Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

  • Kuchangia maswalwa ya msingi hapana ila upuuzi wa kuchangia starehe za watu number moja Sherehe ya kwake yeye aangaike mwenyewe afanikishe wakiachana mbona hawafanyi divorce party ovyooooooh
 
Sawawa muulize kwanza mie jana ckuenda harusini eti ckuchangia msimamo wangu ni houhuo kwani harusi mpaka ufanye sherehe kubwaaaaa,then munaishi maisha ya ajabu ajabu tu apo ndani hiyo pesa c wawekeze mahali iwasaidie
 
VOR

Umeanzisha maada ya msingi sana, ambayo for sure of recent imekuwa inanigusa sana, ikafikia nikaanza kufikiria upande wa pili as far as 'harusi' ceremony is concerned.

Binafsi, as per mwishoni mwa mwezi huu napaswa kutoa kama Laki tisa kama mchango wa harusi, kuna wa my cousin, kaka apo, mates wa kibaruani etc, wengine n elfu hamsin hamsin na laki laki tu...just imagine! mm take hm yangu hata haizid laki sita..wat do u think?

My take
Wengi tunafanya vitu kwa kuiga tu, kutaka ufahari kwa vitu ambavyo ni less important, maisha yanakuwa magumu siku hadi siku huku majukumu yakiongezeka, lazima tubadilike..mtu kwa account yako huta hata 1M..unabak kutusumbua na harusi ya watu mia tatu ukumbi sijui Deluxe?, y dont u make somthing simple tu?, ni sifa za kijinga na kuweka historia unakuwa unataka mtu.
Sijaoa bado, nategemea kufanya hvo miaka kadhaa ijayo, nimejifunza mengi kupitia haya ya ndugu na marafiki kadhaa ambao wameshafanya hvo, for sure i will make something simple and presantable kuliko kubaki na madeni kibao after marriage. It sucks indeed!

Wito wangu, ni kwamba ni vema tukajifunza na kukubali kubadilika kutokana na kubadilika kwa kasi kwa maisha na hali halisi ya sasa, maisha ya kuigana hayana mshiko ktk karne yetu wandugu.

Ni mtizamo tu, naomba msijenge chuki.
 
Harusi yangu nilifanya mie na mke wangu, Hakukuwa na mchango wowote, niliwaalika wanafamilia na marafiki wachache. Harusi ilipendeza sana, walikula na kunywa kwa nafasi na vinywaji walibeba.

nafikiri kuavoid michango watu wafanye kama wewe vinginevyo kila siku watu wataishia kulalamika
 

Nakuunga mkono 100%. huu ni upuuzi na unatuonesha ni vipi tulivyo wajinga. Hivi mnaoana kwa machango ukiambiwa uchangie mume/mke wako na waliokuchangia kuoana utakubali? Nadhani ukikataa utakuwa mwizi wa fadhila. Ukubali tu kuchangia mume/mke kwa waliowachangia kuoana.
 
VOR! Maada hii imenigusa nitawashrikisha kisa kimoja amabcho hicho na vingine vingi vimenifanya mie nipunguze kabisa ushabiki wa hii michango bila kuangalia ni nani!

Kuna familia moja ilikuwa na binti anaolewa hapa nmaanisha kuwa wazazi wa huyu binti pamoja na ndugu zao! sasa ikiwa umebaki mwezi mmoja Baba mkubwa wa binti huyu akaugua, na ikafikia mahala inatakiwa apelekwe KCMC ; kechekesho ni kuwa wakati kule kwenye michang ya send off kukiwa kumeshamiri na wamebakiza kiasi kidogo wafikie malengo ...............kwa mgonjwa zilipataikana fedha chache sana kiasi kwamba Mama mkubwa alizazmika kuuza baadhi ya mali zao ili ampeleke mumewe kwenye matibabu, kisa hakikuishia hapa siku kabla ya send off kuka kunahitajika pesa nyingine za vipimo na matibabu zaidi.......ilishindikana kwani kilichokuwa kimebaki ni nyumba ikiwa vitu visivyo na thamani na ndimo watoto wa baba mkubwa walimojihifadhi, ndugu walipogeukiwa kwamba watoe msaada ........walimjibu mama huyo kuwa wao wamechoka na ikibidi amrudishe mgonjwa aje kufia nyumbani! Send off ikaendelea na siku 2 baada ya send offf yule mzee yaani Baba mkubwa akafariki.........................wapwaz na mabinamz huku ndiko utu wa baadhi yetu ulikofikia linapokuja suala la hizi sherehe..................Mungu atusaidie sana! Asante VOR kwa kujitoa kwako!
 
huu ni ujinga kabisaaa,,twataka mambo ya kifahari wakt uwezo huna ya nn?haruc co lazima watu wanywe mpaka wasaze huu ni ulimbukeni kabisa andaa shughli kulingana na uwezo wako uliokuwa nao,,,
 
Kwahiyo watu wanaanza maisha baada ya kuoana sio? maana yake ni kuwa ikiwa mtu hakuwahi kuoa wala kuolewa anakuwa hajawahi kuanza maisha, na hivyo anakuwa hajawahi kuishi sio?

Yeah tunapata kazi za mabar maids, wabeba soda na wabeba box vilevile

mtoa mada anazungumzia maisha ya ndoa , kuna tofauti kubwa sana maisha kabla ya ndoa na maisha baada ya ndoa .
 
no acheni tuolewe kwanza ndo mlete hizi mada zenu hapa!!
Tatizo hii ni vicious cycle yaani hata ukiolewa haitakwisha bali utabaki na madeni (tena wale waliokuchangia laki tano tano..) kuna siku itabidi urudushe hizo laki tano tano.., Je kweli ni uungwana harusi yako kamati inachangisha mchango wa milioni 50 wakati labda milioni nne zingetosha..?

Kweli ni uungwana yule best yako sababu anashida ameshindwa kuchanga na asije kwenye ndoa yako wakati yule rafiki wa rafiki yako wa rafiki anaefanya nae kazi ambae humjui ndio aje sababu tu kachanga..?

Je kweli ni uungwana baada ya wewe kuondoka zako wazee wako wabaki na madeni ya kulipia kadi za harusi za watu waliochangia.. (alafu hapa kumbuka kama mtu alitoa laki 5 usitegemee atakuelewa kama wewe utatoa elfu 30).., na hii nimeshuhudia mtu anaenda saccos kuomba mkopo ili achangie harusi ya mtoto wa rafiki yake ambae na yeye alimchangia...

Kwahiyo utaona rafiki yangu kwamba hapa tunaendekeza umasikini na kurudishana wote nyuma..., mtakapoanza michango ya kununua viwanja, kuchangishia biashara, elimu n.k. hayo ndio maendeleo lakini sio kuchangishana kuvuja mali...!!!! na sio kweli kwamba kusherekea ni mpaka watu wanywe mpaka wasahau mlango upo wapi, kama fungo halitoshi nenda kijijini kafunge ndoa ya kawaida au ita marafiki wachache kwenye tafrija na kila mwenye miguu aje kanisani / msikitini au serikalini.. kushuhudia ndoa
 
Kutoa mchango wa harusi ni hiari sio lazima.
uoni kwamba sasa hivi bila kuchanga hupati kadi na kadi imekuwa kama kiingilio.., vipi wale marafiki zako wa karibu sana ambao hawana hizo minimum amount za kuchanga je wasije...!!??

Na kutokuwepo kwa watu wako wa karibu huoni kwamba ina defeat the all notion ya kusherekea na kushuhudia kwa watu wako wa karibu, pia huoni kwamba kwa kuweka kadi kadhaa na michango kadhaa mara nyingi hata ile amount inayotakiwa huwa inapitwa..?, na kesho au keshokutwa atakaekuja kulipia hio loan ya michango ni hao wanandoa (sababu sio ustaarabu kama mtu alitoa kwako na wewe usitoe kwake..)

Ni kwamba sasa ishakuwa nikune mgongo nikukune kisigino...!!! hakuna cha kuchangia kwamba shughuli ili iwe nzuri, bali ni kuchanga ili nikanywe na kusaza na yeye aje achange huyu mjukuu wangu atakapoolewa
 

sie wengne rahaaa ukitaka ufahari weye mwenyewe! Watu wanatakiwa wale na kunywa basi! Ukijumlisha na mahari lets assume labda ni laki 7 ukichukua laki 3 ya watu kula one mil kwisha...nyie wenzetu wa kanisani huwa nawahurumia cost hazkwepeki.
 

Nimeipenda sana hiyo. Kuchangishana noma bana. Maisha yenyewe magumu haya.
 

Ila huu kweli ni upuuzi, mtu huendi kwenye harusi ya kakaako mtoto wa shangazi kisa huna sh.20000 ya mchango,

mie nadhani mambo yakipemba yanafaa mtu unaoa kwa mahari ya sh. 2000 na kisha mnapata kijikombe cha chai na andazi basi shereh imeisha mnatawanyika. Ukipiga hesabu gharama ya sherehe nzima unakuta sh 30000 tu.
 
Wandugu nimejiuliza mara nyingi nini hasa umuhimu wa sisi Watanzania kuendekeza swala la michango hususani ya harusi, na vicheni pati, imekuwa kama sehemu ya desturi siku hizi kuona mtu anapotaka kuoa kuitisha vikao na kupanga bajeti mpaka za milioni 25 kwa harusi ya siku moja tuu.
OK! ni sawa na watu wanachanga, lakini mwisho wa siku wewe unaechangiwa unakuwa na deni na hii ikimaanisha shughuli yako ikiisha utaanza na wewe kupokea kadi mbalimbali za michango wakati mwingine unaweza letewa kadi tano kwa mara moja na zote hizo unapaswa uchangie, mbaya zaidi wanakuwa wamekuwekea na kiwango kabisa,
Wakati mwingine mmoja wa watu waliokuchangia anaweza akaja kukuomba mchango kufanikikisha harusi ya rafiki wa shemeji yake na mathalani shughuli yenyewe inapangwa kufanyiwa mkoani.
Hawajali hali yako wanachojua kwakuwa walikuchangia na wewe unapaswa kuchanga! hawakumbuki vyakula walivyokula na vinywaji walivyokunywa na vingine kubeba kwenye pochi zao, watakachotaka ni na wewe uchange.
Kwanini uishi kwa stress? uiogope hata simu yako inapopigwa namba ngeni? ukimbie kila unapowaona wazee wa michango? fanya maamuzi!
Nionavyo;
Tuamue sasa kama wasomi na kama generation mpya, bora ufanye shughuli ndogo, ambayo ipo ndani ya uwezo wako ukikwama bora ukope bank, au uombe msaada kwa ndugu zako wa karibu, hii itakufanya uwe huru kwani hutalazimika kuchangia watu wengine wanaotaka sherehe kubwa za sifa.
.Tuchangie mambo ya lazima kama misiba na Elimu, kwani unapomchangia mtu kuweza kupata elimu yake unakuwa umewekeza ili mtu huyo aisaidie jamii yake, na kukupunguzia mzigo. Wakenya wana ile kitu wanaita Harambee ambayo imewasaidia wengi kupata elimu.
.Wengi watachukizwa na msimamo wako lakini watakuja kuelewa siku moja, kwani ni matumizi mabaya ya raslimali, kuteketeza 25ml kwa siku moja tuu.
.Serikali ianze kutoza kodi hizi shughuli ili mwishoni watu waachane na anasa hizi.

Kama nimekukwaza nisamehe bure, lakini hivyo ndo nionavyo mimi.
 
Najua ni matatiz ya Maisha ndo yamekukuta kifedha zaidi.. Lakini unakumbuka kwamb hata we kweny harus yako kuna watu uliwakwaza kwa michang ya harus yako.. Fanya Kazi kwa bidii,uongez kipato chako,vi2 kama hv viskusumbue.. Acha kulalamika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…