Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

hapana mkuu, ukiifanyia matengenezo inafika zaidi ya hapo. naona ipo mitaa sawa na wakina Altezza, na baadhi ya 2.0L engine cars.

Hapo niliposema huo ulaji nilicalculate siku moja kulikua na heavy traffic Buguruni. nadhani kwa Foreni za kawaida unaweza piga 10km/L.

Naijua Voltz kwa kiwango chake. Naweza kukushauri uichukue coz kwa ukubwa haitofautiani sana na Xtrail.

Voltz ilitengenezwa kwa corabollation ya Toyota na General Motors, mwaka 2002 to 2004. Zilitengenezwa units 10,000 tu. Ila usiogope kuhusu spare parts coz inaingiliana na corolla nyingi tu kama Allex, Auris, RunX, corolla saloon etc.

Ina engine ya displacement 1.8L either 2ZZ_GE au 1ZZ_FE zote i4. Ni four wheel drive na hiyo engine unapata 118hp. So ata uko ulipokutaja kuwe na milima au matope usiwe na wasiwasi
Nimewahi endesha hapa Dar kama Mwezi mmoja. Ulaji wake wa mafuta kwa hapa Dar ni 8/9km kwa lita. Highway inafika hadi 11km kwa lita. Sio paperwork I traveled with her Dar to Dodoma once.

Ina shape nzuri na ndani ipo comfortable sana. Handling poa sana.

48373d81304dd83fda63cb090dac758a.jpg


5eca222f267bbbea94cefc4083674992.jpg


7d1619ae9789e8a7f02b70a814b72607.jpg
Mbona ni LHD mkuu? Volts ni nzuri lakini kwa uchache wake ukiharibika body spare itasumbua sana kuipata. Engine parts zinaingiliana na hizo gari ulizotaja. Bora achukue Harrier 4 cilinder ingawaje engine zake nyingi ni 2.4L hadi 3.0L
 
Hiyo gari kuna siku nilikuwa garage nimeikuta apo inatengenezwa fundi anasema ni bora upewe gari aina ya Toyota 10 kuliko upewe hiyo moja.
 
Mbona ni LHD mkuu? Volts ni nzuri lakini kwa uchache wake ukiharibika body spare itasumbua sana kuipata. Engine parts zinaingiliana na hizo gari ulizotaja. Bora achukue Harrier 4 cilinder ingawaje engine zake nyingi ni 2.4L hadi 3.0L
Hiyo picha nime download tu ndio maana. Ila nyingi tu RHD.

Jamaa nimeona analalamika 9km/L sasa ataweza kweli Harrier kaka 2.4L au 3.0L?
 
Ofisi zenu ziko wapi na ninyi ni maagent wa kampuni gani ya japani?
 
Nissan ina roho ngumu, mimi ninayo nissan march, spare ukifunga umefunga. Spare zake ni genuine ndiyo maana ni gharama kidogo. Gereji huendi mara kwa mara. Hutojuta kuwa na nissan
 
Akili za wengine changanya na zako ili upate jibu sahihi. From simple analysis kwenye hii mada 92% wameeleza matatizo makubwa ya Nissan Xtrail kwenye gharama ya spear, maintenance costs, fuel consumption, na mambo kede kede ambayo mwisho wa cku UTAJUTA, it's up to you to decide. Ila kama mpunga uko vizuri beba baba!
 
usijaribu hiyo gari itakufilisi utauza hata kuku kabla hawajaanza kutaga ili utengeneze gari,shockup moja shs 600000 wakati ya rav4 ni 80000,ninayo imenishinda hata kuuza haiuziki mtu anakuja anasema labda nikupe3,000,000
Ya Rav 4 haimalizi miezi 6, lakini ya Nissan ni miaka siyo chini ya 10. Nina Nissan serena nimetoa shock up baada ya miaka kumi toka niinunue Japan! Zinasumbua, lakini Mombasa zipo tele. Nilinunua mbili za mbele kwa 600,000 Tsh.
 
Akili za wengine changanya na zako ili upate jibu sahihi. From simple analysis kwenye hii mada 92% wameeleza matatizo makubwa ya Nissan Xtrail kwenye gharama ya spear, maintenance costs, fuel consumption, na mambo kede kede ambayo mwisho wa cku UTAJUTA, it's up to you to decide. Ila kama mpunga uko vizuri beba baba!
Muzi, Angalia post #47, kuna kitu nimeandika
 
Nina Xtrail mwaka wa nne sasa. Cha muhimu ni umpate fundi permanent na anayejua. spea zake ni gharama lakini ukiifunga utasahau kwa safari ndefu ni nzuri wala huchoki
Ndugu hiyo Nissan miaka 4 nipe contacts za fundi unayemuamini kuwa anazijua gari hizo. Pia service unafanyia wapi kwa hapa Dar. Spare original zinapatikana duka gani. Pia nataka ushauri jinsi ya kuitunza. Asante
 
Wadau nimejichanga toka 2014 mpaka leo nimetimiza lengo la kama 8000 USD nataka kuagiza Nisaan X-trail toka japan. Mwenye ujuzi wa hiz gari msaada tafadhali. Vipi ulaji wa mafuta, spea, ugumu kwa barabara za bonyokwa hukoooo...
Kwa muoenekano iko bomba,lakini durability ni ndogo sana fight upate Rav4
 
Kitu kingine kinachonivutia kuhusu NISSAN, watu ni wachache, ule wizi wa taa, vifaa vya gari haupo katika NISSAN, tofauti na TOYOTA.
 
Hakuna gari mbovu ni wewe na maintenance yako soma manual book ujue inahitaji nini, epuka oil na spare za bei rahisi..
 
Hahaha! Niliwahi kumiliki hicho kipando ilikuwa kabla sijakiwasha kuanza safari natest namba ya fundi wa karibu wa maeneo ninayokwenda kwa kuwa chochote kinaweza tokea!
Hahaha hapa imebidi nicheke tu[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Daah! X trail ni ugonjwa wa moyo bora hata Passo
Hivi Passo shida yake ni nini hasa? Umbo lake au performance au vyote? Maana karibu thread zote zinazohusu passo humu ni inawekwa katika kejeli zaidi...shida ya hii gari ni nini hasa kwa wazoefu?
 
Mkuu wasikutishe mimi ninayo mwaka wa tano sasa nimetembea nayo nchi nzima na hivi jana nimetoka nayo kigoma. Suala la spear kuwa ghali siyo kweli ni kasumba tu ya baadhi ya wauzaji kwa sababu ukinunua utasahau lini mara ya mwisho uliinunua.

Fanya hii simple research angali Xtrail ngapi zipo njianni leo tangu nambe T .... AAA angalia hata zisizo na matunzo bado mwonekano upo poa linganisha na brand zingine


Kuhusu mafuta ni driving habit ya mtu, kama ni mtu unapenda rally mjini, highway yaani kila mahali hata uwe na vitz itakula above normal. Ila kama una accelerate kawaida kwa maana hulazimishi kuondoka kwa kasi, kutaka gari ifike 100km/hr ndani ya mita chache basi mafuta inakula normally. Kwa lugha raisi kama uliwahi kuwa na GX100 haina utofauti na Xtrail 10-11km per litre highway na around 8 - 10 town errand.


Naomba nitoe elimu kwa watu kuhusu ulaji wa mafuta. Magari mengi ya kisasa yamefungwa kitu kinaitwa oxygen sensor. Hii kitu ni muhimu sana sana kwa wenye kutaka kuokoa ulaji wa mafuta. Kazi yake ni kutoa signal kwa fuel control system kwamba ongeza ama punguza mafuta ili yachomwe vizuri na kwisha kabisa. Zikifa maana yake fuel consumption inakuwa kubwa unabadili filters, plug, nozel etc bado ulaji unakua juu.

Life span ya hizo sensor ni 100,000km sio mpaka zikupe alam. Kama gari yako iliwahi kuunguza cyllinder head na kuchanga maji na oil kwa vyovyote siyo nzima. Badilisha
 
Back
Top Bottom