiwekewe kikomo, wananchi ndiyo wanaostahili kuamua na kwamba, umri usiwe kikwazo.

Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya (CCM) na Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Paul Kimiti (CCM) ni miongoni mwa wabunge waliokaa muda mrefu bungeni ambao hivi karibuni walitamka uamuzi wa kung'atuka.

Mbunge wa Mtera, John Malecela na Mbunge wa Njombe Kaskazini, Jackson Makweta (wote wa CCM) pia ni wakongwe ambao hawajaeleza nia ya kuachia nafasi hizo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Wakichangia zaidi maoni, Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes ingawa aliunga mkono kwamba maneno maneno yanaweza kudhibitiwa kwa kuweka ukomo, alisema wananchi pekee ndiyo wanaofahamu muda anaostahili mbunge wao kuwatumikia.

Blandes alisema, "hayo maneno maneno kama kuna ukomo, ni kweli unaweza kuyakomesha. Hata mbunge atafanya kazi kwa amani siyo sasa hivi ambapo wengine wanafanya kazi kwa kuwazia majimbo. Lakini wananchi ndiyo wenye ‘speed governor' (kidhibiti mwendo) cha ubunge."

Mbunge huyo alitofautiana na wa Muhambwe, Kijiko, kuhusu wabunge wa muda mrefu kwa kusema kutokana na uzoefu walio nao, wanasaidia kutoa michango mizuri na ambayo ni chachu kwa wabunge wengine.

Alitoa mfano wa Mbunge wa Njombe Kusini, Anne Makinda, Mzindakaya, Malecela na Kimiti kuwa ni miongoni mwa watu wenye michango endelevu inayotokana na uzoefu wao bungeni.

Mbunge wa Tabora, Siraju Kaboyonga pia alipingana na mapendekezo ya kuweka ukomo kwa malengo ya kumfanya Mbunge asikae muda mrefu na kusema ni chanzo cha kuyapotezea majimbo maendeleo.

Akitolea mfano wa majimbo ya mkoani Tabora aliyodai yamekuwa yakibadilisha wabunge kila kipindi cha uchaguzi isipokuwa Tabora Mjini, Kaboyonga alisema majimbo yasiyobadilisha mara kwa mara wabunge yana maendeleo tofauti na yanayobadilisha.

Mbunge wa Muhambwe, Felix Kijiko (CCM) alikubaliana na Waziri Pinda kwa kusema wabunge wanaokaa muda mrefu wamebaki kufanya kazi kwa mazoea.

Alisema Mbunge aliyepata wadhifa huo tangu miaka ya 1970 hapaswi kuwepo hadi sasa na kwamba hafanani kimtazamo na wabunge wa sasa.

"Wabunge wa miaka ya 1970 walichaguliwa kutokana na uwezo wa kusema sema. Waangalie wabunge wanaosema sema sana majimboni kwao wamefanya nini," alisema Kijiko ambaye ana kipindi kimoja bungeni bila kuwataja wabunge waliokaa muda mrefu bungeni huku akisisitiza, "wewe wachunguze wabunge wanaosema sana, majimboni mwao hakuna wanachofanya."

Mwanataaluma, Profesa Mwesiga Baregu pia aliunga mkono kwamba wananchi waachiwe wachague kiongozi wanayemtaka bila kushawishiwa kwa hongo na kujengewa hofu yoyote.

Alisema iwapo Watanzania watakuwa na uwezo wa kuchagua kiongozi kwa kuzingatia utendaji wa mgombea ni lazima watakuwa wanachagua kiongozi bora kuliko ulivyo mfumo wa sasa hivi.


"Sasa hivi wananchi hawachagui kiongozi bora, wanaweka mbunge ambaye anatumia fedha nyingi kuwahonga na kila baada ya uchaguzi anatumia fedha, katika hali ya namna hiyo hakuna kiongozi bora wa jimbo," alisema Profesa Baregu.

Alisema Waziri Mkuu ahangaike na elimu ya uraia kwa wananchi ili waepuke kurubuniwa na kujengewa hofu, kwamba wakichagua fulani au chama fulani hawawezi kupelekewa maendeleo.

Alisema sasa hivi wananchi wanahongwa na kujengewa hofu hivyo kujikuta wanachagua mbunge chini ya shinikizo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor Kimesera alisema tatizo kwenye ubunge si ukomo, bali tatizo ni namna hata wabunge wabovu wanavyochaguliwa tena kuongoza kwa vile tu wanatoa rushwa.

"Tatizo ni rushwa, hili tukiliondoa Watanzania watapata wabunge bora." Mwenyekiti wa NLD, Dk. Emmanuel Makaidi alidai mapendekezo ya Waziri ni kujisumbua kwa kuwa ndani ya CCM wapo watu walioigeuza siasa kama ajira yao, jambo ambalo ni vigumu kwao kumuunga mkono.
 
nakubaliana na hoja kwamba wananchi waachiwe waamue ni muda gani mbunge anastahili kukaa bungeni si lazima kila kitu kiwe na ukomo.

ukomo tulioweka kwenye urais unachangia kuchochea matumizi mabaya ya madaraka hasa katika kipindi cha pili cha urais kwani huchukuliwa kuwa ni kipindi cha "kufunga mahesabu" baada ya biashara (kipindi cha kwanza). sasa na ubunge ukiwa hvyo si nchi "itafyatuka" kwa ufisadi?

hivyo ukifanya utafiti utaona kuwa hata ukomo wa urais haujatusaidia sana.
 
Hivi bunge bado lipo???????????????????? Jamani nendeni nyumbani mle ugali mkalale
 
ukomo tulioweka kwenye urais unachangia kuchochea matumizi mabaya ya madaraka hasa katika kipindi cha pili cha urais kwani huchukuliwa kuwa ni kipindi cha "kufunga mahesabu" baada ya biashara (kipindi cha kwanza). .

Huo wizi unaofanywa ndani ya awamu ya pili unatokana na viongozi ambao wameingia madarakani kwa uroho wa kutumia madaraka yao kujitajirisha wao, familia zao, jamaa na marafiki wao wa karibu.

Nyerere hakuwa na tamaa na sidhani kama alikurupuka bila kutafakari kwa kina kwamba 1985 ilikuwa ni mwaka wake wa mwisho madarakani. Na hakutumia kipindi chake cha mwisho madarakani kufanya madudu ya kuwafisadi Watanzania kama hao waliomfuatia.
 
Kuna haja ya kumuuliza Mweshimiwa Pinda kama alivyotangaza mali zake alitaka hiweje?

Je alitaka walioko chini yake wote wakae kwenye TV na kutangaza?

Je kama watafanya ukomediani ana means zozote za kuwashughulikia?

Halafu ikumbukwe viongozi wa umma ni wengi mno je wote wakiita waandishi wa habari na kutangaza mali zao watatumia muda gani?

Nafikiri kuna haja kama Mweshimiwa Pinda ameona mapungufu katika ujazaji wa fomu za viongozi aagize suala hilo lisahihishwe au aagize chunguzi zaidi kuliko kukaa na kutangaza.
 
Huo wizi unaofanywa ndani ya awamu ya pili unatokana na viongozi ambao wameingia madarakani kwa uroho wa kutumia madaraka yao kujitajirisha wao, familia zao, jamaa na marafiki wao wa karibu.

Nyerere hakuwa na tamaa na sidhani kama alikurupuka bila kutafakari kwa kina kwamba 1985 ilikuwa ni mwaka wake wa mwisho madarakani. Na hakutumia kipindi chake cha mwisho madarakani kufanya madudu ya kuwafisadi Watanzania kama hao waliomfuatia.

sawa mkuu, alini kumzungumzia nyerere unazungumzia exceptions. kumbuka ukitunga sheria ya ukomo wa madaraa unaufanya mfumo mahususi wa uongozi ambao utam-regualte kila mtu, na ndio tunasema tusimjadili nyerere, tujadili manufaa ya mfumo na ufanisi wake ndipo tutajua kuwa tunauhitaji ama la. ndio mamana nasema kukitungwa sheria ya ukomo wa vipindi vya ubunge pia, biashara zitafanyika ntingi sana na mahesabu yatafungwa mengi sana kuanzia ikulu hadi majimboni! ndipo ninaposema nchi itafyatuka kwa ufisadi
 
Mimi nakubaliana na Mweshimiwa Pinda hapa, kuwepo na ukomo katika suala zima za kuwa mbunge.

Jamani haiingiii akilini mtu alikuwa mbunge kuanzia mwaka sabini na mpaka sasa miaka alobaini eti bado anagombea ubunge, huyu ni wa kusaidia.

wengi wanaweza kupata siyo kwa sababu wameleta maendeleo hila ni mfumo wetu wa rushwa.

Ikumbukwe ktk nchi ya Tanzania ukweli ni wachache wanaochaguliwa kuwa wabunge hili walete maendeleo au wanapendwa na wananchi.

Wengi wanachaguliwa kwa kununua wapiga kura, hili linajulikana na wapiga kura wengi Tanzania si wasomi hivyo kuna haja ya kuwajibishana kwa kutumia sheria kuliko kusubiri kutumia masanduku ambayo tunajua kuwa ukiwa na pesa hili si tatizo.

Hili wananchi wasaidiwe hatuna budi kuwekeana sheria, halafu sheria pia iende mbali kuhakikisha ahadi anazozitoa mbunge zinawekwa kwa maandishi na zinatekelezwa, vinginevyo Mbunge kama hajafanya hivyo(hajatekeleza ahadi) na hakuna sababu za msingi kuwe na kipengele cha kuweza kushitakiwa kwa udanganyifu/utapeli.
 
jamani sheria ya maadili ya viongozi wa umma hailazimishi mu kutaja hadharani mali zake kama alivyosema makinda bali humlazimisha kutaja kkwenye tume pekee. hivyo pinda ana hiyari ya kutaja kwenye tume na kukaa kimya kama anavyofanya wengine au kuweka hadharani kama mkapa na sumaye walivuopata kufanya. sheria haimzuii. ni sawa na kusema sheria ya ndoa imeruhusu talaka lakini haiwazuii waliotalikiana kupendana tena!

sheria huwa inazuia kitu kibaya na hailazimishi kitu kizuri kisifanywe. ndiyo tabia ya sheria

hivyo mama makinda yuko sahihi kadhalika na pinda naye.

labda sasa ni wakati muafaka wa kufanyia sheria hii marekebisho kama alivyopendekeza kichuguu hapo juu no 20
 
Back
Top Bottom