Nimejiwekea Mpango Mkakati wa kuacha Punyeto nimekusudia na nina hakika sitopiga tena Punyeto. Karibu katika Thread hii hujifunze na tupeana mbinu mbalimbali za Kuacha na Punyeto.
Siku ya Kwanza yenye Massa 24, ilikuwa jana nliamua na nimehacha kupiga Punyeto,
Ilikuwa ni tabia niliyokuwa nayo kwa miaka kadhaa mpaka siku ya Jana nilipoamua kuacha kabisa. Nimeona jinsi nilivyokuwa nakifurahia kitendo hiki kabla ya kupiga Punyeto ila nikishapiga najutia na ninachukia naona nimekosea sana. Nilisoma Faida zake kwenye Mitandao na baadae nikasoma Madhara yake.
Ila kutokana na Maamuzi yangu ambayo nimeyafurahi sana nimeamua kuacha kitendo hiki na Ninamshukuru sana Mungu kwa kuwa amenihakikisha kuwa naweza tena naweza zaidi kuacha na kutokurudia kupiga Punyeto.
Asante Mungu
Siku ya Kwanza Jana 1 Nov 2020
Leo Tar 2 Ni siku yangu ya Mbili toka nimeacha kupiga Punyeto, na Leo nimejitahidi sana kujiepusha na kukaa mwenyewe au pekee yangu. Kuna wakati hali ilikuja ila nikaamua kwenda nje nikatembea kidogo niliporudi hali ikawa imetulia.
Siku ya Pili nimeishinda hii hali, nimedhamiria Moyoni, na najua nitaweza na Mungu ananisaidia