Shangaeni kwanza hizo dini zenu, Hao Miungu wenu mnaowaomba kwa majina ya vificho ambayo ni aina ya mizimu hiyo hiyo mnayoipinga.
Yesu kwa lugha ya kificho ni Zues/Azazel, ambaye ni aina ya mzimu wa wamisri wa kale, na huu mzimu ulikuja kubadirishiwa jina miaka ya 300 A.D na hao hao watu weupe.
bila kusahau hayo majina ya Allah, Yehovah, elishadai, Elohim hawa nao ni wale wale mizimu kama mizimu wengine.
mkae mkijua mtu akifariki hawi mzimu na hatowai kuja kuwa mzimu, bali imani ya kumuomba mtu aliyekufa ilikuja baada ya kuona matendo ya mtu huyo akiwa hai, hivyo hata akifa baadhi ya watu waliendelea kuamin mtu huyo ataweza kuwasikia walio hai kwa kumuomba awaunganishe na Nguvu za Miungu awasaidie kupeleka maombi hapa pia utaona ibada hizi za umizimu zipo hata kwa jamii za imani za ukristo(katoric mzimu wa bikra maria na watakatifu wengine).
Ni ngumu kutenganisha umizimu na dini, ushirikina, uchawi na uganga, haya mambo si mazuri maana yanaharibu jamii.
Mizimu ni aina ya viumbe wa kiroho ambao ni tofaut na binadamu/mtu, na viumbe hawa wana nguvu za kutenda muujiza wowote ule, iwe uponyaji, na miujiza kama hiyo ya mvua ama kuzuia majanga.
kila jamii imepitia hizo mbanga za kuabudu mizimu, ubaya ni pale jamii za wazungu, wahindi na waarabu walipoforce kuwaaminisha watu weusi waamini Imani za Mizimu yao kuwa ni bora kuliko imani za mizimu ya jamii za watu weusi, na hapa ndipo ugumu na ubaya ulipoanza.
hakuna imani iliyosahihi maana hizi zote zimeibuka baada ya watu kusaliti Asili ya Dunia ambayo inampasa mtu kutoabudu aina yoyote ya kiumbe iwe ni hivyo vinavyojiita Mungu, mizimu, majin ama mashetan,
hivi vyote ni viumbe vilivyoumbwa hapa hapa dunian na vilijipa majina na makufuru ili kumfanya mtu awe mtumwa wao, ila ukwel unabaki ni kwamba, Asili ya Uumbaji ndiyo ilipaswa kuabudiwa, na Asili hiyo haihusiani na dini wala aina yoyote ya Miungu yenu ya uongo, na asili hiyo watu tumeshaisahau baada ya ujio wa hii mizimu/Miungu kuwapotosha watu na ndipo majanga na matatizo yalipoanzia hapa, vita, njaa, mauwaji, magonjwa, na kila aina ya matatizo yamekuja baada ya kusaliti Asili ya Uumbaji.