Mjadala: Je, ni jinsi gani mtu anaweza kuacha punyeto?

Foxhound

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
28,710
Reaction score
76,243


BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU
Habari wanaJf?

Hii ni kutoka kwa rafiki yangu mmoja wa karibu sana. Amenisimulia kuwa alianza kufanya mchezo huo tangu yupo darasa la saba hiyo ikiwa mwaka 2000, alisema alianzia kwa kufanya mara moja kwa siku hadi ikafikia kipindi siku kwake ikawa haiwezi kupita bila kufanya.

Baadae ikawa anafanya hadi mara tatu kwa siku kitendo ambacho anasema kilikuwa kikimtesa sana kwani ilikuwa kwake ni lazima afanye ili akili yake ikae sawa lasivyo siku hiyo hatokuwa vizuri (huwa kama anaumwa).

Kwa sasa tayari ana mke na mtoto lakini ameshindwa kuacha licha ya kufundishwa njia mbalimbali kama kutazama mpira, wrestling, kutumia vidonge vya kupunguza ge.nye, kupaka pili pili kiganjani, kujichanganya na watu n.k.

Anaomba ushauri wenu ili aweze kuachana na hali hiyo.
---
---
---

UFAFANUZI NA USHAURI WA KITAALAMU KUHUSU TATIZO HILI
KUJICHUA NI NINI HASA?
Kwa Kiingereza tendo hili linaitwa ‘’ likiwa na maana ya kupiga punyeto. Hapa nimetumia kwa ulaini kabisa; kujichua. Lugha nyepesi na rahisi kufikika kwa wengi ni kujiridhisha! Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake.

Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha!

Wengine wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha.

INAWEZEKANAJE KUJIRIDHISHA?
Ni rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa inayotumiwa na waathirika ni kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo husika likiendelea kufanyika.

Habari mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu sana kuacha. Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo huo.

Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote. Hapa chini tutaona kwa undani jinsi tatizo hili linavyoumiza vichwa vya wengi.

Ni kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari? Zipo athari nyingi sana rafiki yangu ambazo nitazieleza hapa chini.

CHANZO NI NINI HASA?
Jambo la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo mwanzo wa kutopea huko.

Kwa vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni wakati wa kuoga.

Kwa kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo.

Huwa kama mzaha, akiwa hajui hatma yake, lakini msisimko anaoupata ndiyo unaomchanganya na mwisho wake anashangaa kila kitu kimemalizika. Unajua atakachosema? Sikia: “Mh! Kumbe ndiyo mwisho wake ni hivi? Lakini kama nimesikia starehe hivi…”
Hiyo hutokea pia wakati wa kuoga, ambapo wakati wa kujisugua kwa dodoki, msisimko ukitokea, madhara yanakuwa kama nilivyoeleza hapo juu.

Wenye umri mkubwa au wa kati, huanza tabia hii hasa baada ya kuanza mchezo wa kuangalia video za kikubwa wakiwa peke yao. Kwa sababu wanachotazama kinahusisha msisimko wa mapenzi, basi bila kutarajia hujikuta tayari!
Hii inafanana pia na kwa watoto wa kike, vyanzo nilivyoeleza hapo juu pia husababisha kwa karibu sana.

Sababu nyingine ni kunyimwa au kutotoshelezwa kimahaba na mwenzake.Wengi imewagusa, lakini kuna makundi mawili; wapo waathirika ambao wanatamani kuachana na utumwa huu na wengine wameathirika zaidi, kiasi kwamba hawana mpango wa kuacha.

Wengine wameenda mbali zaidi, kwa vile hawafikirii kuachana na mchezo huu, wamefikia hatua wanasema kwamba hakuna madhara kwa mtu anayejichua! Watu wanatetea wazi wazi, kwamba kujichua hakuna madhara. Sikia rafiki yangu, hata anayevuta sigara anajua kwamba ina madhara kwa afya yake, lakini ili kujifariji, atajenga hoja kwamba, haimdhuru na badala yake inamsaidia sana kuondoa baridi na haina kilevi.

Wakati mvuta sigara akisema hivyo, mlevi naye atakuja na hoja kwamba, pombe inamsaidia sana kupunguza mawazo. Kila mmoja atatetea upande wake. Ni jambo la kawaida kabisa.

Nikiwa naelekea kuendelea na mada yetu, rafiki yangu mpendwa kama wewe ni ‘muumini’ wa tabia hiyo, unatakiwa kufahamu kwamba unafanya jambo HATARI sana, si tu kwa afya yako, kisaikolojia na dhambi ya uzinifu ambayo hiyo itatokana na uhusiano wako mwema na imani ya dini yako, NDOA yako ipo/itakuwa hatarini.

Nadhani mnakumbuka wiki iliyopita nilieleza maana ya kujichua, namna tendo linavyofanyika na jinsi mtu anavyoanza mchezo huo bila kutegemea. Sasa rafiki, hebu tuendelee kwenye namna tatizo linavyokua.

UKUAJI WA TATIZO
Mwathirika akishazoea, hufanya tendo hilo kama sehemu ya maisha yake. Alianza bila kujua matokeo yake, lakini sasa amejikuta akianza kuupenda na idadi ya ufanywaji wa tendo huanza kupanda, baada ya siku tatu, siku mbili, kila siku na hatimaye kwa siku zaidi ya mara moja.

“Kaka Shaluwa, najichukia sana, yaani nimekuwa mtumwa kabisa wa kufanya huu ujinga.

Kwa siku nafanya mara mbili au zaidi, lakini si chini ya hapo,” alisema rafiki mmoja, aliyenipigia simu baada ya kusoma sehemu ya kwanza ya mada hii wiki iliyopita.

Ukweli ni kwamba, mfanyaji kwa vile ameshapata ‘mteremko’ wa kutimiza haja zake, kwanza ataanza kuwadharau wanawake/wanaume, kwamba hawawezi kumtisha, kwa sababu ana njia za kujifurahisha mwenyewe.

Pili, hufikia hatua ya kuwachukia watu wa jinsia pacha, akiwaona kama ‘wanaringa’ hasa kama atakuwa amemshawishi kimapenzi na kukatawaliwa.

ATHARI ZAKE
Zipo athari nyingi sana ambazo mwathirika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo huu. Hapa nataka nizungumze kwa herufi kubwa kabisa kwamba, ndugu zangu usidanganyike kwamba hakuna madhara kwa kufanya mchezo huu.

Yapo MADHARA makubwa sana ambayo yanapatikana kwa mchezo huo. Achana na propaganda za mitaani, zenye utafiti hewa.

Sikia nikuambie rafiki yangu, hasa wewe ambaye unafanya mchezo huo. Upo kwenye hatari kubwa ya kushindwa kufurahia mapenzi, kwa vile mazoea ya kiungo siri chako ni kwenye vitu ‘artificial’ zaidi ya ‘natural’.

Mwanaume aliyezoea kujiridhisha mwenyewe, akikutana na mwanamke, hana muda mrefu sana, kila kitu kinamalizika.

Siyo hivyo tu, uwezo wa kurudia tendo unakuwa mdogo au unakosekana kabisa. Kinachotokea ni kwamba, kiungo siri chake kinakuwa kimeshazoea, aina nyingine ya ‘hali ya hewa’ hivyo kinapokutana na sehemu siri za kike, ambazo ni laini na zenye ute mwepesi, inakuwa rahisi kumaliza ‘biashara’ mapema wakati wateja bado wanahitaji!

Kiungo siri cha mwanaume huwa kigumu, hivyo kusababisha maumivu kwa mwanamke kutokana na sugu aliyoitengeneza bila kujua. Kwa kawaida viungo siri vyote ni laini sana na vinatakiwa kubaki katika hali hiyo ili kuleta msisimko wenye usawa.

Mazoea yoyote tofauti na yale ambayo yanatakiwa hupunguza msisiko na kusababisha mmoja wa washiriki wa tendo la ndoa kubaki na kiu na mwenzake.

“Najuta kuufahamu huu mchezo, kila siku ninapokutana na mume wangu, ananiacha nikiwa sijatosheka. Kiukweli tangu amenioa, sijawahi kufurahia tendo la ndoa. Nilianza huu mchezo zamani sana, tangu nikiwa kidato cha tano.

“Kuna rafiki yangu mmoja nilikuwa nakaa naye bweni moja alinifundisha. Sikujua kama madhara yake ni makubwa kiasi hiki. Ilikuwa ni shule ya wasichana tupu, kwa hiyo akanidanganya kwamba tuachane na wanaume tujichue…kumbe alikuwa ananisaga!” hii ni sehemu ya ushuhuda mwingine wa mchezo huo.

Athari nyingi ambayo mtu anaweza kuipata kwa kujichua ni kumaliza ‘kazi’ mwenyewe bila hata kwenda kazini. Akipita mtu wa jinsi pacha, ambaye ana mvuto, kazi inaishia hapo hapo!

UPO KUNDI GANI?
Uko wapi rafiki yangu? Nazungumza na wewe ambaye unafanya mchezo huo, bado unataka kuendelea nao au unatamani kuacha? Shika maneno yangu, kwamba ni HATARI kujichua, halafu weka nia ya kutaka kuacha huu utumwa, kisha vuta subira hadi wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ambayo haitaacha kitu.

MFADHAIKO
Mtu ambaye anaendekeza kazi hii, hupata mfadhaiko. Anayepata mfadhaiko, huwa mwepesi sana wa kuwa na matamanio kwa jinsia ya upande wa pili.

Si ajabu mtu mwenye mchezo huo, kutembelea akimwangalia mwanamke kuanzia Magomeni hadi Manzese! Amefadhaika. Ameshazoea kumaliza kazi nzima akiwa peke yake, kwa hiyo raha yake inabaki kuwa katika picha tu na si kitu halisi.

Macho yanakuwa juju juu, si kwa kupenda, ni kwa sababu tayari ameshaathiriwa na tatizo hilo. akitoka hapo, ujue moja kwa moja faragha, anaanza mambo yake. Kelele nyingi, kumbe yupo peke yake!

Mfadhaiko hauishii hapo, hata akiwa kwenye vyombo vya usafiri au mkusanyiko wa watu, mwathirika huweza kumaliza ‘kazi’ kwa macho tu, tena wakati mwingine bila kuwa na taarifa. Anakuja kugungua baadaye sana, kwamba kumbe kila kitu kilishafanyika bila hiyari yake.

KUSHINDWA TENDO LA KAWAIDA
Mwenye mchezo huo, pamoja na uhodari wake wa kujifurahisha akiwa peke yake, anapokutana na mwenzi wake faragha, kazi inakuwa si ya kiwango cha kuridhisha. Kuna athari nyingi ambazo hujitokeza.

Kwanza, anakosa ujasiri, hayupo tayari kuandaliwa, kumuandaa mwenzake. Kishazoea kufanya kila kitu haraka haraka, tena kwa kutumia hisia zaidi kuliko uhalisia wa tukio lenyewe.

Anakuwa goigoi, anachelewa kuwa tayari, hata akiwa tayari anafika safarini mapema zaidi. Mbaya zaidi, akifika hawezi kuanza safari nyingine. Hata kama akianza, kuna uwezekano mkubwa wa kuishia njiani.

Baadhi yao, hubaki wakiwa baada ya wahusika wao kuwagomea katikati ya safari. Zipo athari nyingi zaidi ya hizo, kutegemea na namna tatizo lilivyokomaa na aina ya jinsia.

KUFEDHEHEKA
Baada ya hayo hapo juu kujitokeza kwenye ndoa/uhusiano wa mwathirika, kinachofuata sasa inakuwa ni kufedheheka. Kwa bahati mbaya sana, unaweza kufanya siri mchezo wako, lakini athari zikawa wazi kwa mwenzako.

Hata kama hatagundua chanzo cha tatizo, lakini atagundua kwamba huna msisimko, huwezi kazi au vyovyote vile. Wengi husema kwa hisia, humaanisha kwamba hakuna wanachopata kutoka kwa wenzao, lakini mambo yakizidi kuwa hovyo, wanafunguka: “Mwenzangu kila siku unaniacha na kiu, una tatizo gani?”

Kauli hiyo rafiki yangu, inatosha kabisa kukufanya ushindwe kazi moja kwa moja. Unajua nini? Utaanza kuwaza: “Kumbe siwezi kitu…halafu mwenzangu ameshagundua. Nitafanyaje mimi? Mbona nahadhirika?”

Ndugu yangu, ikifikia hapo utakuwa unamkimbia mwenzako na kwenda chemba kumaliza biashara zako mwenyewe. Furaha ya moyo itatokea wapi? Kama ndiyo mnaishi kinyumba au mpo ndani ya ndoa ndiyo kabisaaa!
Umeona kazi hiyo?

UNATAKA KUACHA?
Hakuwa dawa kubwa sana ya kuacha mchezo huu. Najua wengi walikuwa na hamu ya kutaka kusikia, wataachaje huu mchezo. Ndugu zangu.Usitarajie kwamba nitakuja kuingia kwenye nafsi yako na kukuambia ACHA KUJICHUA! Ndugu zangu, nitawapa dondoo chache sana, lakini kubwa ni kwamba ATHARI nilizotaja hapo juu zinatosha kabisa kukubadilisha!

Hebu nikuulize, utakuwa na hamu ya kuendelea na haya mambo kama ndoa yako itakuwa hatarini? Nani atakubali kufedheheka? Nani atakubali kupoteza heshima yake? Bila shaka hakuna. Pitia dondoo zifuatazo;

(i) Badilisha utaratibu wa kulala, lala kifudifudi, badala ya chali (rejea maelezo yangu ya awali kuhusu chanzo cha tatizo)
(ii) Acha kuangalia mikanda ya kikubwa ukiwa peke yako.
(iii) Kaa mbali na simulizi zinazohamasisha mapenzi, mazungumzo ya aina hiyo na kampani za watu wanaopenda kusimulia mambo ya faragha.

(iv) Acha mazoea ya kujishika sehemu zako za siri.
(v) Fanya mazoezi ya viungo angalau robo saa tu kwa siku.
(vi) Juu ya yote haya, FUTA kabisa mawazo ya jambo hilo. AMUA kwa dhati ya moyo wako, tambua na ogopa athari ambazo unaweza kuzipata, kisha ACHA KABISA mchezo huo ili kulinda heshima yako na kujipa furaha ya maisha

BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU:
---
---
---
---
---

---
Ndugu na rafiki wa jamii forum naomba maoni Juu ya hihi mada..nasi tuma maoni yetu ndani ya link hihi ambayo itakusaidia kuelewa sayansi ya PUNYETO na namna ya kuachana nayo ....usiache kusubscribe na kutoa maoni yako
---



PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HII:
- Punyeto: Nilivyoanza, nilivyoacha na hali ya sasa - JamiiForums
 
Mwenzenu nilikua mhanga wa hio ishu ila nashangaa najikuta mwezi wa nane sijafanya .
Lakini kabla ya hapo siku 3 zilikua hazipiti acheni jamani ukiwa na imani kwa Mungu hakuana kinachoshindikana. Mwambie asali sana ana asikate tamaa atajikuta kaacha tuu.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Kwanza pole sana ndugu, na usijihisi mnyonge maana kati ya watu 20 waliokomenti hapa yawezekana asioatikane hata mmoja ambaye hsjajilipua, even akina dada.

Selfie imekuwa ni tatizo sugu la wanaume wengi, hata waliopo kwenye ndoa hujikuta wakipiga kabla yakukutana na mwenza wake au hata muda mchache baada yakukuta kimwili!

Nini kifanyike ili uweze kuacha?

Jiweke busy na kazi, fanya kazi za mikono, jisomee magazeti, tizama mpira, acha kuangalia movie zenye ngono ndani yake, acha kabisa kutembelea blogs na websites za video za ngono.
Pia usichati na mwanamke kuhusu ngono kama haupo karibu nae ili ashiki ikikukamata mfanye.

Sali au Swali sana Mungu atakusaidia.

Mwisho kumbuka Selfie hukupatia raha ya dk 5 kati ya masaa 24 ya siku, kwamaana nyingine utakuwa nahasira na msongo wa mawazo kws masaa 23 na dk 45 ,mara baada ya kujifyatua.

Selfie huleta raha kwa muda mfupi ila ina madhara mengi sana ambayo ukiyatafakari kwa kina ndonga ni lazima ilale usingizi, tazama madhara ya Selfie

1. Majuto na Msongo wa mawazo mara tuu baada ya wazungu kutoka

2. Nguvu nyingi kupotea mwilini (ukijilipua mara moja nguvu unazopoteza mwilini ni sawa na mtu aliyekimbia kwa kasi km 7 bila kupumzika)

3. Hufifisha uwezo wa kufikiri, husababisha ubongo kupoteza kumbukumbu na kusahau mara kwa mara, mfano kushika simu na mkono wa kushoto huku ulitumia mkono wa kulia kuitafuta hadi chini ya kitanda wakati mwingine unaweza hata kuazima simu ya mtu kubeep simu yako uliyoishikilia kwa mkono wa kushoto!

4. Misuli ya kiuno na ya uume kulegee hivyo kukufanya kukosa nguvu za kiume au kuwa na uwezo mdogo wakusimamisha, yaani uume husimama hali ukiwa legelege kiasi hata cha kondomu kushindwa kuvalika, acha tuu kumridhisha mwanamke!

Kujilipua husababisha ndonga kuwa na hisia kali na za haraka unapokuwa na mwanamke chumbani, yaani kitendo cha kumtomasa mwanamke unajikuta ushajikojolea, hii inaleta karaha na fadhaa sana, hivyo kupelekea kushindwa kumridhisha mwanamke kingono. Hii itakufanya ujiskie hovyo na hata kuogopa kuwa na mwanamke ukihofia aibu iliyowahi kukuta ulipokuwa na salome wako.

5. Mwisho Selfie huvunja vunja na kuua viungo vya mwili na dalili zake,nutaskia kelee (mf. Tasuu) kwenye magoti na viwiko vya mikono, sana sana magotini!

Fikiria zaidi hayo madhara utaacha kabisa kujichua kama ulivyoacha maziwa kwa mama yako.

Mwandishi wa makala haya, ni Mwalimu wa Biolojia kutoka chuo kikuu cha Finland,( University of Finland) na pia ni mtaalamu wa Maswala ya Afya ya uzazi!
 
Tatizo la punyeto limekuwa ni tatizo la muda mrefu la vijana wengi na wengi kwa namna moja au nyingine wameshindwa kuacha ingawaje wengi wanachukia sana kitendo hicho.

Mbaya zaidi wengi wanapiga punyeto halafu vyakula wanavyokula havina ubora na vinazidi kudidimiza nguvu zao za kiume.

Katika uzi huu tutajaribu kuangalia mzizi wa tatizo (nini kinapelekea watu wapige punyeto) ,kwa nini ukiingia huwezi kuacha, je tangu uanze kujichua umenufaika kwa mangapi na umesababisha kuharibu system ya maisha yako kwa kiasi gani, namna ya kuliondoa tatizo(kuacha kujichua) namna ya kurudisha nguvu za kiume zilizopotea kipindi chote cha kujichua


Karibuni mtiririke
 
Sijui kwanini nimekua wa kwanza kuuona huu uzi!!

Boss, hii kitu ni balaa usipoweka nia na kuichukia. Yaani uweke nia alafu uichukie toka moyoni hapo ndio utaiacha!! Otherwise utakua unapiga marktime!!
 
Nina uhakika kabisa asilimia 65 ya wanaume katika kipindi cha ukuaji wao,walijiusisha na huu mchezo ambao ukianza kuacha mpaka upate msichana ambae unakaa nae kabisa..
 
Duuu,nilidhani ni habar kamili kumbe ni trailer
Nimefanya hivyo sikutaka niwatafunie kila kitu

Nimeacha kwanza nione watu huwa mna mtazamo gani juu ya suala hili kabla sijaanza kutoa suluhisho na namna ya kuzirudisha nguvu zilizopotea kwa kasi zaidi.
 
Kila kitu ni nia, ukitia nia unaweza ila binafsi ninaamini kuwa ukiwa bize na shughuli za hapa na pale inakufanya mtu ubongo wake ukoconcetrate katika mambo mengine ambayo ni ngumu kukupelekea kuwaza ngono.
 
Kila kitu ni nia, ukitia nia unaweza ila binafsi ninaamini kuwa ukiwa bize na shughuli za hapa na pale inakufanya mtu ubongo wake ukoconcetrate ktk mambo mengine ambayo ni ngumu kukupelekea kuwaza ngono.
Noted
 
Balehe ni mojawapo ya sababu ya kupiga punyeto, sasa hiyo tabia inaendelea iwapo hujapata mwenza na kupelekea kuwa senior punyeto cracker.

Nyingine ni mifadhaiko labda umemuona mwanamke amenona au umeangalia picha, video za ngono nayo inapelekea punyetoism
 
Nimefanya hivyo sikutaka niwatafunie kila kitu

Nimeacha kwanza nione watu huwa mna mtazamo gani juu ya suala hili kabla sijaanza kutoa suluhisho na namna ya kuzirudisha nguvu zilizopotea kwa kasi zaidi.

Unaleta vitu nusunusu vyanini sasa....heading ya maana halaf uzi mwepesi
 
Nataka nichukue baadhi ya mawazo ambayo ni basic zaidi halafu naenda ku edit uzi kwa kuongezea na vitu ninavyovijua ili msomaji apate urahisi zaidi maana sio wote wanaweza kusoma comments zote za watu bali kuna wengine wanasoma mwanzoni mwa thread basi halafu wanaondoka sasa kama hakutakuwa kumeshiba sana tutakuwa hatuja tatua tatizo bado kwa sababu watakao nufaika ni wachache
 
Sometimes mtu yupo single, kutongoza gals anaona usumbufu coz mtabembelezana wiki kadhaa, kuchukua milupo unaogopa magonjwa na ww ni mzee wa vukavuka, kwanini asijisitiri na nyeputo.

Its Affordable and Safe ama mnasemaje wazee wa CHAPUTA🙂🙂.

Hzo ni kati ya sababu, vema tukajikita zaidi kwenye kusaidia pipo waachane na hii kitu yaani unakuta mwingine mpaka anaoa lakini haachii uwanachama. Hii na kwa KE, hawa wanakuja kwa kasi sana siku hz, wanatoys kabisa
 
Salaam wazee wenzangu,

Rejea mada tajwaMMwenzenu nlianza kupiga puli/Punyeto 2003. Kuna wakati naacha Ila inafika kipindi natamani kupiga tena.

NIna mademu na napiga show ya nguvu ioa baada ya muda napiga puli
So nimeamua niache ila sijui nitumie dawa gani ambayo itanisaidia moja Kwa moja kuacha hii Punyeto jamanii msaada please.
 
its not simple kaka but kama unania kweli ya kuacha fanya yafuatayo:

01:Acha kuangalia video,picha za ngono (porn)

02:achana na stories za ngono sababu hizo zinachangia sana

03;epuka kukaa mwenyewe kwa muda mrefu penda kukaa na company na io company muwe mnazungumzia issue zingine.

04:usikae bila kufanya kazi (kuwa-busy) kila muda jishuhulishe NB fanya mazoez sana hasa nyakati za jion inakata kiu sana sabab viungo vinachoka.

05:ikitokea umefanya yote na bahat mbaya ukajikuta umerudia usikate tamaa maana ningumu kuacha mara moja endelea na hiyo dozi.

06:usi-ruhusu mawazo yako kuwaza wanawake au ngono ikiwezekana usipende kujichanganya na wanawake sabab ukimuona mwanamke haswa wale wako sex utaanza ku-create image ya maungo yake yandani na hiyo itakua kichocheo.

07:mwisho kwa leo jiweke zaid kwenye dini kama wewe mkristo penda kusoma sana neno.mafundisho pia unaweza kumshirikisha kama ni pastor au Sheikh au muumin yoyote unamuamin akusaidie kiroho zaid.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…