Mizimu imenichagua kuwa mganga japo nina shahada

Mizimu imenichagua kuwa mganga japo nina shahada

Joined
Jun 1, 2022
Posts
21
Reaction score
27
Mimi ni member humu Ila hii ni ID mpya....

Umri wangu ni miaka 29
Elimu yangu ni Shahada
Sijaoa Sina Mtoto

Tangu nimemaliza chuo miaka 8 iloyopita sikuwahi bahatika kupata ajira, nimetafuta Sana kazi lakini holaaa!

Katika Asili yangu yani Upande wa BABA sijui kizazi Cha ngapi alikuwepo MGANGA, pia katika Upande wa MAMA ulikuwa wa kichifu pia UGANGA upo

HIVYO NIMECHAGULIWA MGANGA na MIZIMU YANGU

Miaka Kama Sita Nyuma nimekuwa na MAONO katika kichwa changu naweza kujua Mengi ya sirini yanayonihusu Na hata ya watu, DAWA na TIBA mbalimbali.

MIZIMU imeniambia kabisa nilizaliwa niwe MGANGA na Pesa yangu nitaipata kwa MIUJIZA ya mikono yangu.

Naskitika Sana kuacha VYETI vyangu
 
Naitamani sana kuijua hiyo taaluma.
Mkuu naomba unipe baadhi ya miti/mizizi pm
 
Achana na mizimu wewe, njoo kwa YESU kuna zaidi ya hivyo.

Pesa, Mali dhahabu ni Mali ya Bwana
Bwana huyo anataka watu wake wawe masikini ili waende mbinguni.

Bwana wenu ana bifu na matajiri, akawaambia ni ngumu tajiri kuingia mbinguni kama ilivyo ngamia kupenya kwenye tundu la sindano🥵🥵🥵
 
Kwamba mko sehemu kama somalia au Afghanistan?

neno survive lina maana nzito sana
Ndo iko hivyo.

Scenario za kukosa pesa ya kula, kodi na bil vinakukaba kwa pamoja ni sehemu tu ya tunachotakiwa kusurvive.

Sisi ambao tuna watoto hali ni mbaya zaidi
 
Pole, kuna watu wengi wanapitia na changamoto hiyo wengine wanafikia hatua mpaka wanaumwa hoi vitandani
 
Mimi ni member humu Ila hii ni ID mpya....

Umri wangu ni miaka 29
Elimu yangu ni Shahada...
Kama unataka kuukataa uganga, Nenda pale buguruni Rozana, Kuna ostadh anaitwa Charles Athumani ndio issue zake hizo akakusomee visomo, Kuna mama alikuwa anasumbua Kama wewe lakin Sasa hivi mzima.
 
Kama unataka kuukataa uganga, Nenda pale buguruni Rozana, Kuna ostadh anaitwa Charles Athumani ndio issue zake hizo akakusomee visomo, Kuna mama alikuwa anasumbua Kama wewe lakin Sasa hivi mzima.
Aliyekwambia MIZIMU unaweza kuikataa Nani?


Utazinguka dunia Hii na hutaeeza kuizuia Mizimu ya UKOO wako labda Kama ni ya jirani yako🤔
 
Back
Top Bottom