uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 17,060
- 32,400
Ni maeneo gani ya Kiuchumi unadhani yanahitaji kufanyiwa Uwekezaji unaoweza kuzalisha Ajira nyingi nchini?
Shiriki kwa kutoa Mapendekezo katika Mjadala utakaofanyika kupitia X Spaces ya JamiiForums leo Julai 25, 2024 kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku
- Bofya hapa kutoa maoni yako
UPDATES
Malembo Lucas, Mkurungezi wa Malembo Farm/ Mshauri wa Kilimo Biashara
Umri wa Wastani wa Mkulima wa Tanzania ni Miaka 60, kwa Mujibu wa FAO, lakini nusu ya Watanzania ni Vijana
Vijana waliopo kwenye Sekta ya Kilimo ni wachache sana, sababu kubwa ni Mtazamo
Vijana wengi wana mtazamo hasi kuhusu Kilimo, Vijana wanaona Kilimo ni kazi ngumu au Adhabu
Sababu nyingine inayowafanya Vijana wasichangamkie Fursa za kilimo ni Mitaji. Vijana wengi hawana Mitaji
Kwenye Miaka ya 70 Mikopo ya Kilimo ilikuwa ni zaidi ya asilimia 30
Changamoto kubwa ni kuwa hatujafungamanisha Sekta ya Fedha na Kilimo hali inayosababisha Vijana kushindwa kupata usaidizi wa fedha za kuingia kwenye Kilimo
Muhimu ni kufungamanisha Sekta ya Kilimo na Sekta ya Fedha
Yaani kama Kijana ana andiko lake zuri kuhusu Kilimo aende akaliwasilishe Benki na aweze kukopesheka
Vijana wengi wanakosa Mikopo kwa kukosa dhamana
Tatizo lingine linalokwamisha Vijana kuingia kwenye Kilimo na Ufahamu na Ufikiaji wa Masoko
Mkulima ana mazao ila hajui auze wapi, na mnunuzi anataka bidhaa ila hajui anunue wapi
Kwa hiyo changamoto ni ukosefu wa ufikiaji wa taarifa za masoko, kwasababu hatujafungamanisha Sekta ya Kilimo na Teknolojia
Ili tupunguze tatizo la Ajira nchini ni lazima tuwekeze kwenye Kilimo cha Kisasa
Kuwekeza kwenye Kilimo cha Biashara
Dickson Kamala, Mwakilishi wa Kundi la Vijana
Kwa nchi kama Tanzania ni kama bado hatujawa Serious kuona kama ukosefu wa ajira ni changamoto
Ukweli ni kwamba hali mtaani ni mbaya sana
Sekta ya Viwanda vya Uzalishaji kama SIDO ingeweza kupunguza tatizo la ajira nchini lakini kwa sasa tuna tunaingiza mapanga, mikuki na mashoka wakati zamani yalitengenezwa hapa hapa
Sasa kama tutaingiza hata majembe, wale Vijana pale SIDO Watakuwa na kazi gani?
Kama taifa tulipaswa kuwa na Sera Mbadala kuona ni kwa namna gani VETA na SIDO itatuokoa na tatizo la Ajira
Ukienda pale Kariakoo bidhaa nyingi zinatoka nje. Fedha yote ikitumika kuagiza bidhaa nje lazima uchumi uyumbe
Ukiangalia hizi takwimu za Wizara ya Fedha, kuna sehemu kama Taifa tulikwama
Na tunahitaji Mjadala wa Kitaifa wa kuelezana ukweli kwamba kuna sehemu tulikosea na tunaweza kurekebisha
Deo Sabokwigina - Mkurugenzi wa Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu (Chuo Kikuu cha Iringa)
Ni kweli kwamba ukiongea na Wahitimu wengi wanalalamika hawana ajira lakini pia ukiongea na Waajiri wanalalamika hawapati Vijana wenye Maarifa na Ujuzi wanaouhitaji
Mfumo wa Elimu kuanzia ngazi ya Msingi unaawaandaa wahitumu Kuajiriwa
Mfumo hauwaandai kuwa unaweza ukakosa na ukapaswa kuajiriwa, kwa hiyo mtu anasoma akijua atakuja kuvaa suti na kuajiriwa kwenye Ofisi za Watu
Vijana wengi wanahitimu huku hawana maarifa na mtazamo wa kujiajiri au kuendesha biashara, hiyo inaitwa 'Business Skills Problem'. Tatizo lingine ni Uzoefu. Waajiri wanataka Uzoefu mfano Miaka Mitatu. Muda wote Kijana amesoma Nadharia, huo uzoefu anautoa wapi?
Mfumo unapaswa kumuandaa Mhitimu aweze kujiajiri. Apate 'business skills' Darasani Iifike sehemu elimu iwe kwa Vitendo. Wanafunzi waunganishwe na Wajasiriamali wanaofanya shughuli kama zao, kama sehemu ya elimu yao, wapate uzoefu
Kwenye kila programu ya Elimu wachomeke masomo ya Ujasiriamali Mfano, anayesomea Sheria apate elimu itayomwezesha kuwa Wakili wa Kujitegemea akimaliza Shule
Shukuru Amos, Mtaalamu wa Masoko ya Kiditali/ Mwanzilishi Tanzlite Digital
Hatujaishia tuu kununua bidhaa nje ya nchi lakini pia bado tumekuwa tunaingiza 'Knowledge Experts'Niliingia kwenye Digital Marketing baada ya kozi yangu niliyoisomea (Ualimu) kukosa Soko
Ukosefu wa Vituo vya Kujifunzia mafunzo ya Kidigitali au kozi ya Mtandaoni unawanyima Vijana fursa ya kutafuta fursa katika soko la kidigitaliKwasababu kujifunza unahitaji Vifaa, Internet n.k vitu ambavyo ni changamoto
Ukosefu wa Vituo vya Kujifunzia mafunzo ya Kidigitali au kozi ya Mtandaoni unawanyima Vijana fursa ya kutafuta fursa katika soko la kidigitaliKwasababu kujifunza unahitaji Vifaa, Internet n.k vitu ambavyo ni changamoto
Fursa za Ajira za Mtandaoni zipo wazi kwa wote lakini Watanzania wengi tunashindwa kuzichangamkia kwasababu bado tuko kama Kisiwa
Kama nchi tuna tatizo la mtazamo, tatizo la Branding. Kwa sababu hatutazamwi kama Kituo cha Uchumi wa KidigitaliSababu ni kama Sera na over protectionism, vitu ambavyo vinakwamisha Vijana ambao wameamua kujiajiriMchakato wa Kurasimisha ujasiriamali wa kidigitali (huko BRELA nk) bado ni mrefu sana
Sekta ya Uchumi wa Kidigitali bado haijarasimishwa sana nchiniSafari ya kujiajiri katika mambo ya kidigitali bado ni ngumu sana, bado ni msitu tunaoufyeka na bado hatujaanza kuneemeka
Vijana wengi tunaitumia Mitandao kama Burudani lakini kuna Vijana ambao wameanza kutumia mitandao kutengeneza na kukuza brand zao za kijasiriamali mfano MalemboFursa zipo Mtandaoni uwezeshwaji ukiwa mzuri, naamini huku kuna fursa kubwa changamoto ndio hizo gharama za mtandao nk
Naamini Mamlaka zetu hazijachukulia Mtandao kama dhana inayoweza kukomboa Uchumi wa Vijana Mambo kama haya yanakwamisha Vijana kuingia kwenye Uchumi wa Kidigitali
Hakuna