Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
"FEIS BUKU" kabisaaaaaaaa umesadifu jina hapa.no acheni tuolewe kwanza ndo mlete hizi mada zenu hapa!!
Speak with facts..... Je unamjua mr husninyo..... Amesema atafunga ndoa ya mkeka sasa ni nani alimchangia
Harusi yangu nilifanya mie na mke wangu, Hakukuwa na mchango wowote, niliwaalika wanafamilia na marafiki wachache. Harusi ilipendeza sana, walikula na kunywa kwa nafasi na vinywaji walibeba.
katika kumbukumbu zangu mimi Harusi mtu ulikuwa unafanya kwa uwezo wako... unaita marafiki zako na ndugu mnasherekea hicho kilichopo.
Sasa mtu anakuletea Kadi tena ina kiwango.... na Watu hawakuchangii sababu wanakupenda ni kama wanakukopesha kwamba na wao siku yao ikifika na wewe utachanga...
Michango Inafika mpaka mamilioni ya pesa.... watu wanakuja wanakunywa na kula.. wewe na mwenza wako mnaenda kuanza maisha (wengine hata nyumba hamna) na deni la watu kama mia moja waliokuchangia ambao na wewe inabidi uwachangie....
HIVI NI MIMI TU NINAYEONA KUWA HUU NI UPUUZI NA UJINGA... AU KUNA YEYOTE ANAYENIUNGA MKONO.....
sasa wana Jf hebu tushauriane,tufanyeje?kupiga ban hii kitu!kuwe na campaign,au elimu kwa umma,au hadi waje wazungu watuelimishe?
Kwahiyo watu wanaanza maisha baada ya kuoana sio? maana yake ni kuwa ikiwa mtu hakuwahi kuoa wala kuolewa anakuwa hajawahi kuanza maisha, na hivyo anakuwa hajawahi kuishi sio?
Yeah tunapata kazi za mabar maids, wabeba soda na wabeba box vilevile
Tatizo hii ni vicious cycle yaani hata ukiolewa haitakwisha bali utabaki na madeni (tena wale waliokuchangia laki tano tano..) kuna siku itabidi urudushe hizo laki tano tano.., Je kweli ni uungwana harusi yako kamati inachangisha mchango wa milioni 50 wakati labda milioni nne zingetosha..?no acheni tuolewe kwanza ndo mlete hizi mada zenu hapa!!
uoni kwamba sasa hivi bila kuchanga hupati kadi na kadi imekuwa kama kiingilio.., vipi wale marafiki zako wa karibu sana ambao hawana hizo minimum amount za kuchanga je wasije...!!??Kutoa mchango wa harusi ni hiari sio lazima.
uoni kwamba sasa hivi bila kuchanga hupati kadi na kadi imekuwa kama kiingilio.., vipi wale marafiki zako wa karibu sana ambao hawana hizo minimum amount za kuchanga je wasije...!!??
Na kutokuwepo kwa watu wako wa karibu huoni kwamba ina defeat the all notion ya kusherekea na kushuhudia kwa watu wako wa karibu, pia huoni kwamba kwa kuweka kadi kadhaa na michango kadhaa mara nyingi hata ile amount inayotakiwa huwa inapitwa..?, na kesho au keshokutwa atakaekuja kulipia hio loan ya michango ni hao wanandoa (sababu sio ustaarabu kama mtu alitoa kwako na wewe usitoe kwake..)
Ni kwamba sasa ishakuwa nikune mgongo nikukune kisigino...!!! hakuna cha kuchangia kwamba shughuli ili iwe nzuri, bali ni kuchanga ili nikanywe na kusaza na yeye aje achange huyu mjukuu wangu atakapoolewa
Ambacho huwa kinanichekesha ni pale unakuta mtu anapokuomba huo mchango huwa inafika mahali inakuwa kama lazima, kana kwamba ni deni!
Ukweli ni kwamba, Mimi binafsi ni mtu wa daraja la kati, uwezo wa kufanya sherehe ya mil 6, 7 mimi mwenyewe ninao. Ila nilitaka kufikisha ujumbe huu kwa jamii, mimi nilienda kanisani na mke mchumba wangu (sasa mke wangu) jumamosi moja miaka mitano iliyopita, nikafunga ndoa na baada ya hapo tukarudi nyumbani. Sikumchangisha mtu na wala mimi mwenyewe sikutumia hela yoyote zaidi ya shela , suti na pete. Mimi na mke wangu tunaishi kwa amani, nina watoto watatu,
Kaka mambo ya misiba ni shida na mtu lazima mnawajibika kwa hali na mali kusaidia hapa sijaongelea kwamba michango haifai (mtu yeyote aje saa yoyote kuchangisha elimu, nitampa bila shida..... Msiba tena bila mchango kupita mimi mwenyewe nina wajibu wa kuchanga) sasa basi kwenye msiba tunachanga ili kumzika mwenzetu na pesa zibaki kuwasaidia wafiwa (mambo ya sare na tshirt ni ya nini)?
Kuhusu harusi huwezi hukajustify michango.... hivi umeshaona cost ya harusi?, hivi bila kujifanya tajiri ukafanya harusi kubwa huyo mke humpati?, kuna faida gani ya kufuja mali kwa siku moja? extended family hazijaanza leo, mbona zamani watu walikuwa wanafanya harusi bila michango???? Sasa unakuta A anaoa, B yupo kwenye kamati ya michango, na anampa C kadi za michango asambaze, ambazo anakupa wewe uchange ambaye hata huyo A humjui ni nani.... matokeo yake D ambaye ni rafiki wa karibu wa A ila hana pesa za kuchanga anashindwa kuhudhuria kama huu si ulimbukeni ni nini???? Sasa hadi Anayeoa anapewa baadhi ya kadi za ndugu lets say 20, kwahiyo hadi mtu unapangiwa ndugu wa kuja kusherekea.