MJADALA: Je, Pikipiki gani ni bora kwa matumizi ya nyumbani au biashara kwa Tanzania?

MJADALA: Je, Pikipiki gani ni bora kwa matumizi ya nyumbani au biashara kwa Tanzania?

Twende pamoja kwa waliotumia na wanaotumia pikipiki tuu.

Kati ya hizi pikipiki unaipenda sana ipi na kwanini(based katika matumizi binafsi)?
1. Boxer
2. SANLG
3. Feckon
4. TVS King
5. Hero
6. King Lion
Kati ya hizo zote, hakuna pikipiki yenye ubora hapo
 
Hii yamaha crux ni pikipiki nzuri sana.
1. Inakula wese vizuri tu lt1 unaenda mpka 55km hadi 60km kutegemea na uendeshaji wako
2. Ina kamlio flani amazing kama kamluzi hivi, kapo kwenye yamaha nyingi (huwa nakafurahia)
3. Sio yeboyebo kama mchina, zipo chache.
4. Service ni kawaida tu, mie natumiaga total oil 8000/= na 500/= au 1000/= ya fundi kumwaga oil. Service huwa nafanya kila mwezi, pikipiki ni binafsi halafu haina mizunguko zaidi ya mishe zangu na nyumbani tu.
Changamoto nlizokuwa napata ni pamoja na; 1. Upatikanaji wa vifaa (sio kila duka waweza pata spea).
2. Brake zake sio strong kivile sababu ni drum especially ya mbele halafu utaudjust sana hizo break ili zibaki na ile grip unayoitaka
3. Tairi zake ni nyembamba zinataka lami tu kwa hiyo ukipita sehemu yenye kamchanga kuwa makini sana sana sana sanaaa..... yaani kwa lugha nyingine ukiona mchanga punguzu mwendo mapema sana kabla hujawa maarufu mbele ya umati wa watu kwa mfano anapopita SanlG,Fekon n.k kama kuna mchanga unaopitika vizuri tu, ukiwa na yamaha crux unaweza kukutupa chini.
Vilevile tairi zake ni za tube kwa hiyo ukipiga msumari haina cha kusubiri ndani ya dk moja upepo kushnei, sali sana sehemu ya mafundi iwe karibu.
4. Kana gia 4 tu kwa hiyo kanadai sana gia
5. Ngoma ni kick to start only
Mbali na hizo changamoto naikubali sana.
Nashukuru kwa uchanguzi ulio balance pande zote
 
Wacha maneno pikipiki kwa matumizi binafsi ni mnyama Honda ace tu na jamii zake nyingine na hakuna ubishi katika hilo.
 
Naam!? Mkuu nilijibu nikiwa na haraka kidogo lakini Honda ace ni pikipiki ngumu kiujumla kuanzia kwenye injini mpaka nje lakini kama wewe ni mbeba mizigo mizito sana kwenye pikipiki hii haikufai ila nimezitumia sana ninazijua vzr ndio maana hata leo dukani bei zake ni juu kidogo mm nilichukua used kwa mtu ambaye ameitumia toka 1998 lakini ukiiona huwezi kuamini kama ni ya mwaka huo
 
Naam!? Mkuu nilijibu nikiwa na haraka kidogo lakini Honda ace ni pikipiki ngumu kiujumla kuanzia kwenye injini mpaka nje lakini kama wewe ni mbeba mizigo mizito sana kwenye pikipiki hii haikufai ila nimezitumia sana ninazijua vzr ndio maana hata leo dukani bei zake ni juu kidogo mm nilichukua used kwa mtu ambaye ameitumia toka 1998 lakini ukiiona huwezi kuamini kama ni ya mwaka huo
Mimi mizgo n kg 20 kurud itafaa?

Sent from my itel S12 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Umetaja Piki piki Nyingi tuu kama Boxer,Fekon,Sanlg,TVS,nk
Ila Mwisho wa yote Kuna Pikipiki moja inaitwa HOAUJUE...au Kiswahili wanasena "Haujue"....hi Pikipiki ni Nomaaa Asikwambie Mtuu,Uliza waendesha Pikipiki watakuambia...
Ni Imara,inapiga Mzigo na Nzito.
Ikitulia Barabarani Hakuna na Boxer, TVS,au wala sijui nini atafuata hii,
Niliwahi Siku moja Kupakia Mzigo wangu,gunia 2 za Nazi kwenye "Hoaujue" nami nikapanda Boxer,Tumeanza tuu Boxer akatupita akaenda mbali,baada ya kama Dk 7 hivi,lilitupita kama tunesimama,Nikamwambia Dereva wa Boxer Aisee vipi ongeza mwendo Mkuu,akaniambia hiyo ni "Hoaujoue" taamka "Haujue" ni balaa siwezi fuata pale linapokuwa limechanganya!
Na ni BORA usipime! Yaani Imara!
Inavumilia kila hali!
Haojue ndo habari ya mjini, nimeikubali
 
Back
Top Bottom