Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Hivi wadada wakiambiwa tufanye harusi ndogo tu watakubali?
 
Hawa waoaji na wanaoolewa hata ukiwaambia huna hela wanaendelea kukusumbua.
Urafiki unageuka kuwa uadui, kipato changu chenyewe ni kidogo hakinitoshelezi, halafu jitu linatoka huko linaniambia nilichangie, as if na mimi ntakuwa nanufaika usiku na huyo mkewe.
Nimechoka na maombi yenu ya michango ya fedha kwa ajili ya harusi.

mkuu kama ulioa kwa kuchangisha michango na we changa.Natumaini anayekupa kadi ya mchango anakufahamu na we wamfahamu .so changa.
 
Shika msimamo wako, yaliyopita si ndwele
Kinachokuliza nini,au ujaoa.Lakini unapenda kwenda kwenye harusi ukale ambavyo ujachangia,Mkuu ndo matumizi.KAZI OMBA ALLOWANCE YA ENTERTEMENT Hini upate ya kuchangia watu.
 
Hawa waoaji na wanaoolewa hata ukiwaambia huna hela wanaendelea kukusumbua.
Urafiki unageuka kuwa uadui, kipato changu chenyewe ni kidogo hakinitoshelezi, halafu jitu linatoka huko linaniambia nilichangie, as if na mimi ntakuwa nanufaika usiku na huyo mkewe.
Nimechoka na maombi yenu ya michango ya fedha kwa ajili ya harusi.

Duhh umenena kweli Kiranja,
Kama kuna kitu kinanikera siku hizi ni michango ya harus jaman na vikao, mana usipoangalia weekend nzote unakuwa busy na vikao tu,

Aaagrrr inaudhi sana, vingine kuacha kuchanga inakuwa ngumu hawakuelewi. Hata kama walinichangia ni miaka hiyooooo nlishalipia. Huu utaratibu sijui ulitoka wap?

Haya
 
Utamaduni huu sijui umetokea wapi?

Hata sielewi,,

Nlipenda ya jamaa mmoja alioa juzi, yeye aliita marafiki zake zaid kama 9, akawaeleza ili waweze kumsaidia majukumu mengine. Lakin marafiki wale wakataka japo nao wamchangie hata kidogo wakatoa michango yao, mwisho jamaa kamalizia na wengine wakaalikwa ukumbini.

Ss wengine budget 8-10m, akiulizwa bwana harusi unakiasi gani umeandaa 1m, yaani hizo 7 zote ndo wachangiaj mhhhhhh.

Ndo maana ndoa cku hizi fashion..
 
Kuchangia si vbaya unapoona unao uwezo.
sijawahi kusoma maandiko msaada uwe ni lazima....!
Shughuli zangu hua najipanga mwenyewe....kisha nazipeleka taarifa kwa ndugu na jamaa ...nao bila hasira wala woga wanahudhuria ...Tunasherehekea vzuri.
Ukisubiria michango utapoteza muda wako...pia utaongeza uadui(chuki)....japo watakusaidia!
Nimewazoesha nao hua hawanilazimishi kuchangia...japo hua wakinipa taarifa za shughuli zao.
Pia ntachangia kwenye matatizo si kwenye sherehe!
Mtazamo wangu!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Mi nimeshapoteza marafiki wa3 kisa sijachangia harusi zao. Hata nilipowatumia ujumbe wa pongezi baada ya ndoa hawajanijibu. Jamani kwani kuchangia harusi lazima?
 
Mkitaka makubwa lazima michango itazidi. Mnataka Kicheni pati kabla ya harusi , baadae harusi shamra shamra zake kubwa kupita uwezo. Ni aibu mtu kwenda kuomba omba wakati atanaka kuoa inaonesha hayuko tayari kuweka mke ndani ya nyumba. Mwambie rafiki yako kuwa unataka kuowa na yeye ataona ni zawadi gani akupe. usizidishe kumpangia kiasi cha fedha au kitu gani akununulie.

Nakumbuka zamani mtu anakwenda kuchukua mke wake , wanafanya sherehe za wastani na kumpandisha baiskeli kumleta kwake - mambo yalikuwa safi kabisa hakuna kero wala kujitia presha.

Kuiga kunya kwa tembo kupasuka msamba !!
 
Hawa waoaji na wanaoolewa hata ukiwaambia huna hela wanaendelea kukusumbua.
Urafiki unageuka kuwa uadui, kipato changu chenyewe ni kidogo hakinitoshelezi, halafu jitu linatoka huko linaniambia nilichangie, as if na mimi ntakuwa nanufaika usiku na huyo mkewe.
Nimechoka na maombi yenu ya michango ya fedha kwa ajili ya harusi.

Mkono siku zote unatakiwa uguse pale unapofika, vinginevyo utaishia kujiumiza. Kama huna sema sina atayetaka kukuelewa atakuelewa na asiyetaka kukuelewa na kujenga uadui kwa kukosa mchango wako basi na iwe hivyo. Mtu kama huyu si rafiki wa kweli kama ni rafki wa kweli atahakikisha anadumisha urafiki katika shida na raha na ukimwambia huna atakuelewa. Hakuna miti ya kwenda kuvuna ngawira na vipato vya Watanzania wengi vinafahamika.
 
changia unachoweza hata elfu 20 inatosha kwa mtu asiyekuhuu sana..kama wa karibu unaweza gonga elfu 50..mambo ya ku-pledge kilo ngapi sijui au kuchangia halafu unaumia ndani ya moyo siyo kitu kizuri.
Muhimu zaidi kama unaoa uwe na list ya watu wanaokuchangia send-off na harusi ili ikitokea kumchangia mtu fulani unaangalia list kama reference..mtu hajakuchangia, mpotezee!!
Bora hii adha siipati kabisa mana mjini payroll ya mwezi unaweza kuwa unamalizia kwa michangoz..
 
Aaah! siyo lazima? Mtu akileta kadi ya mchango kwa ajili ya upungufu wa kupeleka watoto shule nafikiri nitakopa kusaidia ili mwenzetu asiadhirike. Harusi nini bwana? Starehe yako na mkeo usumbufu kwa wenzako.

Siyo lazima, mimi siletewi kadi.
 
Mbaya zaidi unaletewa kadi ya mchango ya mtu usiyemfahamu kabisa aliyeileta ni rafiki yako wa karibu na kiwango cha chini unatajiwa, hii haijakaa vizuri.
 
Hawa waoaji na wanaoolewa hata ukiwaambia huna hela wanaendelea kukusumbua.
Urafiki unageuka kuwa uadui, kipato changu chenyewe ni kidogo hakinitoshelezi, halafu jitu linatoka huko linaniambia nilichangie, as if na mimi ntakuwa nanufaika usiku na huyo mkewe.
Nimechoka na maombi yenu ya michango ya fedha kwa ajili ya harusi.

...ha ha ha, changia biblia au msahafu. Waambie huo ndio uwezo wako!
Issshhh....eti utanufaika na mkewe, he he he!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom