Mizimu imenichagua kuwa mganga japo nina shahada

Mizimu imenichagua kuwa mganga japo nina shahada

Kama unataka kuukataa uganga, Nenda pale buguruni Rozana, Kuna ostadh anaitwa Charles Athumani ndio issue zake hizo akakusomee visomo, Kuna mama alikuwa anasumbua Kama wewe lakin Sasa hivi mzima.
Naikataa Vipi talanta niliyopewa na MUNGU wangu....

Hivi KIPAJI adhwimu Kama hiki kwenye familia yenu kipo?
 
Kama unataka kuukataa uganga, Nenda pale buguruni Rozana, Kuna ostadh anaitwa Charles Athumani ndio issue zake hizo akakusomee visomo, Kuna mama alikuwa anasumbua Kama wewe lakin Sasa hivi mzima.
Na kama ni Mkristo unataka kuacha uganga we nenda tu kwa Kuhani Musa Kimara Temboni. Watu wanatolewa uchawi na uganga pale.

Hawachagui Dini

Bwana YESU atukuzwe.
 
Mkuu sikiliza nikuambie..

Usisikilize maneno ya watu humu, uganga ni kipaji kama vipaji vingine kama kuimba, kuigiza au mpira. Hayo maono unayoyaona ndio kipaji chenyewe na ukiyatumia vizuri yanaweza kukufikisha mbali kimaisha kuliko hivyo vyeti. Sasa hivi maisha ni magumu sana mkuu ukipata uchochoro wa kupiga pesa usiulazie damu!

Hao wanaokushauri uache hicho kipaji chako ndio hao hao wanakupita barabarani wakiwa kwenye ma range rover na ma vx wanakutimulia vumbi tu wakati na wao hela wanapata kwa kula rushwa, dhuluma, madawa ya kulevya, nk. Infact wengine hela wamepata kwa waganga.
Mimi ni member humu Ila hii ni ID mpya....

Umri wangu ni miaka 29
Elimu yangu ni Shahada
Sijaoa Sina Mtoto

Tangu nimemaliza chuo miaka 8 iloyopita sikuwahi bahatika kupata ajira, nimetafuta Sana kazi lakini holaaa!

Katika Asili yangu yani Upande wa BABA sijui kizazi Cha ngapi alikuwepo MGANGA, pia katika Upande wa MAMA ulikuwa wa kichifu pia UGANGA upo

HIVYO NIMECHAGULIWA MGANGA na MIZIMU YANGU

Miaka Kama Sita Nyuma nimekuwa na MAONO katika kichwa changu naweza kujua Mengi ya sirini yanayonihusu Na hata ya watu, DAWA na TIBA mbalimbali.

MIZIMU imeniambia kabisa nilizaliwa niwe MGANGA na Pesa yangu nitaipata kwa MIUJIZA ya mikono yangu.

Naskitika Sana kuacha VYETI vyangu
 
Na kama ni Mkristo unataka kuacha uganga we nenda tu kwa Kuhani Musa Kimara Temboni. Watu wanatolewa uchawi na uganga pale.

Hawachagui Dini

Bwana YESU atukuzwe.
Kwani nimeomba kutolewa UGANGA?

La hasha... Hi kitu ni TALANTA yangu siwezi kuimbia
 
Kwenye mabango uandike "KUTANA NA MGANGA MWENYE SHAHADA" Tutakuja na mashida zetu
 
Nimecheka kwa sauti
Ungekuwa unajua kumakinika ungerudia kusoma..... Nipoteze ada miaka nane ya Kuwa jobless au ukiwa jobless unalipia ada? Maono haya yamekuwa yakija nikiwa nishamaliza skul!



Jipange ukosoe Tena!
 
Jamaa nije basi unifanyie dawa nipate kazi za sensa, za tamisemi
 
Mganga anakupa utajiri lakini Katu hawezi uchukua utajiri huo au kumpa ndugu sababu anajua madhara ya utajiri akupao maana at the end ni lzm uliwe kichwa.
So mganga anaogopa kuliwa kichwa,so yeye ugeuka Dalali tu.
Huwezi mpa sumu mtoto wako.
 
Uganga unalipa wahi faster njaa kwako ni mwiko, utazikimbia kuku.
 
Back
Top Bottom