Mizimu inapata wapi nguvu za kuleta mvua?

Mizimu inapata wapi nguvu za kuleta mvua?

Halafu mtu akifa anageuka kuwa mzimu, kesho mnaenda kumuomba alete mvua, huu upuuzi tumeupata wapi? Mfu anapata wapi Nguvu za kuleta mvua?
Inategemea na aina ya kifo cha mtu, sio kila anae kufa anakuwa mzimu ( ancestor spirit). Mizimu kuleta mvua yes, ni roho zile zina access spiritual portal ambazo kama zipo chini ya principalities wa eneo ilo ambao ni side yao.
 
Kumbe unajua inatoa adhabu pia, basi elewa inaleta mvua, baraka na neema sio kwa waafrica tu hata races nyingine hufanya hivi..
Mizimu haina uwezo wa kuadhibu mtu
 
YANI MWAFRIKA AKIPATA ELIMU ANAKUWA KIUMBE HATARI SANA NIMEAMINI
True kabisa

Juzi kuna mzee mmoja nilikua najadiriana nae Jambo, akaniambia tatizo vijana wa siku wanatanguliza sana usomi wao mbele, shida ndio inaanzia hapo, sikutaka kumfukua sana alikua anamaanisha nini ila nmeanza kumwelewa

Mfano juzi wahadhiri wa Chuo kikuu UDSM wanataka kufanya tafiti km uchawi upo au haupo, inaingia akilini kweli? Yaan umesoooma sasa umefika hatua ya kuanza kupingapinga kila kitu unachokiona unapinga tu, ila ukipigwa tukio unakimbilia kwa Mwamposa kukanyaga Mafura

Kuna watu ni sheeebzi type kabisa
 
ajabu zaidi mvua nayo inayokuja[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Nakumbuka kijijini kwetu Massanza Kona, zamani ilikuwa wilayani Magu mwaka 1984, kulikuwa na njaa kali, tulitambika na kuiita mizimu itusaidie kwa nguvu zote, hatukupata msaada wowote, hadi tilipoletewa msaada wa mahindi ya Melika ndio ikawa nafuu yetu
 
Back
Top Bottom