Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Bora hata tungekuwa tunachangaian mahari mtu akapate mke.[/QUOTE]

Haahaaaa... Kweli mkuu! Au utakuta mtu kwenye msiba wa rafiki yake anatoa ulfu kumi, wakati kwenye harusi alimchangia laki moja.... Nonsense!
 
Mmh! Hii ni dalili kuwa maisha ya watanzania yameanza kuwa magumu sana!
 
Kwanza kabisa, wakuu
hongereni kwa sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar!
Pili, nitangulize samahani iwapo nita-sound vibaya kwa baadhi yetu
kwani binadamu tumeumbwa tukiwa na mitazamo tofauti ktk masuala
mbalimbali.
Leo nazungumzia juu ya MICHANGO YA HARUSI, hasa za siku hizi, nalisema
hili bila kumung'unya maneno, utakuta mtu yuko Lindi, na wewe uko
Mwanza, anadai kakuweka kwenye kamati kuu ya harusi yake na hivyo
kadirio la chini utapaswa kuchangia Tsh. 100,000 na itakubidi uhudhurie
sherehe hizo Lindi ukitokea Mwanza! Piga picha, utakuta mtu mwenyewe
ulikutana nae Advanced Level miaka minane iliyopita na wala haujakutana
nae tena zaidi ya kuongea naye kwa simu kwa interval ya mara moja kwa
mwaka huku mkikumbushiana yalopita!
Harusi imekaribia utapokea sms mara tano kwa kutwa unakumbushiwa juu ya
mchango wako! Usipotoa atanuuuuuna, atakuseeeeema.....! Hii imekaaje
wakuu?
Naomba kuwasilisha.

ifike kipind tuwe tunachangiana watu ambao n staff na wale ambao tunaishi katika current residence!!
 
Wasiochangia hiyo kitu ni wengi sana, ungana nao! Kiukweli inabore. Najuta kwanini nilichangisha watu wakati naoa vinginevyo ningekuwa mmoja wao wasiochangia.

Vinginevyo tukubali kuwa sisi si mali yetu wenyewe, tu mali ya jamii tunazozichangia ktk mambo mbali mbali likiwemo Hilo la harusi na send off.
 
Mimi nimejiapiza mwaka huu sitochangia hata shilingi 10, labda itokee mwanafamilia wa karibu anaoa ama kuolewa.

Nikifanikiwa kutochangia mwaka huu, basi huu ndo utakuwa utaratibu endelevu katika maisha yangu.

Inashangaza sana, mtu anajijua hana uwezo hata wa kupata milioni 2 lakini anang'ang'ania kufanya harusi ya milioni 15.

Iliniuma sana baada ya mwaka jana December kupiga hesabu za michango yote ya harusi na kujikuta nimechangia karibu milioni 1.4 kiasi ambacho ningeweza kufanya kitu kingine cha maana.
 
Mtaji huo kama hujui aise maana hapo inawezekana 50 hivi mlimaliza nae advance level na kama kila mmoja akamwambia amemuweka kwenye kamati hakosi 25 watakao mchangia!Niaminicho mimi kule aliko iwe lindi au sumbawanga kuna kamati sasa ile real ya sherehe kama mwanajamii wa pale so hizi zako wewe na wenzio iwe alisoma nao o level au chuo ni za kwake tuuu!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mimi nimefikia kiwango cha juu kabisa cha upinzani wa michango hata mtoto wa baba mwenye nyumba sikuchanga
 
Ni bora tukaelekeza michango yetu kwenye elimu , tukifanya hivi tutaiona jamii yetu ikibadilika. Kuna mambo kama vile mtoto kashindwa kuendelea na masomo sababu wazazi hawana uwezo au amefeli wazazi hawataki tena kumsomesha. Tuwasaidie watu kama hao na tutashangaa manake jamii itachange mno. Hebu fikiria huo mchango wa laki moja au elfu hamsini tukizikusanya na kulipa chuo au shule wanazosoma wanajamii wenzetu hasa wale walioshindwa kulipa ada kwa sababu ya ukata si tutakua tumeinuana sana.

Harusi sikatai kua tusishirikiane lkn imekua too much mtu anakaa nyumba ya kupanga vyumba viwili halafu harusi bajeti yake ni mil 10, si bora angepewa pesa hii aende akajenge chumba kimoja na aepukane na kero za mwenye nyumba. Kumbuka wanapochanga sio kwamba wanakupenda ile ni biashara na umaarufu . Kama kweli lengo letu ni kumuwezesha kijana anae oa basi tumpe ile pesa yote tuliyochanga na tumshauri afanye kitu cha maendeleo kwake.
 
Kwasasa niko busy na kutafuta hela, jamani niacheni siwezi kuchangia harusi.
 
Hapa nina kadi 3, ila mojawapo ndiyo ya huyo mtu unayemsemea, ambaye tulisoma nae shule moja(na sio darasa moja) twenty years ago.
Najuta kukutana naye kariakoo.kwanza nilikuwa nimemsahau, akajitahidi sana kunikumbusha ili nikumbuke anikabidhi kadi.Sijui haya mawasiliano yataendelea hadi baada ya harusi yake.
 
Mee too inanikera xana nina kadi 4 za workmates wanasema najiwekea hazina ya wachangiaji kwenye harusi yangu while marriage is not on my life plan list
ndoa za dharura hazina guarrantee.endelea kuweka hazina dada yangu nikiwe Sebeko
 
Last edited by a moderator:
Mmmmm! Leo imeletwa ya pili zote hela
Nafikiri tuwashauri watu wawe wanafungia ndoa kwa KAKOBE.'
kama sikosei pale ndoa zinafungwa mara moja kwa mwaka.
wanandoa mnakusanyika kanisani, mnafungishwa ndoa wote kwa pamoja kama vile a graduation ceremony, halafu mnapiga MENU kanisani, na baada ya hapo mnatawanyika.hakuna mchango
 
Kwanza kabisa, wakuu hongereni kwa sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar! Pili, nitangulize samahani iwapo nita-sound vibaya kwa baadhi yetu kwani binadamu tumeumbwa tukiwa na mitazamo tofauti ktk masuala mbalimbali.
Leo nazungumzia juu ya MICHANGO YA HARUSI, hasa za siku hizi, nalisema hili bila kumung'unya maneno, utakuta mtu yuko Lindi, na wewe uko Mwanza, anadai kakuweka kwenye kamati kuu ya harusi yake na hivyo kadirio la chini utapaswa kuchangia Tsh. 100,000 na itakubidi uhudhurie sherehe hizo Lindi ukitokea Mwanza! Piga picha, utakuta mtu mwenyewe ulikutana nae Advanced Level miaka minane iliyopita na wala haujakutana nae tena zaidi ya kuongea naye kwa simu kwa interval ya mara moja kwa mwaka huku mkikumbushiana yalopita!
Harusi imekaribia utapokea sms mara tano kwa kutwa unakumbushiwa juu ya mchango wako! Usipotoa atanuuuuuna, atakuseeeeema.....! Hii imekaaje wakuu?
Naomba kuwasilisha.

Umeandika unasema bila kumung'unya maneno hapa JF.

Wanaokuomba michango nao unawaambia hivyo hivyo bila kumung'unya maneno kwamba michango yao ni kero?

Ulalamishi kwa mambo uliyo na ufumbuzi mwenyewe nao ni kero vilevile, hususan kwa sababu mpango mzima wa kusema bila kumung'unya maneno unaufahamu.
 
Hahaha. Umenikumbusha i met a total stranger in a training. Siku ya pili tu anasema kaunguliwa nyumba huko alikotoka. Ati anataka kupitisha mchango! Nikauliza ni mchango wa kurepair nyumba ama! Manake nyumba imeungua vibaya sana. Nilimueleza wazi mchango wangu ni wa hali. Ukihitaji mtu wa kuongea nae im here! Urafiki wa siku 2 hautoshi kuchangiana majanga, wanahusika mnaokula nao raha daily! Nahisi aliniona mchawi japo wengine walimchangia alfu kumi kumi!

Daadek kauzu zaidi ya dagaa!!
 
Ukitaka kujua kujua juu ya timbwili la michango nenda kwa wanajamii wa SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE!!!!!!!!!!!!!
 
Hehehe. Mie siku hizi za uso tu! Mambo ya kugugumia maumivu staki. Ofisini nilishawaambia mambo ya kuchangiana hadi mume wa binamu wa cousin wake shangazi staki! Na mie sichangishi mtu. Kuna mijitu ikienda vikao vya harusi inabeba kadi 20 inakuja kugawa kama sakrament. Akhuu.
Daadek kauzu zaidi ya dagaa!!
 
Wasiochangia hiyo kitu ni wengi sana, ungana nao! Kiukweli inabore. Najuta kwanini nilichangisha watu wakati naoa vinginevyo ningekuwa mmoja wao wasiochangia.

Vinginevyo tukubali kuwa sisi si mali yetu wenyewe, tu mali ya jamii tunazozichangia ktk mambo mbali mbali likiwemo Hilo la harusi na send off.

Ni kweli, kwani mla vya wenzake na vyake huliwa! Si maanishi mnavyofikiri
 
Hehehe. Mie siku hizi za uso tu! Mambo ya kugugumia maumivu staki. Ofisini nilishawaambia mambo ya kuchangiana hadi mume wa binamu wa cousin wake shangazi staki! Na mie sichangishi mtu. Kuna mijitu ikienda vikao vya harusi inabeba kadi 20 inakuja kugawa kama sakrament. Akhuu.

Kwa hiyo siku Kongosho akiolewa/akimuoa Zombie hutachangia...really?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom