MJADALA: Je, unapendekeza Serikali na Sekta Binafsi zifanye nini cha tofauti ili kuondoa tatizo la ajira nchini?

MJADALA: Je, unapendekeza Serikali na Sekta Binafsi zifanye nini cha tofauti ili kuondoa tatizo la ajira nchini?

Ni maeneo gani ya Kiuchumi unadhani yanahitaji kufanyiwa Uwekezaji unaoweza kuzalisha Ajira nyingi nchini?

Shiriki kwa kutoa Mapendekezo katika Mjadala utakaofanyika kupitia X Spaces ya JamiiForums leo Julai 25, 2024 kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku

- Bofya hapa kutoa maoni yako

UPDATES

Malembo Lucas, Mkurungezi wa Malembo Farm/ Mshauri wa Kilimo Biashara

Umri wa Wastani wa Mkulima wa Tanzania ni Miaka 60, kwa Mujibu wa FAO, lakini nusu ya Watanzania ni Vijana

Vijana waliopo kwenye Sekta ya Kilimo ni wachache sana, sababu kubwa ni Mtazamo

Vijana wengi wana mtazamo hasi kuhusu Kilimo, Vijana wanaona Kilimo ni kazi ngumu au Adhabu

Sababu nyingine inayowafanya Vijana wasichangamkie Fursa za kilimo ni Mitaji. Vijana wengi hawana Mitaji

Kwenye Miaka ya 70 Mikopo ya Kilimo ilikuwa ni zaidi ya asilimia 30

Changamoto kubwa ni kuwa hatujafungamanisha Sekta ya Fedha na Kilimo hali inayosababisha Vijana kushindwa kupata usaidizi wa fedha za kuingia kwenye Kilimo

Muhimu ni kufungamanisha Sekta ya Kilimo na Sekta ya Fedha

Yaani kama Kijana ana andiko lake zuri kuhusu Kilimo aende akaliwasilishe Benki na aweze kukopesheka

Vijana wengi wanakosa Mikopo kwa kukosa dhamana

Tatizo lingine linalokwamisha Vijana kuingia kwenye Kilimo na Ufahamu na Ufikiaji wa Masoko

Mkulima ana mazao ila hajui auze wapi, na mnunuzi anataka bidhaa ila hajui anunue wapi

Kwa hiyo changamoto ni ukosefu wa ufikiaji wa taarifa za masoko, kwasababu hatujafungamanisha Sekta ya Kilimo na Teknolojia

Ili tupunguze tatizo la Ajira nchini ni lazima tuwekeze kwenye Kilimo cha Kisasa

Kuwekeza kwenye Kilimo cha Biashara

Dickson Kamala, Mwakilishi wa Kundi la Vijana
Kwa nchi kama Tanzania ni kama bado hatujawa Serious kuona kama ukosefu wa ajira ni changamoto

Ukweli ni kwamba hali mtaani ni mbaya sana

Sekta ya Viwanda vya Uzalishaji kama SIDO ingeweza kupunguza tatizo la ajira nchini lakini kwa sasa tuna tunaingiza mapanga, mikuki na mashoka wakati zamani yalitengenezwa hapa hapa

Sasa kama tutaingiza hata majembe, wale Vijana pale SIDO Watakuwa na kazi gani?

Kama taifa tulipaswa kuwa na Sera Mbadala kuona ni kwa namna gani VETA na SIDO itatuokoa na tatizo la Ajira

Ukienda pale Kariakoo bidhaa nyingi zinatoka nje. Fedha yote ikitumika kuagiza bidhaa nje lazima uchumi uyumbe

Ukiangalia hizi takwimu za Wizara ya Fedha, kuna sehemu kama Taifa tulikwama

Na tunahitaji Mjadala wa Kitaifa wa kuelezana ukweli kwamba kuna sehemu tulikosea na tunaweza kurekebisha

Deo Sabokwigina - Mkurugenzi wa Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu (Chuo Kikuu cha Iringa)
Ni kweli kwamba ukiongea na Wahitimu wengi wanalalamika hawana ajira lakini pia ukiongea na Waajiri wanalalamika hawapati Vijana wenye Maarifa na Ujuzi wanaouhitaji

Mfumo wa Elimu kuanzia ngazi ya Msingi unaawaandaa wahitumu Kuajiriwa

Mfumo hauwaandai kuwa unaweza ukakosa na ukapaswa kuajiriwa, kwa hiyo mtu anasoma akijua atakuja kuvaa suti na kuajiriwa kwenye Ofisi za Watu

Vijana wengi wanahitimu huku hawana maarifa na mtazamo wa kujiajiri au kuendesha biashara, hiyo inaitwa 'Business Skills Problem'. Tatizo lingine ni Uzoefu. Waajiri wanataka Uzoefu mfano Miaka Mitatu. Muda wote Kijana amesoma Nadharia, huo uzoefu anautoa wapi?

Mfumo unapaswa kumuandaa Mhitimu aweze kujiajiri. Apate 'business skills' Darasani Iifike sehemu elimu iwe kwa Vitendo. Wanafunzi waunganishwe na Wajasiriamali wanaofanya shughuli kama zao, kama sehemu ya elimu yao, wapate uzoefu

Kwenye kila programu ya Elimu wachomeke masomo ya Ujasiriamali Mfano, anayesomea Sheria apate elimu itayomwezesha kuwa Wakili wa Kujitegemea akimaliza Shule

Shukuru Amos, Mtaalamu wa Masoko ya Kiditali/ Mwanzilishi Tanzlite Digital
Hatujaishia tuu kununua bidhaa nje ya nchi lakini pia bado tumekuwa tunaingiza 'Knowledge Experts'Niliingia kwenye Digital Marketing baada ya kozi yangu niliyoisomea (Ualimu) kukosa Soko

Ukosefu wa Vituo vya Kujifunzia mafunzo ya Kidigitali au kozi ya Mtandaoni unawanyima Vijana fursa ya kutafuta fursa katika soko la kidigitaliKwasababu kujifunza unahitaji Vifaa, Internet n.k vitu ambavyo ni changamoto

Fursa za Ajira za Mtandaoni zipo wazi kwa wote lakini Watanzania wengi tunashindwa kuzichangamkia kwasababu bado tuko kama Kisiwa

Kama nchi tuna tatizo la mtazamo, tatizo la Branding. Kwa sababu hatutazamwi kama Kituo cha Uchumi wa KidigitaliSababu ni kama Sera na over protectionism, vitu ambavyo vinakwamisha Vijana ambao wameamua kujiajiriMchakato wa Kurasimisha ujasiriamali wa kidigitali (huko BRELA nk) bado ni mrefu sana

Sekta ya Uchumi wa Kidigitali bado haijarasimishwa sana nchiniSafari ya kujiajiri katika mambo ya kidigitali bado ni ngumu sana, bado ni msitu tunaoufyeka na bado hatujaanza kuneemeka

Vijana wengi tunaitumia Mitandao kama Burudani lakini kuna Vijana ambao wameanza kutumia mitandao kutengeneza na kukuza brand zao za kijasiriamali mfano MalemboFursa zipo Mtandaoni uwezeshwaji ukiwa mzuri, naamini huku kuna fursa kubwa changamoto ndio hizo gharama za mtandao nk

Naamini Mamlaka zetu hazijachukulia Mtandao kama dhana inayoweza kukomboa Uchumi wa Vijana Mambo kama haya yanakwamisha Vijana kuingia kwenye Uchumi wa Kidigitali

Hakuna
 
Mada kama hizi huwezi kukuta wana jf wanachangia sana, inaonyesha kabisa watz wana vipaumbele gani

Mzee mzima Dr Restart yupo uzi wa kula tunda kimasihara huu anafanya hajauona
Acha ubogus.

Nilikuwa live X. Na nilipata nafasi ya kuchangia. Baadae space ikashuka.

Sikujoin tena.

Tatizo unadhani wote marue rue kama wewe.
 
Kilimo biashara, kwa maoni yangu na ujuzi mdogo nilioupata katika biashara ya mazao, nimetambua kuwa kilimo kinalipa isipokuwa miundombinu ya kilimo ndiyo siyo rafiki. Wakulima wetu hawathaminiwi ili hali ndiyo wanaolisha taifa, sababu ya kutokuthaminiwa kwa wakulima kunafanya hata vijana wasio na ajira waone ukulima ni sawa na kazi ya kimaskini.

Hali hii imejenga dhana kiasi kwamba hata mkulima mwenyewe haoni sababu yoyote ya kumridhisha mwanae kazi ya kilimo. Hii pia imechangiwa na ukosefu wa elimu juu ya kilimo.

Ukosefu wa mtaji katika kilimo pia ni tatizo. Linalofanya vijana wengi washindwe kuingia katika kilimo (kilimo kinahitaji mtu ambaye tayari yupo stable kiuchumi, ama ana biashara nyingine inayomuingizia kipato)
Tanzania tumezungukwa na mataifa ambayo kama tungewekeza katika kilimo, nina uhakika vijana wengi kusingekuwa tunalalamika juu ya ukosefu wa ajira.

Malawi ukame, Zambia hawana ndizi tamu kama za Tukuyu, kiasi kwamba ukipeleka ndizi uhakika wa soko upo changamoto nyingine ni mlolongo wa vibali, rushwa na kodi pamoja na utitiri wa ushuru. Hizi changamoto zinakatisha tamaa.
 
Masoko ya uhakika yanayotoa thamani halisi ya jasho la mzalishaji husika.

Na pia muangalie watu wasipate togauti na thamani wanayoileta kwa Taifa. Mfano kumpatia mtu fulani (mwanasiasa/muajiriwa whatever) posho iliyozidi thamani anayoitoa kwa jamii nao ni UTAKATISHAJI FEDHA na UHUJUMU.

Kila mtu alipwe kwa haki thamani halisi ya kazi yake, hapo ndio uchumi utatengemaa
 
Ni maeneo gani ya Kiuchumi unadhani yanahitaji kufanyiwa Uwekezaji unaoweza kuzalisha Ajira nyingi nchini?

Shiriki kwa kutoa Mapendekezo katika Mjadala utakaofanyika kupitia X Spaces ya JamiiForums leo Julai 25, 2024 kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku

- Bofya hapa kutoa maoni yako

MICHANGO YA WAZUNGUMZAJI WAALIKWA

Malembo Lucas, Mkurungezi wa Malembo Farm/ Mshauri wa Kilimo Biashara

Umri wa Wastani wa Mkulima wa Tanzania ni Miaka 60, kwa Mujibu wa FAO, lakini nusu ya Watanzania ni Vijana

Vijana waliopo kwenye Sekta ya Kilimo ni wachache sana, sababu kubwa ni Mtazamo

Vijana wengi wana mtazamo hasi kuhusu Kilimo, Vijana wanaona Kilimo ni kazi ngumu au Adhabu

Sababu nyingine inayowafanya Vijana wasichangamkie Fursa za kilimo ni Mitaji. Vijana wengi hawana Mitaji

Kwenye Miaka ya 70 Mikopo ya Kilimo ilikuwa ni zaidi ya asilimia 30

Changamoto kubwa ni kuwa hatujafungamanisha Sekta ya Fedha na Kilimo hali inayosababisha Vijana kushindwa kupata usaidizi wa fedha za kuingia kwenye Kilimo

Muhimu ni kufungamanisha Sekta ya Kilimo na Sekta ya Fedha

Yaani kama Kijana ana andiko lake zuri kuhusu Kilimo aende akaliwasilishe Benki na aweze kukopesheka

Vijana wengi wanakosa Mikopo kwa kukosa dhamana

Tatizo lingine linalokwamisha Vijana kuingia kwenye Kilimo na Ufahamu na Ufikiaji wa Masoko

Mkulima ana mazao ila hajui auze wapi, na mnunuzi anataka bidhaa ila hajui anunue wapi

Kwa hiyo changamoto ni ukosefu wa ufikiaji wa taarifa za masoko, kwasababu hatujafungamanisha Sekta ya Kilimo na Teknolojia

Ili tupunguze tatizo la Ajira nchini ni lazima tuwekeze kwenye Kilimo cha Kisasa

Kuwekeza kwenye Kilimo cha Biashara

Dickson Kamala, Mwakilishi wa Kundi la Vijana
Kwa nchi kama Tanzania ni kama bado hatujawa Serious kuona kama ukosefu wa ajira ni changamoto

Ukweli ni kwamba hali mtaani ni mbaya sana

Sekta ya Viwanda vya Uzalishaji kama SIDO ingeweza kupunguza tatizo la ajira nchini lakini kwa sasa tuna tunaingiza mapanga, mikuki na mashoka wakati zamani yalitengenezwa hapa hapa

Sasa kama tutaingiza hata majembe, wale Vijana pale SIDO Watakuwa na kazi gani?

Kama taifa tulipaswa kuwa na Sera Mbadala kuona ni kwa namna gani VETA na SIDO itatuokoa na tatizo la Ajira

Ukienda pale Kariakoo bidhaa nyingi zinatoka nje. Fedha yote ikitumika kuagiza bidhaa nje lazima uchumi uyumbe

Ukiangalia hizi takwimu za Wizara ya Fedha, kuna sehemu kama Taifa tulikwama

Na tunahitaji Mjadala wa Kitaifa wa kuelezana ukweli kwamba kuna sehemu tulikosea na tunaweza kurekebisha

Deo Sabokwigina - Mkurugenzi wa Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu (Chuo Kikuu cha Iringa)
Ni kweli kwamba ukiongea na Wahitimu wengi wanalalamika hawana ajira lakini pia ukiongea na Waajiri wanalalamika hawapati Vijana wenye Maarifa na Ujuzi wanaouhitaji

Mfumo wa Elimu kuanzia ngazi ya Msingi unaawaandaa wahitumu Kuajiriwa

Mfumo hauwaandai kuwa unaweza ukakosa na ukapaswa kuajiriwa, kwa hiyo mtu anasoma akijua atakuja kuvaa suti na kuajiriwa kwenye Ofisi za Watu

Vijana wengi wanahitimu huku hawana maarifa na mtazamo wa kujiajiri au kuendesha biashara, hiyo inaitwa 'Business Skills Problem'. Tatizo lingine ni Uzoefu. Waajiri wanataka Uzoefu mfano Miaka Mitatu. Muda wote Kijana amesoma Nadharia, huo uzoefu anautoa wapi?

Mfumo unapaswa kumuandaa Mhitimu aweze kujiajiri. Apate 'business skills' Darasani Iifike sehemu elimu iwe kwa Vitendo. Wanafunzi waunganishwe na Wajasiriamali wanaofanya shughuli kama zao, kama sehemu ya elimu yao, wapate uzoefu

Kwenye kila programu ya Elimu wachomeke masomo ya Ujasiriamali Mfano, anayesomea Sheria apate elimu itayomwezesha kuwa Wakili wa Kujitegemea akimaliza Shule

Shukuru Amos, Mtaalamu wa Masoko ya Kiditali/ Mwanzilishi Tanzlite Digital
Hatujaishia tuu kununua bidhaa nje ya nchi lakini pia bado tumekuwa tunaingiza 'Knowledge Experts'Niliingia kwenye Digital Marketing baada ya kozi yangu niliyoisomea (Ualimu) kukosa Soko

Ukosefu wa Vituo vya Kujifunzia mafunzo ya Kidigitali au kozi ya Mtandaoni unawanyima Vijana fursa ya kutafuta fursa katika soko la kidigitaliKwasababu kujifunza unahitaji Vifaa, Internet n.k vitu ambavyo ni changamoto

Ukosefu wa Vituo vya Kujifunzia mafunzo ya Kidigitali au kozi ya Mtandaoni unawanyima Vijana fursa ya kutafuta fursa katika soko la kidigitaliKwasababu kujifunza unahitaji Vifaa, Internet n.k vitu ambavyo ni changamoto

Fursa za Ajira za Mtandaoni zipo wazi kwa wote lakini Watanzania wengi tunashindwa kuzichangamkia kwasababu bado tuko kama Kisiwa

Kama nchi tuna tatizo la mtazamo, tatizo la Branding. Kwa sababu hatutazamwi kama Kituo cha Uchumi wa KidigitaliSababu ni kama Sera na over protectionism, vitu ambavyo vinakwamisha Vijana ambao wameamua kujiajiriMchakato wa Kurasimisha ujasiriamali wa kidigitali (huko BRELA nk) bado ni mrefu sana

Sekta ya Uchumi wa Kidigitali bado haijarasimishwa sana nchiniSafari ya kujiajiri katika mambo ya kidigitali bado ni ngumu sana, bado ni msitu tunaoufyeka na bado hatujaanza kuneemeka

Vijana wengi tunaitumia Mitandao kama Burudani lakini kuna Vijana ambao wameanza kutumia mitandao kutengeneza na kukuza brand zao za kijasiriamali mfano MalemboFursa zipo Mtandaoni uwezeshwaji ukiwa mzuri, naamini huku kuna fursa kubwa changamoto ndio hizo gharama za mtandao nk

Naamini Mamlaka zetu hazijachukulia Mtandao kama dhana inayoweza kukomboa Uchumi wa Vijana Mambo kama haya yanakwamisha Vijana kuingia kwenye Uchumi wa Kidigitali

Deo Sabokwigina - Mkurugenzi wa Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu (Chuo Kikuu cha Iringa)
Chuoni kwetu tuna utaratibu wa kuwafanya Wanafunzi wajifunze kwa matendo, hawajifunzi kwa nadharia. Kama ni masuala ya fedha anayafanya kwa vitendo, hatufanyi masomo ya kufikirika

Uthubutu sio kitu rahisi, hii ni kwa mtu yeyote, kupata hasara ni jambo la kawaida. Mfano kuna Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza walithubutu kuanzisha biashara ya Vyakula vya Zanzibar, wakapata wateja wengi. Walipohama eneo na kwenda kupanga kwenye eneo kubwa zaidi na kuwekeza fedha nyingi, hawakupata wateja. Hiyo ni sehemu ya kuonesha uthubutu na wakianza kufanya hivyo kuanzia ngazi ya chuo, inawafunza ili wakihitimu wawe na uwelewa mzuri wa mazingira halisi ya biashara na ajira

Malembo Lucas, Mkurungezi wa Malembo Farm/ Mshauri wa Kilimo Biashara
Kilimo kinahitaji matumizi ya Teknolojia kwa kiwango kikubwa, mfano kuna Wakulima wanapata hasara kutokana na mabadiliko ya ArdhiKuna umuhimu wa Serikali kuingilia kati kusaidia Wakulima na kuwatengenezea njia sahihi

Asilimia 65 ya Vijana wanaotoka Vijijini kwenda Mijini wanaacha fursa ya Kilimo kutokana na mazingira kuwa changamoto na kutokuwa rafiki

Hatuwezi kufikia maendeleo ya Teknolojia kama hatujawekeza kuwawezesha Vijana katika kujiendeleza katika kilimoDuniani kwa jumla ardhi inayofaa kwa kilimo ipo Afrika, Tarifa za FAO zinaonesha Tanzania kuna eneo kubwa linalofaa kwa kilimo lakini hatujalitumia inavyostahili

Tukitengeneza Sera nzuri na mazingira mazuri, fedha nyingi zinazopelekwa nje zitabaki Nchini, kutakuwa na fursa nyingi Tanzania tupo katika Soko Huru la Biashara lakini tujiulize tunauza nini kwenye hilo soko?

MAONI YA WADAU WACHANGIAJI

Owek Dozi: Ili kukabiliana na changamoto ya ajira tunatakiwa kuhakikisha Elimu inaendana na uhalisia wa mahitaji ya Jamii, Elimu inatakiwa kuwa na uwezo wa kubadilisha uwezo wa mmoja mmoja na inatakiwa kuendana na dhana za Kidigitali ilivyo kwa wakati husika

Mou Saliim: Kila mwaka kuna ingizo jipya la wenye uhitaji wa ajira, wale wanaopata ajira wanaweza kuchukua miaka hadi 25 kuacha ajira walizonazo, hiyo inaonesha kuna changamoto kubwa ya ushindani katika Soko la AjiraLicha ya kuwa soko linabadilika na mahitaji yanaongezeka, bado kuna changamoto kubwa katika Soko la Ajira la Kuajiriwa

Kuna fursa nyingi kwenye ajira mbali na zile za kuajiriwa, kuna mambo mengi ambayo hayajafanywa Nchini, unaweza kuangalia wenzetu wanafanya nini kisha wewe ukafanya kwa kuendana na mazingira yanayokuzunguka

Nikiwa mwekezaji, nimewekeza fedha nyingi katika mradi, ninahitaji faida, hivyo siwezi kusema nachukua mtu anayekuja kufanya majaribio, ndio maana watu wengi wanapenda kuajiri wale wenye uzoefu kwa kuwa misingi yetu ya elimu haitoe Elimu inayondana na soko lilivyoKuna watu wengi ambao wametoka chuo lakini wameshindwa kuwa na uwezo wa kuendana na soko, hiyo imesababisha Soko la Ajira lionekane gumu
Nasikitika hii kitu nimeikosa kwanini JF hamkuiweka hewani mapema watu tushiriki!
 
Tubadili mfumo wetu wa Elimu, uendana na dunia ilipo, hii ndilo jambo la kwanza ili Kwanza tuzarishe skilled work force, tuhakikishe kila taaluma inaendana na wakati tuliopo.

Elimu ya form five na six ifutwe na baadala yake vijana wetu akimaliza form four waende college moja kwa moja miaka 3, kama mwanasheria akapate diploma ya Sheria, kama mhasibu akapate diploma ya uhasibu, kama ni engineer akapate diploma ya engineering, kama mwalimu basi akapate diploma ya ualimu nk.
Watakaofaulu hapo ndio waendelee na Elimu ya juu Kwa maana ya degree.

Hapo kwenye diploma, engineering and technology iwe ni special case, na wanaohitimu kwenye ufaulu wa kawaida kwenye engineering and technology wapewe scholarship wakasome short courses za mwaka mmoja mmoja kwenye area ambazo tutazifocus kwenye nchi kama China, Korea, Ujerumani na USA, tujitahidi walau kila mwaka waende vijana kama 300 kwenye program ya miaka hata 20.

Hii skilled workforce ikishakuwa kubwa maana yake vijana watajikita kwenye production zaidi na sio uchuuzi, maana yake pia watatoa ajira nyingi Kwa wenzao mitaani na kuongeza exportation ya bidhaa za mikono na kuacha kutegemea China, India, Pakistani nk.

Skilled workforce inayoendana na technolojia ya kisasa ikishakuwa kubwa maana yake pia wengi watakuwa na uwezo wa kwenda kujitafutia kazi huku na kule duniani.

JWTZ lianzishe production industries kwa ajili ya kutengeneza silaha kama bunduki, tanks, simple military vehicles, artillery, patrol boats, matractors, power tillers nk, kupitia hii program yakudevoloped skilled workforce kubwa maana yake JWTZ itabidi iajili vijana wengi Kwa ajili ya kurun hivi viwanda na kuexport silaha na nyingine zibaki kwa matumizi ya ndani.

JWTZ ianzishe mashamba makubwa ya kilimo cha kisasa, hapa vijana wengi skilled kwenye kilimo na mitambo watapata ajira na Taifa litazarisha chakula kingi ambacho tutauza nje na kingine kubaki kwenye akiba yetu.

Kupitia zana za kilimo zitakazozalishwa na JWTZ kama nilivyoonyesha juu hapo maana yake wakulima wetu nao watanufaika na kuachana na kilimo cha kizamani na uzarishaji wa chakula utakuwa mkubwa sana.

Serikali sasa, itoe kipaumbele hata Kwa kuweka hela kwenye madini ya chuma pale Liganga, tukichimba chuma na kuwa na chuma maana yake sasa hii skilled workforce tutakayokuwa nayo mitaani itajikita kwenye uzarishaji rahisi wa bidhaa za vyuma, maana yake gharama za uzarishaji zitakuwa chini maana chuma kipo hapa, bidhaa nyingi zitazarishwa na hawa vijana na kuuza nje, ajira nyingi zitatengenezwa na serikali itaingiza pesa nyingi kupitia exportation ya hizi bidhaa za chuma.

Ukishakuwa na Chuma na Gharama za umeme ukashusha Kwasababu tutakuwa automatically na Stieggler maana yake hawa vijana wengi tutakaokua nao ambao ni skilled watakuwa na uwezo wa kucompete kwenye world market Kwa kuzarisha cheap products.

Mwisho kabisa serikali iachane na mentality ya kukusanya kodi tu kwenye uchuuzi unaofanywa na watu wake, ijikite kutumia population ya vijana na watu wengi wenye nguvu kufanya uzarishaji (kuzarisha bidhaa) kupitia viwanda vidogovidogo, hili linawezekana kwa kuweka miundombinu sahihi kama kuwa na mfumo mzuri wa elimu utakaozarisha skilled workforce, kulifanya jeshi JWTZ kuwa more productive na kuajili hawa skilled workforce, kuhakikisha gharama za usarishaji zinakuwa chini Kwa kuweka nguvu kwenye uzarishaji wa chuma, umeme na maji vya kutosha.
 
Kilimo na masoko ya uhakika,kila mara wakulima wakiweka nguvu kwenye zao flani mwaka huo bei inakuwa mbovu. Parachichi zinaoza hovyo wakati soko halijulikani. Uchumi wa uvuvi uzinagtiwe na ulete tija.

Vijengwe vitaru vya kuzalisha sato ndani ya mazingira ya asili kama kule Lamadi na kwingineko.
Kilimo cha mbao ngumu kiimarishwe na kuboresha muda wa uvunaji

Gesi ichakatwe ili iuzwe kwa bei nafuu na lolipelekwe kwenye uzalishaji wa mbolea kuepusha uagizaji nje
Fitna zipungue na husda kwa wenye nia ya kuimarisha uchumi.

Tuwekeza kwenye zao la mahindi kwa wingi nchi jirani zote ni soko mpaka sudani kusini na visiwani shelisheli
Natamani kuona tunazalisha Michele supa na kuupeleka Canada

Ngano izalishwe kwa wingi na bidhaa zake ziwe za kutosha kuepusha kuagiza nje,pia mapato ya makaa ya mawe tujue tija yake.Serikali isijenge Barabara kwa Kasi kuliko kuwekeza kwa watu.

Tuangalie.pia kupunguza ugonjwa wa kamati na afya ya akili.watu wanacheza sana kamali.
 
1. Kuondoa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kwny ofisin za umma!
Kuna viongozi wengine ambao wamefunga Fursa za vijana kwny ofisi za UMMA mfano mawaziri,makatibu wakuu,wakuu wa idara muhimu Kwa mfano NSSF ,PSSSF, Wakuu wa Vyuo vikuu nchini,idara ya Sensa na Makazi.Itungwe sheria ambayo itawapa vijana Fursa ya kutoa mchango wao Kwa taifa lao na pia Fursa ya kugawana keki ya taifa Kwa usawa. Ikumbukwe Baba wa Taifa Mwl J.K Nyerere amekuwa Waziri wa Tanganyika na Baadae Rais wa Tanganyika akiwa na miaka 39 na 40 mtawalia Kwa hivyo msiseme vijana hawana uwezo Wala uzoefu.

2. Benki na Taasisi za fedha ziwekewe mazingira wezeshi ya kufanya kazi na vijana.
Ukweli ni kwamba vijana ndio kundi kubwa ndani ya jamii na nchi Kwa hivyo tunapopanga maswala ya fedha lazima kipaumbele Cha kwanza ni kuwafikia walio wengi na kundi Hilo ni vijana! Nini kifanyike?! Sheria,Kanuni, Taratibu,Sera na miongozo itolewe Kwa Benki na Taasisi za fedha nchini kabla ya kupewa fedha za mikopo inayolenga kukuza uchumi na uwekezaji nchini.

Hapa lazima tuwatungie sheria ngumu na zenye adhabu Kali Kwa kukiuka masharti Kwa mfano mkopo maalumu utolewe Kwa vijana(watu) wenye umri kati ya miaka 18-45 na ambao sio watumishi wa UMMA na mkopo huo uwe na riba ndogo na kuwe na taasi maalumu ya kufatilia wanufaika ikiwemo kuwapa ushauri,elimu na uzoefu katika uwekezaji waliopanga.Mikopo yote iwe na bima na pia biashara za hao vijana ziwekewe bima ili kuwasaidia wanapopata misukosuko.Hii itafanya Benki nyingi zifanye kazi na vijana wasiokuwa na ajira rasmi kama watumishi wa UMMA ambao Kwa idadi Yao hawaongezi Pato jipya Kwa taifa zaidi ya kunufaisha mabenki tu.

3. Tuwekeze kwenye ujuzi na sio taaluma tu Kwa vijana wetu wakiwa bado wadogo kabisa.
Hapa maana yangu ni kwamba vijana waandaliwe kuwajibika au kuingia kwenye soko la ajira na kujiajiri wakiwa bado wadogo Kwa mfano kila wilaya na ikiwezekana kila kata iwe na Centre za Serikali Kwa ajili ya kuwapa vijana ujuzi mara tu wanapohitimu hatua Fulani ya elimu kuanzia darasa la saba Hadi chuo kikuu na elimu hii iwe na mwendelezo Yani tuwe na mhitimu wa darasa la saba anaeweza kushona nguo kwny chereani na tuwe na mhitimu wa degree anaeweza kujenga nyumba na sio mhandisi wa ujenzi! Ule mwaka mmoja anaposubiri matokeo ndio mahala pake kijana asikae kizembe nyumbani baada ya kuhitimu. Na elimu hii itolewe Kwa lazima na bila malipo.

Hii itasaidia sana vijana wa kitanzania kujiajiri wenyewe wakiwa bado wadogo na kuzalisha bidhaa nyingi ambazo tutazitumia ndani na nje ya nchi na kudhibiti uagizaji holela wa bidhaa za nje ambazo tunaweza kuzalisha nchini! Kwa hapa Serikali Kwa kushirikiana wadau wa maendeleo Wana wajibu wa kutekeleza.

4. Kufuta nafasi za viti maalum bungeni hii fedha ipelekwe Kwenye mfuko maalumu wa kushughulikia matatizo ya ajira Kwa vijana.

Hapa najua nitagusa wenye mamlaka na hawapendi lakini ukweli ni kwamba mtoto wa kike anachopaswa kupewa Kwa sasa ni Fursa ya pekee kwenye elimu na sio mpaka kuingizwa bungeni kama ilivyo Sasa.Hivi ni nani Sasa hivi atamchagua mbunge mjinga sio kielimu ila Kwa utambuzi wa matatizo ya jamii na suluhisho mbadala Kwa kigezo tu eti ni mwanaume na amwache nwanamke shupavu labda iwe ni Kwa njia ya rushwa tuu. Kwa hivyo pesa hizi zitafungua Fursa nyingi kwa vijana kuliko hizo nafasi mia na kadhaa zinazotumia pesa nyingi bila mafinikio sawia. Ni ukweli mchungu lakini lazima tukubaliane nao.Dada zangu wabunge mlioingia Kwa njia hii naomba mnisamehe lakini na nyie muwe na huruma Kwa vijana wenzenu.

5. Kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ndani na kuteka soko la nje.
Hapa Waziri wa fedha, Waziri wa kilimo na Uvuvi,Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Waziri wa Biashara, Waziri wa Ajira, kazi na maendeleo ya vijana,Waziri wa Elimu na Ufundi na Elimu ya juu,Waheshimiwa mabalozi,Vyuo vya Ufundi,Taasisi za fedha, lazima muwe na dirisha la pamoja shirikishi Kwa ajili ya uanzishwaji wa Viwanda vipya,ufufuaji wa Viwanda vya zamani ili kuzalisha bidhaa nyingi ndani ya nchi na zenye ubora wa kitaifa na kimataifa huku mabalozi wakitutafutia masoko nje ya nchi.Hatua hii inapaswa ifuatwe baada ya kufanikisha hoja yangu ya Tatu hapo juu.

HITIMISHO
Hizo ni hatua chache tuu ambazo nimezianisha lakini zipo nyingi sana na Kwa uwezo wa Mungu nitaandaa andiko maalumu ambalo nikikamilisha ntakabidhi mamlaka za juu za Serikali ili wazichambue waone wapi pa kuanzia na Ikiwa dira ya maendeleo haijagusa haya mambo bado tunaendelea na tatizo hili Kwa kiwango Cha juu zaidi!
 
Back
Top Bottom