MJADALA: Je, unapendekeza Serikali na Sekta Binafsi zifanye nini cha tofauti ili kuondoa tatizo la ajira nchini?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Takwimu za Benki ya Dunia na Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Jamii na Uchumi (REPOA) zinakadiria takriban watu 800,000 hadi 1,000,000 huingia katika Soko la Ajira Tanzania kila Mwaka, ambapo wanaopata kazi ni kati ya 60,000 hadi 200,000 tu

Je, unapendekeza Serikali na Sekta Binafsi zinafanye nini ili kupunguza au kuondoa kabisa changamoto ya Ukosefu wa Ajira nchini?

kazi.jpg
Mjadala.jpg

Je, ni fursa zipi ambazo bado hazijawekewa nguvu au uwekezaji nchini unaoweza kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya kilimo, Biashara, Elimu, Digitali, Afya au Michezo?

Pia soma: Je, Serikali ina mpango gani na ongezeko la ajira nchini Tanzania?

Ungana nasi katika Mjadala utakaofanyika Leo Alhamisi Julai 25, 2024, kupitia XSpaces ya JamiiForums, kuanzia Saa 12 Jioni hadi Saa 2 Usiku

Kuingia na kusikiliza na kushiriki kwenye mjadala utabonyeza hapa:

Malembo Lucas, Mkurungezi wa Malembo Farm/ Mshauri wa Kilimo Biashara
Umri wa Wastani wa Mkulima wa Tanzania ni Miaka 60, kwa Mujibu wa FAO, lakini nusu ya Watanzania ni Vijana

Vijana waliopo kwenye Sekta ya Kilimo ni wachache sana, sababu kubwa ni Mtazamo

Vijana wengi wana mtazamo hasi kuhusu Kilimo, Vijana wanaona Kilimo ni kazi ngumu au Adhabu

Sababu nyingine inayowafanya Vijana wasichangamkie Fursa za kilimo ni Mitaji. Vijana wengi hawana Mitaji

Kwenye Miaka ya 70 Mikopo ya Kilimo ilikuwa ni zaidi ya asilimia 30

Changamoto kubwa ni kuwa hatujafungamanisha Sekta ya Fedha na Kilimo hali inayosababisha Vijana kushindwa kupata usaidizi wa fedha za kuingia kwenye Kilimo

Muhimu ni kufungamanisha Sekta ya Kilimo na Sekta ya Fedha

Yaani kama Kijana ana andiko lake zuri kuhusu Kilimo aende akaliwasilishe Benki na aweze kukopesheka

Vijana wengi wanakosa Mikopo kwa kukosa dhamana

Tatizo lingine linalokwamisha Vijana kuingia kwenye Kilimo na Ufahamu na Ufikiaji wa Masoko

Mkulima ana mazao ila hajui auze wapi, na mnunuzi anataka bidhaa ila hajui anunue wapi

Kwa hiyo changamoto ni ukosefu wa ufikiaji wa taarifa za masoko, kwasababu hatujafungamanisha Sekta ya Kilimo na Teknolojia

Ili tupunguze tatizo la Ajira nchini ni lazima tuwekeze kwenye Kilimo cha Kisasa

Kuwekeza kwenye Kilimo cha Biashara

Dickson Kamala, Mwakilishi wa Kundi la Vijana
Kwa nchi kama Tanzania ni kama bado hatujawa Serious kuona kama ukosefu wa ajira ni changamoto

Ukweli ni kwamba hali mtaani ni mbaya sana

Sekta ya Viwanda vya Uzalishaji kama SIDO ingeweza kupunguza tatizo la ajira nchini lakini kwa sasa tuna tunaingiza mapanga, mikuki na mashoka wakati zamani yalitengenezwa hapa hapa

Sasa kama tutaingiza hata majembe, wale Vijana pale SIDO Watakuwa na kazi gani?

Kama taifa tulipaswa kuwa na Sera Mbadala kuona ni kwa namna gani VETA na SIDO itatuokoa na tatizo la Ajira

Ukienda pale Kariakoo bidhaa nyingi zinatoka nje. Fedha yote ikitumika kuagiza bidhaa nje lazima uchumi uyumbe

Ukiangalia hizi takwimu za Wizara ya Fedha, kuna sehemu kama Taifa tulikwama

Na tunahitaji Mjadala wa Kitaifa wa kuelezana ukweli kwamba kuna sehemu tulikosea na tunaweza kurekebisha

Deo Sabokwigina - Mkurugenzi wa Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu (Chuo Kikuu cha Iringa)
Ni kweli kwamba ukiongea na Wahitimu wengi wanalalamika hawana ajira lakini pia ukiongea na Waajiri wanalalamika hawapati Vijana wenye Maarifa na Ujuzi wanaouhitaji

Mfumo wa Elimu kuanzia ngazi ya Msingi unaawaandaa wahitumu Kuajiriwa

Mfumo hauwaandai kuwa unaweza ukakosa na ukapaswa kuajiriwa, kwa hiyo mtu anasoma akijua atakuja kuvaa suti na kuajiriwa kwenye Ofisi za Watu

Vijana wengi wanahitimu huku hawana maarifa na mtazamo wa kujiajiri au kuendesha biashara, hiyo inaitwa 'Business Skills Problem'. Tatizo lingine ni Uzoefu. Waajiri wanataka Uzoefu mfano Miaka Mitatu. Muda wote Kijana amesoma Nadharia, huo uzoefu anautoa wapi?

Mfumo unapaswa kumuandaa Mhitimu aweze kujiajiri. Apate 'business skills' Darasani Iifike sehemu elimu iwe kwa Vitendo. Wanafunzi waunganishwe na Wajasiriamali wanaofanya shughuli kama zao, kama sehemu ya elimu yao, wapate uzoefu

Kwenye kila programu ya Elimu wachomeke masomo ya Ujasiriamali Mfano, anayesomea Sheria apate elimu itayomwezesha kuwa Wakili wa Kujitegemea akimaliza Shule

Shukuru Amos, Mtaalamu wa Masoko ya Kiditali/ Mwanzilishi Tanzlite Digital
Hatujaishia tuu kununua bidhaa nje ya nchi lakini pia bado tumekuwa tunaingiza 'Knowledge Experts'Niliingia kwenye Digital Marketing baada ya kozi yangu niliyoisomea (Ualimu) kukosa Soko

Ukosefu wa Vituo vya Kujifunzia mafunzo ya Kidigitali au kozi ya Mtandaoni unawanyima Vijana fursa ya kutafuta fursa katika soko la kidigitaliKwasababu kujifunza unahitaji Vifaa, Internet n.k vitu ambavyo ni changamoto

Fursa za Ajira za Mtandaoni zipo wazi kwa wote lakini Watanzania wengi tunashindwa kuzichangamkia kwasababu bado tuko kama Kisiwa

Kama nchi tuna tatizo la mtazamo, tatizo la Branding. Kwa sababu hatutazamwi kama Kituo cha Uchumi wa KidigitaliSababu ni kama Sera na over protectionism, vitu ambavyo vinakwamisha Vijana ambao wameamua kujiajiriMchakato wa Kurasimisha ujasiriamali wa kidigitali (huko BRELA nk) bado ni mrefu sana

Sekta ya Uchumi wa Kidigitali bado haijarasimishwa sana nchiniSafari ya kujiajiri katika mambo ya kidigitali bado ni ngumu sana, bado ni msitu tunaoufyeka na bado hatujaanza kuneemeka

Vijana wengi tunaitumia Mitandao kama Burudani lakini kuna Vijana ambao wameanza kutumia mitandao kutengeneza na kukuza brand zao za kijasiriamali mfano MalemboFursa zipo Mtandaoni uwezeshwaji ukiwa mzuri, naamini huku kuna fursa kubwa changamoto ndio hizo gharama za mtandao nk

Naamini Mamlaka zetu hazijachukulia Mtandao kama dhana inayoweza kukomboa Uchumi wa Vijana Mambo kama haya yanakwamisha Vijana kuingia kwenye Uchumi wa Kidigitali

Chuoni kwetu tuna utaratibu wa kuwafanya Wanafunzi wajifunze kwa matendo, hawajifunzi kwa nadharia. Kama ni masuala ya fedha anayafanya kwa vitendo, hatufanyi masomo ya kufikirika

Uthubutu sio kitu rahisi, hii ni kwa mtu yeyote, kupata hasara ni jambo la kawaida. Mfano kuna Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza walithubutu kuanzisha biashara ya Vyakula vya Zanzibar, wakapata wateja wengi. Walipohama eneo na kwenda kupanga kwenye eneo kubwa zaidi na kuwekeza fedha nyingi, hawakupata wateja. Hiyo ni sehemu ya kuonesha uthubutu na wakianza kufanya hivyo kuanzia ngazi ya chuo, inawafunza ili wakihitimu wawe na uwelewa mzuri wa mazingira halisi ya biashara na ajira

Kilimo kinahitaji matumizi ya Teknolojia kwa kiwango kikubwa, mfano kuna Wakulima wanapata hasara kutokana na mabadiliko ya ArdhiKuna umuhimu wa Serikali kuingilia kati kusaidia Wakulima na kuwatengenezea njia sahihi

Asilimia 65 ya Vijana wanaotoka Vijijini kwenda Mijini wanaacha fursa ya Kilimo kutokana na mazingira kuwa changamoto na kutokuwa rafiki

Hatuwezi kufikia maendeleo ya Teknolojia kama hatujawekeza kuwawezesha Vijana katika kujiendeleza katika kilimoDuniani kwa jumla ardhi inayofaa kwa kilimo ipo Afrika, Tarifa za FAO zinaonesha Tanzania kuna eneo kubwa linalofaa kwa kilimo lakini hatujalitumia inavyostahili

Tukitengeneza Sera nzuri na mazingira mazuri, fedha nyingi zinazopelekwa nje zitabaki Nchini, kutakuwa na fursa nyingi Tanzania tupo katika Soko Huru la Biashara lakini tujiulize tunauza nini kwenye hilo soko?

Nisisitize Kijana jitathimini kuhusu ujuzi ulionao, unaweza kuutumia kwa faida ipiWazazi wangu hawakuamini katika kilimo, nilienda kwenye ajira nikaharibu makusudi, niliamini katika kilimo na nikawekeza katika kilimo. Ninafanya vitu vidogo vidogo ambavyo leo hii vimekuwa na faida kubwa kwangu na familia yangu

Nilisikia fursa ya ufugaji wa konokono, nikaenda kujifunza Nchi Jirani, niliporejea nikawekeza na sasa hivi ninafanya mambo makubwa katika kilimo cha Konokono. Acha kulalamika, chukua hatua sasa

MAONI YA WADAU WACHANGIAJI

Owek Dozi:
Ili kukabiliana na changamoto ya ajira tunatakiwa kuhakikisha Elimu inaendana na uhalisia wa mahitaji ya Jamii, Elimu inatakiwa kuwa na uwezo wa kubadilisha uwezo wa mmoja mmoja na inatakiwa kuendana na dhana za Kidigitali ilivyo kwa wakati husika

Mou Saliim: Kila mwaka kuna ingizo jipya la wenye uhitaji wa ajira, wale wanaopata ajira wanaweza kuchukua miaka hadi 25 kuacha ajira walizonazo, hiyo inaonesha kuna changamoto kubwa ya ushindani katika Soko la AjiraLicha ya kuwa soko linabadilika na mahitaji yanaongezeka, bado kuna changamoto kubwa katika Soko la Ajira la Kuajiriwa

Kuna fursa nyingi kwenye ajira mbali na zile za kuajiriwa, kuna mambo mengi ambayo hayajafanywa Nchini, unaweza kuangalia wenzetu wanafanya nini kisha wewe ukafanya kwa kuendana na mazingira yanayokuzunguka

Nikiwa mwekezaji, nimewekeza fedha nyingi katika mradi, ninahitaji faida, hivyo siwezi kusema nachukua mtu anayekuja kufanya majaribio, ndio maana watu wengi wanapenda kuajiri wale wenye uzoefu kwa kuwa misingi yetu ya elimu haitoe Elimu inayondana na soko lilivyoKuna watu wengi ambao wametoka chuo lakini wameshindwa kuwa na uwezo wa kuendana na soko, hiyo imesababisha Soko la Ajira lionekane gumu

Zuhura Seng'enge: Niliajiriwa katika nafasi ambayo haikuwa taaluma yangu, nilichofanya ni kuhamisha uelewa wa nilichojifunza huko nyuma na kufanya kilichopo mbele yangu, hiyo inamaanisha tunatakiwa kubadilika kulingana na uhalisia na sio kusubiri kilekile tulichokisomea ndicho tukifanyie kazi

Masanja Ng'hwenu: Nimesomea Clinical Medicine lakini kazi ambayo inanipa ulaji ni Fundi Umeme. Kuna Vijana wengi ambao unakuta kasoma masomo fulani akihitimu anawaza kuajiriwa na kuanza kujiuliza aelekee wapi? Inamaana hakujua mwelekeo wake?

Kuna umuhimu wa Serikali kuwekeza zaidi katika Elimu ya vitendo, mfano kufungua Chuo cha Veta kila Wilaya na mfano kilimo kikawa cha kwanza kupewa kipaumbele kwa vitendo, tutafikia wengiTukitegemea Chuo cha Sokoine pekee wanaokwenda kusoma ni wachache lakini VETA ikiwa kila Wilaya Ufundi na Elimu ya Vitendo itasaidia

Mfano Vijana walioajiriwa katika Ujenzi wa SGR, wanatakiwa kuwa na uelewa wa angalau kujenga Kalavati na sio kuwa vibarua pekee

ISMAILI MBOGO: Napendekeza muda wa kustaafu upunguzwe kutoka Miaka 60 hadi 35 au 40 ila kuwe na nyongeza ya mshahara, hiyo ni kusaidia wale wanaoingia katika Soko jipya la Ajira wapate nafasi
 
Wapunguze umri wa kustaafu from 60-50. Pia watengeneza mazingira rafiki vijana kupata hamasa ya kujiajiri mfano kuboresha secta ya kilimo, mawazir wawe active kuwatafutia vijana masoko ya mzao mbali mbali hata nje ya nchi.
 
Wapunguze baadhi ya Kodi ili wenye mitadi wakue/watajirike na kupata uwezo wakufungua miradi mipya (viwanda,nk ili kuajiri vijana. Lakini pia, wachipuke matajiri wengine wapya watakao ajiri. Kodi zikiwa nyingi, zina ua uchumi.

Ninavyo ona hadi leo tunataja matajiri waliojitokeza enzi ya Awamu ya pili (Mzee Ruhsa)

Elimu yetu inatakiwa ibadilishwe kabisa. Elimu yetu kuanzia Chekechea hadi Kidato cha Sita inalenga kutayarisha waajiriwa (watu wenye uwezo wa kukremu kwa ajili ya kutekeleza maagizo ya Boss) na maanisha hawajatayarishwa kutumia akili/kuja na mawazo yao wenyewe na ndio hao wamejaa mtaani.
 
Uwezeshaji wa mazingira ya kiuchumi kwa kila mkoa kulingana na shughuli za kiuchumi mkoa husika , yaani kila mkoa uwe na kipaumbe chake ..Sio watu kurundikana Dar na sasa naona mnapendelea Dodoma .

Kushuka kodi ili kuwa moyo wafanyabishara na taasisi binafsi.
 
Anza na self -investment maana hauwezi kuondoa tatizo la unemployment kwa kuwafanya watu kufatilia Connection , simba na yanga na Umbea tu 24/7

Ili watu wafikie hatua ya kujijajili na kufanikiwa lazima wawe conscious enough , disciplinary , kwa kila kitu

Ikiwemo pesa , muda n.k.

Self-investment ndo itazaa self-employment.

Ukiangalia kuna watu wamejiajiri way back Ila mpaka Leo wapo ktk movement na sio progress

Mikopo
Ajira za masaa
Kustaafu mapema

N.k yote haya yatafikiwa na kuleta matokeo ikiwa WATU wanajitambua na kujua wanahitaji nini in their life.
 
1. Wawekeze kwenye kuzalisha chuma. Chuma hutoa ajira nyingi sana, tena za pesa nzuri.
2. Wajenge irrigations schemes na kuwakatia watu plots. Siyo schemes kama zile za kisharobaro za Bashe, schemes za mitoni, mabwawani na maziwani, schemes za malaki au mamilioni ya ekari.
 
Ni maeneo gani ya Kiuchumi unadhani yanahitaji kufanyiwa Uwekezaji unaoweza kuzalisha Ajira nyingi nchini?

Shiriki kwa kutoa Mapendekezo katika Mjadala utakaofanyika kupitia X Spaces ya JamiiForums leo Julai 25, 2024 kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku

- Bofya hapa kutoa maoni yako

Mjadala.jpg
Mjadala 2.jpg

MICHANGO YA WAZUNGUMZAJI WAALIKWA

Malembo Lucas, Mkurungezi wa Malembo Farm/ Mshauri wa Kilimo Biashara

Umri wa Wastani wa Mkulima wa Tanzania ni Miaka 60, kwa Mujibu wa FAO, lakini nusu ya Watanzania ni Vijana

Vijana waliopo kwenye Sekta ya Kilimo ni wachache sana, sababu kubwa ni Mtazamo

Vijana wengi wana mtazamo hasi kuhusu Kilimo, Vijana wanaona Kilimo ni kazi ngumu au Adhabu

Sababu nyingine inayowafanya Vijana wasichangamkie Fursa za kilimo ni Mitaji. Vijana wengi hawana Mitaji

Kwenye Miaka ya 70 Mikopo ya Kilimo ilikuwa ni zaidi ya asilimia 30

Changamoto kubwa ni kuwa hatujafungamanisha Sekta ya Fedha na Kilimo hali inayosababisha Vijana kushindwa kupata usaidizi wa fedha za kuingia kwenye Kilimo

Muhimu ni kufungamanisha Sekta ya Kilimo na Sekta ya Fedha

Yaani kama Kijana ana andiko lake zuri kuhusu Kilimo aende akaliwasilishe Benki na aweze kukopesheka

Vijana wengi wanakosa Mikopo kwa kukosa dhamana

Tatizo lingine linalokwamisha Vijana kuingia kwenye Kilimo na Ufahamu na Ufikiaji wa Masoko

Mkulima ana mazao ila hajui auze wapi, na mnunuzi anataka bidhaa ila hajui anunue wapi

Kwa hiyo changamoto ni ukosefu wa ufikiaji wa taarifa za masoko, kwasababu hatujafungamanisha Sekta ya Kilimo na Teknolojia

Ili tupunguze tatizo la Ajira nchini ni lazima tuwekeze kwenye Kilimo cha Kisasa

Kuwekeza kwenye Kilimo cha Biashara

Dickson Kamala, Mwakilishi wa Kundi la Vijana
Kwa nchi kama Tanzania ni kama bado hatujawa Serious kuona kama ukosefu wa ajira ni changamoto

Ukweli ni kwamba hali mtaani ni mbaya sana

Sekta ya Viwanda vya Uzalishaji kama SIDO ingeweza kupunguza tatizo la ajira nchini lakini kwa sasa tuna tunaingiza mapanga, mikuki na mashoka wakati zamani yalitengenezwa hapa hapa

Sasa kama tutaingiza hata majembe, wale Vijana pale SIDO Watakuwa na kazi gani?

Kama taifa tulipaswa kuwa na Sera Mbadala kuona ni kwa namna gani VETA na SIDO itatuokoa na tatizo la Ajira

Ukienda pale Kariakoo bidhaa nyingi zinatoka nje. Fedha yote ikitumika kuagiza bidhaa nje lazima uchumi uyumbe

Ukiangalia hizi takwimu za Wizara ya Fedha, kuna sehemu kama Taifa tulikwama

Na tunahitaji Mjadala wa Kitaifa wa kuelezana ukweli kwamba kuna sehemu tulikosea na tunaweza kurekebisha

Deo Sabokwigina - Mkurugenzi wa Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu (Chuo Kikuu cha Iringa)
Ni kweli kwamba ukiongea na Wahitimu wengi wanalalamika hawana ajira lakini pia ukiongea na Waajiri wanalalamika hawapati Vijana wenye Maarifa na Ujuzi wanaouhitaji

Mfumo wa Elimu kuanzia ngazi ya Msingi unaawaandaa wahitumu Kuajiriwa

Mfumo hauwaandai kuwa unaweza ukakosa na ukapaswa kuajiriwa, kwa hiyo mtu anasoma akijua atakuja kuvaa suti na kuajiriwa kwenye Ofisi za Watu

Vijana wengi wanahitimu huku hawana maarifa na mtazamo wa kujiajiri au kuendesha biashara, hiyo inaitwa 'Business Skills Problem'. Tatizo lingine ni Uzoefu. Waajiri wanataka Uzoefu mfano Miaka Mitatu. Muda wote Kijana amesoma Nadharia, huo uzoefu anautoa wapi?

Mfumo unapaswa kumuandaa Mhitimu aweze kujiajiri. Apate 'business skills' Darasani Iifike sehemu elimu iwe kwa Vitendo. Wanafunzi waunganishwe na Wajasiriamali wanaofanya shughuli kama zao, kama sehemu ya elimu yao, wapate uzoefu

Kwenye kila programu ya Elimu wachomeke masomo ya Ujasiriamali Mfano, anayesomea Sheria apate elimu itayomwezesha kuwa Wakili wa Kujitegemea akimaliza Shule

Shukuru Amos, Mtaalamu wa Masoko ya Kiditali/ Mwanzilishi Tanzlite Digital
Hatujaishia tuu kununua bidhaa nje ya nchi lakini pia bado tumekuwa tunaingiza 'Knowledge Experts'Niliingia kwenye Digital Marketing baada ya kozi yangu niliyoisomea (Ualimu) kukosa Soko

Ukosefu wa Vituo vya Kujifunzia mafunzo ya Kidigitali au kozi ya Mtandaoni unawanyima Vijana fursa ya kutafuta fursa katika soko la kidigitaliKwasababu kujifunza unahitaji Vifaa, Internet n.k vitu ambavyo ni changamoto

Ukosefu wa Vituo vya Kujifunzia mafunzo ya Kidigitali au kozi ya Mtandaoni unawanyima Vijana fursa ya kutafuta fursa katika soko la kidigitaliKwasababu kujifunza unahitaji Vifaa, Internet n.k vitu ambavyo ni changamoto

Fursa za Ajira za Mtandaoni zipo wazi kwa wote lakini Watanzania wengi tunashindwa kuzichangamkia kwasababu bado tuko kama Kisiwa

Kama nchi tuna tatizo la mtazamo, tatizo la Branding. Kwa sababu hatutazamwi kama Kituo cha Uchumi wa KidigitaliSababu ni kama Sera na over protectionism, vitu ambavyo vinakwamisha Vijana ambao wameamua kujiajiriMchakato wa Kurasimisha ujasiriamali wa kidigitali (huko BRELA nk) bado ni mrefu sana

Sekta ya Uchumi wa Kidigitali bado haijarasimishwa sana nchiniSafari ya kujiajiri katika mambo ya kidigitali bado ni ngumu sana, bado ni msitu tunaoufyeka na bado hatujaanza kuneemeka

Vijana wengi tunaitumia Mitandao kama Burudani lakini kuna Vijana ambao wameanza kutumia mitandao kutengeneza na kukuza brand zao za kijasiriamali mfano MalemboFursa zipo Mtandaoni uwezeshwaji ukiwa mzuri, naamini huku kuna fursa kubwa changamoto ndio hizo gharama za mtandao nk

Naamini Mamlaka zetu hazijachukulia Mtandao kama dhana inayoweza kukomboa Uchumi wa Vijana Mambo kama haya yanakwamisha Vijana kuingia kwenye Uchumi wa Kidigitali

Deo Sabokwigina - Mkurugenzi wa Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu (Chuo Kikuu cha Iringa)
Chuoni kwetu tuna utaratibu wa kuwafanya Wanafunzi wajifunze kwa matendo, hawajifunzi kwa nadharia. Kama ni masuala ya fedha anayafanya kwa vitendo, hatufanyi masomo ya kufikirika

Uthubutu sio kitu rahisi, hii ni kwa mtu yeyote, kupata hasara ni jambo la kawaida. Mfano kuna Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza walithubutu kuanzisha biashara ya Vyakula vya Zanzibar, wakapata wateja wengi. Walipohama eneo na kwenda kupanga kwenye eneo kubwa zaidi na kuwekeza fedha nyingi, hawakupata wateja. Hiyo ni sehemu ya kuonesha uthubutu na wakianza kufanya hivyo kuanzia ngazi ya chuo, inawafunza ili wakihitimu wawe na uwelewa mzuri wa mazingira halisi ya biashara na ajira

Malembo Lucas, Mkurungezi wa Malembo Farm/ Mshauri wa Kilimo Biashara
Kilimo kinahitaji matumizi ya Teknolojia kwa kiwango kikubwa, mfano kuna Wakulima wanapata hasara kutokana na mabadiliko ya ArdhiKuna umuhimu wa Serikali kuingilia kati kusaidia Wakulima na kuwatengenezea njia sahihi

Asilimia 65 ya Vijana wanaotoka Vijijini kwenda Mijini wanaacha fursa ya Kilimo kutokana na mazingira kuwa changamoto na kutokuwa rafiki

Hatuwezi kufikia maendeleo ya Teknolojia kama hatujawekeza kuwawezesha Vijana katika kujiendeleza katika kilimoDuniani kwa jumla ardhi inayofaa kwa kilimo ipo Afrika, Tarifa za FAO zinaonesha Tanzania kuna eneo kubwa linalofaa kwa kilimo lakini hatujalitumia inavyostahili

Tukitengeneza Sera nzuri na mazingira mazuri, fedha nyingi zinazopelekwa nje zitabaki Nchini, kutakuwa na fursa nyingi Tanzania tupo katika Soko Huru la Biashara lakini tujiulize tunauza nini kwenye hilo soko?

MAONI YA WADAU WACHANGIAJI

Owek Dozi: Ili kukabiliana na changamoto ya ajira tunatakiwa kuhakikisha Elimu inaendana na uhalisia wa mahitaji ya Jamii, Elimu inatakiwa kuwa na uwezo wa kubadilisha uwezo wa mmoja mmoja na inatakiwa kuendana na dhana za Kidigitali ilivyo kwa wakati husika

Mou Saliim: Kila mwaka kuna ingizo jipya la wenye uhitaji wa ajira, wale wanaopata ajira wanaweza kuchukua miaka hadi 25 kuacha ajira walizonazo, hiyo inaonesha kuna changamoto kubwa ya ushindani katika Soko la AjiraLicha ya kuwa soko linabadilika na mahitaji yanaongezeka, bado kuna changamoto kubwa katika Soko la Ajira la Kuajiriwa

Kuna fursa nyingi kwenye ajira mbali na zile za kuajiriwa, kuna mambo mengi ambayo hayajafanywa Nchini, unaweza kuangalia wenzetu wanafanya nini kisha wewe ukafanya kwa kuendana na mazingira yanayokuzunguka

Nikiwa mwekezaji, nimewekeza fedha nyingi katika mradi, ninahitaji faida, hivyo siwezi kusema nachukua mtu anayekuja kufanya majaribio, ndio maana watu wengi wanapenda kuajiri wale wenye uzoefu kwa kuwa misingi yetu ya elimu haitoe Elimu inayondana na soko lilivyoKuna watu wengi ambao wametoka chuo lakini wameshindwa kuwa na uwezo wa kuendana na soko, hiyo imesababisha Soko la Ajira lionekane gumu

Zuhura Seng'enge: Niliajiriwa katika nafasi ambayo haikuwa taaluma yangu, nilichofanya ni kuhamisha uelewa wa nilichojifunza huko nyuma na kufanya kilichopo mbele yangu, hiyo inamaanisha tunatakiwa kubadilika kulingana na uhalisia na sio kusubiri kilekile tulichokisomea ndicho tukifanyie kazi

Masanja Ng'hwenu: Nimesomea Clinical Medicine lakini kazi ambayo inanipa ulaji ni Fundi Umeme. Kuna Vijana wengi ambao unakuta kasoma masomo fulani akihitimu anawaza kuajiriwa na kuanza kujiuliza aelekee wapi? Inamaana hakujua mwelekeo wake?

Kuna umuhimu wa Serikali kuwekeza zaidi katika Elimu ya vitendo, mfano kufungua Chuo cha Veta kila Wilaya na mfano kilimo kikawa cha kwanza kupewa kipaumbele kwa vitendo, tutafikia wengiTukitegemea Chuo cha Sokoine pekee wanaokwenda kusoma ni wachache lakini VETA ikiwa kila Wilaya Ufundi na Elimu ya Vitendo itasaidia

Mfano Vijana walioajiriwa katika Ujenzi wa SGR, wanatakiwa kuwa na uelewa wa angalau kujenga Kalavati na sio kuwa vibarua pekee

ISMAILI MBOGO: Napendekeza muda wa kustaafu upunguzwe kutoka Miaka 60 hadi 35 au 40 ila kuwe na nyongeza ya mshahara, hiyo ni kusaidia wale wanaoingia katika Soko jipya la Ajira wapate nafasi

-------------

Malembo Lucas (Mkurungezi wa Malembo Farm/ Mshauri wa Kilimo Biashara)
Nisisitize Kijana jitathimini kuhusu ujuzi ulionao, unaweza kuutumia kwa faida ipiWazazi wangu hawakuamini katika kilimo, nilienda kwenye ajira nikaharibu makusudi, niliamini katika kilimo na nikawekeza katika kilimo. Ninafanya vitu vidogo vidogo ambavyo leo hii vimekuwa na faida kubwa kwangu na familia yangu

Nilisikia fursa ya ufugaji wa konokono, nikaenda kujifunza Nchi Jirani, niliporejea nikawekeza na sasa hivi ninafanya mambo makubwa katika kilimo cha Konokono. Acha kulalamika, chukua hatua sasa
 
Hakuna uwekezaji mkubwa na wawekezaji wengi wanaweza kuja kuwekeza kama hatujaandaa soko,na hapa ni soko la ndani kwanza.

Soko la ndani litaandaliwa kwa kuwawezesha vijana kiuchumi hasa katika kilimo. Kilimo ni msingi wa mwanzo katika kuandaa Taifa katika uwekezaji wa viwanda na biashara kubwa,za kati na ndogondogo.

Hivyo,kwa maoni yangu,tuanze na kilimo kinachobeba watu wengi kwa kuboresha miundombinu,kurahisisha upatikanaji wa pembejeo bora hasa mbegu na zana za kilimo pamoja na masoko ya uhakika.

Kwenye masoko ya uhakika, serikali itilie mkazo kwa kuweka wataalamu wa masuala ya biashara za mazao ya kilimo pamoja na bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo na kiwe na vitengo katika idara za usalama wa Taifa katika kutafuta kukuza na kulinda masoko ya nje na ndani ya nchi ili kumnyanyua mkulima.

Wananchi hasa wakulima wakiwa na fedha,wawekezaji wa viwanda na watoa huduma mbalimbali kutoka mataifa makubwa kwa madogo watakuja kuwekeza kwenye nchi yetu.

Baada ya hapo,idadi ya wakulima itapunguzwa kwa kutengeneza wafanyakazi wa viwandani wengi kulingana na uwekezaji ili wazalishaji wa mazao ya kilimo wawe wachache na wapate faida kwa kile wanachozalisha.​
 
Ibueni kwanza wawekezaji wazawa ktk nyanja zote, mmeachia sana wageni wanashikilia uchumi kuna hatari kubwa mnaitengeneza!
 
Kwanza sehemu za mipaka ya nchi. Pili sera ya viwanda na miradi kuvunjwa sio kila viwanda na miradi kuwa sehemu moja inapelekea sehemu nyengine kushindwa kuwa eco economic system.

Tatu serikali kuacha ubinafsi wa wawekezaji na sera.

Leo kuna makampuni makubwa ambayo tukiruhusu waje kuwekeza hapa kwenye fursa tutapata. Sio mdalali nazungumzia kama makampuni ya treni japan. Makampuni yenye viwanda vikubwa.

Nne bado kuna tatizo viongozi kuwa wafanya biashara ili linapelekea kutotaka ushindani ndani ya nchi.
 
Tehama kuna Pesa nyingi sana mtandaoni zinazoliwa na wajuzi wachache wasiotaka kuwafundisha wengine.
 
Poor government ideology

Dunia ipo Kasi sana serikal ya tz inashindwa kwendana na hii kasi ivo tupo nyuma ya mda now tupo Karne ya 21 lakn mwenendo wa serikal Bado upo Karne ya 19.

Viongoz mizigo wasio na maono pia ni tatizo ktk nchi,.

Rushwa,ufisadi Bado ni tatizo sugu ktk nchi, Hela nyingi zinakopwa lakin mianya ya upogaji ni mikubwa san
 
Back
Top Bottom