Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Klugger ni mnyama chukua hutajuta

Ishu ya magari hii nahisi inategemeana sana na mtunzo anayoyafanya mmiliki. Gari kama gari ni kifaa kama ilivyo vifaa vingine kama Simu au Saa za mkononi, usipokuwa mtu wa kuijali gari yako unaweza ukalalamikia gari fulani kuwa mbovu ili hali kuna mtu anaikubaki huwezi mwambia kitu.

Mie nina Brevis kangu, watu wa humu Jf wanakarushiaga mawe hadi unaweza omba ukarudishe Yard ukauze kwa bei ya mradi umeiuza. Hii gari nimekuwa nayo, naifurahia sana, Mafuta inatumia vizuri hasa unapokuwa na safari ndefu na pia ni stable sana Barabarani
 
Umetumia maneno mabaya kwenye reply yako mimi nimeshamiliki Nissan zifuatazo
Nissan Serena engine zake zinaigiliana na Xtrail ugonjwa wake unafanana...
Mkuu Ile reply Yangu nimeongea Kwa ujumla hasa hapa jukwaani. Pia haina uhusiano na comment yako Ndugu Yangu.
 
Hii gari ikichemsha incase umesahau kutia maji kwenye rejeta au inavuja ujue itaua piston blocks...hapo unakua huna namna zaidi ya kubadili Engine...ishanitia hasara ya Engine sina ham nayo...mafundi waliniambia Engine zake ni Alminium...
 
Nissan ni gari confitable roading yaani ikiwa kwenye speed inatulia tuli hausikii mtetemo wowote hasa ukiwa ufunga vioo na umewasha ac
 
Ninayo NISSAN X-TRAIL tangu mwaka 2011 hadi leo iko barabarani. Nimebadikisha fan belt mara moja na ball joint mara mbili. Stabilizer link ndo mara nyingi. Lkn sijaona tatizo hiyo gari kabisa. Ni nzuri kwa masafa marefu. Uwe makini na mfumo wake wa upozaji.
 
Nadhani watanzania wengi ni watu wa kusikia na kupitishwa mambo hata wasiyoyajua. Bro ni Xtrail ni gari moja nzuri Sana kuliko hata Harrier. Naongea nikiwa na uzoefu wa hizo gari.

Watu wanasema sio nzuri lakini hawakuambii shida ni nini. Yenyewe ni Kama gari Toyota za kisasa mfano Noah vox zenye gearbox za chain Lazima utumie special transmission fluid(CVT) Kama unataka idumu.

Xtrail haitaki oil za ajabu ajabu Kama ni 5w30 za total, tumia hiyo au zinazofanana transmission tumia type ii au iv. Na fanya service kwa wakati hutakaa usikie shida yeyote. Mi nimeitumia zaidi ya 4yrs sijawahi kupata shida nayo na kila siku ipo safari I. Nimenunua ikiwa na 68,000km Leo ipo 391,000km bado Chuma inatembea na leo umeenda Lushoto.

Kwa hiyo tusitishane au kufokeana
 
Back
Top Bottom