Mjadala: Benki nzuri kwa mikopo ya wafanyabiashara (15m-500m)

nyiokunda karibu Sana mkuu, unasuggest benki ipi 10M-100M na 100M-500M hapo kwenye kufinance biashara tofauti pengine wanafanya diversifying ya portfolio zao.
kuna tajiri namfahamu alikopa kupitia biashara ya Pharmacy akajenga hoteli kubwa. Alilipa vizuri kabisa
 
Pole Pole Sana mkuu, utasimama tena naamini usikate tamaa
 
wengi wanakopa ,na wanaishi kwa hizo hela kama zao.
wengi wanakopa kiasi kikubwa kuliko uwezo wao wa kulipa, matokeo yake mkopo huo huo unatumika kufanya marejesho. hapa hutoboi, hadi kamtaji kako ulikokuwa nako katakufa. mkopo haujengi uwezo wa kulipa mkopo
unatakiwa kuwa na uwezo wa kulipa huo mkopo kabla hujakopa
yaani mkopo usitikise biashara yako
mkopo ni taaluma ambayo wengi hawana. unamhonga afisa mikopo akupe hela nyingi, kisha zinakushinda kurejesha
 
Endelea kujidanganya mikopo ni hatari Kwa masikini
Masikini ni mentality!! You become what you think!!
Mfano una biashara inakuingizia faida ya 4M kwa mwezi kwa mwaka ni 48M
Unahitaji kupanua wigo wa biashara, kwanini usifanye Hivyo? Au unataka asset mpya? Au umepata tender kubwa?
Nimekupa challenge nitajie Tajiri unayemfahamu ambaye hajawahi kukopa, MMOJA TU
 
Elimu hii ni muhimu Sana, kingine riba za benki zetu ziko juu Sana
 
Ushauri wangu from uzoefu binafsi, pita kwao wote na hayo masharti nafuu yako, waachie wao waamue kama wanakuhitaji. Of course uwe tayari ku compromise, ukiwa kama mfanyabiashara negotiation haiwezi kuwa jambo geni.
Kwa uzoefu wako benki ipi nzuri? Itaje mkuu tupe uzoefu
 
Huyo ana idea ya biashara hiyo ,kuhusu mikopo midogo kama 20 hadi 30 kuna bank zinatoa kwa haraka. N security zake hata sales agreement. Nitarudi
 
Biashara ya pharmacy ni kuuza dawa, unaamini anaweza kujenga hotel au kuna dawa za kulevya pia.

Elewa hapa duniani kuna biashara za watu ni cover tu kuhaada watu source of income yake lakini income yake halisi siyo hiyo unayoiona wewe kwa macho.
 
watu wengi wanatajirisha benki na taasisi za fedha kwa kusema kauli uliyotoa kuwa matajiri wanakopa.....kuna situation ambazo zitapelekea mtu kukopa na kuna kitu kinaitwa bad debts na good debts....biashara kama inakwenda sawa hakuna haja ya kukopa...biashara kama inazidiwa wateja au inazidiwa mtaji uwezo wa kuhudumia au kujihudumia kugenerate profit ndio wakati ambao unaweza kwenda kukopa...vinginevyo ni kuwatafutia maafisa benki mishahara.....
 
Biashara ya pharmacy ni kuuza dawa, unaamini anaweza kujenga hotel au kuna dawa za kulevya pia.

Elewa hapa duniani kuna biashara za watu ni cover tu kuhaada watu source of income yake lakini income yake halisi siyo hiyo unayoiona wewe kwa macho.
Kwa nini umjudge mtu bila ushahidi? Kwahiyo matajiri wote wanauza madawa?
 
Tupe darasa mkuu!!
 
Unaulizia uzuri wa benki kimajengo au kua na mtaji mkubwa, mimi nadhani ungekua specifiki uulize yenye riba nafuu na masharitu mazuri lakini pia kinategemea na aina ya mkopo unao taka.
Nimeuliza kwa 10-100M ipi ina masharti nafuu, na 100M-500M ,Aina ya mkopo ni mkopo wa biashara kuongeza asset (asset financing)
 
Acha habari zako za kujifariji kama unakopa million 20 hakikisha bank account Yako Ina hicho kiasi usilete habari za kujifariji hapa wengi wamefirisika kisa hiyo mikopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…