Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

poleni sana mnaosumbuliwa na hilo tatizo, hiyo michango unatakiwa kuweka utaratibu tangu mwanzo kama ni wa kutoa au sio wa kutoa, ukijenga tabia ya kutokutoa na watu wakalijua hilo hakuna atakaekusumbua, ila ukijifanya wewe ni baba huruma au unazo wakati umepigika na mambo hayaendi utaumia....fanya maamuzi yako binafsi kwa manufaa ya maisha yako na wala usifanye mambo kwa ajili tu ya kumridhisha mtu mwingine.
 
Hii Thread nimeipenda sana, pia ina mafunzo megi tu!! Nadhani wakati umefika sasa lazima tuseme BIG NO katika michango ya harusi!! Lazima tuwe na pa kuanzia!! Unadai michango kama uliniwekesha pesa sasa unataka nikulipe?? Tuache upumbavu huo?? Ndo maana wa-TZ tuko nyuma KI-ELIMU sana ukilinganisha haswa na jirani zetu wa Kenya!! Wao wanachangia elimu, matibabu na siyo upumbavu huu!! We need to change our mind set!! It can be done, and really that old-fashion mentality need be abolished immediately!!

Nawasilisha!! Siombi samahani kwa walokwisha sambaza kandi, wenyeviti wa kamati, wanaochukua kazi mbalimbali za harusi, nakadhalika kwani tumesha wajua, ni wajasiriamali hao!!!!! Hawana lolote zaidi ya kuganga njaa zao!!

Utasikia..........Chakula nimajua mpishi mzuri-si mchukue akapike kwako, MC namjua MC bomba - si mchukue ukanywe naye kahawa, Picha za mnato na Video-niachie mimi=Ebo!! nakadhalika nakadhalika...................hao ni wajasiriamali!!

Tuanze sasa kugomea michango hiyo isiyo na mbele wala nyuma!!! Kaaa Mweee!!!
 
haya , mwanangu kaja na CLASS PARTY tsh 10000/=
iko kazi........................................................................

Nmh, mimi nimeambiwa sijui Xmas concert ya tarehe 8dec sh 20,000/= na DVD sh 5,000/= (shuleni kwa Mtoto huko!)
 
kinachotuumiza hapa ni Culture tu hamna kingine.. nisipotoa atanionaje? n.k Lakini uhalisia unabakia pale pale. mtu anaahirisha vitu vya maana na kujinyima ili achangie harusi.ghrrrrrrrrrrrrrr

Mitani haiwezi kukuwa kamwe, na unajikuta umebanwa ktk mtego wa umaskini!
 
Nina mtihani mkubwa mwenzenu; nina niece wangu ambaye amechumbiwa. Wazazi wake wamefariki; nimebaki kama mzazi, msimamo wangu ni kutochangia na kutochangisha michango ya harusi. Sasa nashindwa kumwambia huyo niece wangu, msimamo wangu kwani huenda asinielewe na kuanza kummiss mama yake!

Ofisini kwangu, wanajua msimamo wangu mchango ninayotoa ni magonjwa, elimu na misiba tu!
 
Nmh, mimi nimeambiwa sijui Xmas concert ya tarehe 8dec sh 20,000/= na DVD sh 5,000/= (shuleni kwa Mtoto huko!)

Mkuu Kaunga I can bet ni skuli gani hiyo.
Mie nina vijana wawili pale ila nimewaambia watoto kuwa sichangii hiyo kitu na wamenielewa.
 
Watu wengine jamani huwa hawana aibu,unakuta mtu hamjaonana karibu miaka mitatu siku anakutafuta mnaonana unaanza kufurahi,unashangaa anakutolea kadi ya mchango ha!! kuna watu wanajua kuchuna sura.

wengine hata miaka 10 hamjaonana akipata namba yako2 baada ya salamu anatangaza na shida!lol
 
Nina mtihani mkubwa mwenzenu; nina niece wangu ambaye amechumbiwa. Wazazi wake wamefariki; nimebaki kama mzazi, msimamo wangu ni kutochangia na kutochangisha michango ya harusi. Sasa nashindwa kumwambia huyo niece wangu, msimamo wangu kwani huenda asinielewe na kuanza kummiss mama yake!

Ofisini kwangu, wanajua msimamo wangu mchango ninayotoa ni magonjwa, elimu na misiba tu!

iumweleze tu huyo niece msimamo wako na mfanye sherehe kifamilia na ndugu wa karibu , utakuwa umemfundisha kitu kitakachomsaidia maishani. kweli michango inaudhi mno
 
WAKUU!

Kinacho tusumbua katika hili ni ulimbukeni usio kuwa na kwao. Wanzetu wanachangishana kwa ajili ya elimu na matatizo mengine ya kijamii na si michango ya harusi. Ukiangalia majirani zetu kama Kenya, wanasonga mbele ki elimu kutokana na kusaidiana bila kujali huyu anatoka familia gani. Hata wagonjwa wanao hitaji kupata matibabu zaidi nje ya nchi yao, utakuta wanachangiwa fedha za kuwasafirisha kupata tiba kwenye nchi zilizoendelea kitabibu.

WaTz tumekuwa jamii ya kupenda ufahari na ushindani kwenye mambo yasiyokuwa na tija. Kama ni sherehe, naamini haya ni matakwa ya mtu binafsi, hivyo ujipime mwenyewe uwezo wako na si kuzungukia wengine kisa kuomba usaidiwe kushereheka. Hata huku nchi zilizoendelea, mambo hayo hayapo kabisa. Na kama likitokea, kila mtu na anakwenda na mlo wake.
 
:spy:
Kwa sababu waoaji wameongezeka arusi zirudishwe kuwa jukumu la familia husika, hii ni mhimu sana izingatiwe.

Kweli kabisa inabidi sasa Watanganyika tubadilike, twende na wakati!!! HARUSI + MICHANGO=BIASHARA :spy:
 
kadi hizi na zifananisha na yale matoleo ya kanisani,,alafu baadhi ya makanisa huwa yanapigia prom watu wachangie
 
Hivi kwani mtu ni lazima kuingiza udini katika reply? mambo ya Ramadhaan na E'id yamekhussu nini hapa? mnatakiwa mkue !
 
Nina mtihani mkubwa mwenzenu; nina niece wangu ambaye amechumbiwa. Wazazi wake wamefariki; nimebaki kama mzazi, msimamo wangu ni kutochangia na kutochangisha michango ya harusi. Sasa nashindwa kumwambia huyo niece wangu, msimamo wangu kwani huenda asinielewe na kuanza kummiss mama yake!

Ofisini kwangu, wanajua msimamo wangu mchango ninayotoa ni magonjwa, elimu na misiba tu!

Mueleze kwa upole na mwambie arusi zisizo makubwa huwa zinadumu sana! mimi arusi yangu alikuja sheikh, walii wangu ambae ni baba yangu, mume wangu, mashahidi, wazazi na ndugu wachache tu, na mpaka leo miaka 20 nipo na mume wangu.

Lakini kwa mtazamo wangu michango inadumaza sana! sijawahi kuchangisha wala kuchangia ispokuwa kwa mtu ambae amenigusa sana.
 
Nilichangia harusi moja kubwa sana mwaka jana. Ndoa hiyo ikavunjika baada ya miezi nane, nataka wanirudishie hela yangu.
Afadhali miezi nane, wengine hata wiki haiishi ndoa ishavunjika!
 
Michango ya Harusi ni ujinga namba moja na adui wa maendeleo. imekithiri sana kanda ya kaskazini.
hebu tathmini kuwachangia arusi za watu watano kila mwezi kwa kiwango cha za 30,000 kwa mmoja = 150,000.
yaani unafanyia kazi arusi tu. pmbaf
 
Back
Top Bottom